Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,575
- 51,373
Akiongea na wananchi wa Mpwapwa Jana, Ndugu Lissu anasema kuwa Wiki takriban mbili amekuwa akishambuliwa "kisiasa" na watu wa makundi matatu kutokana na kauli zake za kuhoji aina ya muungano tulionao na pia kwa kukemea rushwa ndani ya chama.
Amesema kuna makundi matatu yameng'aka kwa kauli zake. Makundi hayo ni Wana CCM kama Mzee Kinana, Amos Makalla na Nape, Halima Mdee na baadhi ya Wanachadema wenzie.
Kundi la CCM limekerwa na Kauli za Lissu za Kuhoji Mzanzibari kutawala Tanganyika na kuwaamulia Watanganyika mambo ambayo ni ya Kitanganyika na wala siyo hata ya Muungano, wakati Wazanzibari kule Zanzibar maslahi yao wameyalinda kikamilifu kupitia katiba yao ya Zanzibar na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kundi la Halima Mdee, Lissu anasema ameshangaa Mdee kaingiaje ktk kukerwa na kauli zake huko Iringa, lakini akasema kuwa kutokana na historia ya Mdee kuhongwa Ubunge hawezi kushangaa kwa nini Mdee Kakerwa na kauli yake ya kujemea rushwa hadharani.
Kundi la Tatu la baadhi ya Wanachadema, Lissu anasema kuwa hilo kundi halikatai kuwa alichosema ni kweli, ila linataka haya aliyoyasema akayasemee ndani ya chama, sirini.
Lissu akajibu hoja kuwa kwa nini ameyasema hadharani. Amesema kuwa.
1. Rushwa ni adui wa haki, ni lazima apigwe vita hadharani na sirini.
2. Pili, akasema kuwa kukemea rushwa hadharani kunawafanya wananchi wajue kuwa chama hakitaki mchezo na rushwa, na hii inakijenga chama zaidi kuliko kukibomoa. Ukikemea rushwa sirini wananchi hawatajua kuwa mnakemea rushwa.
3. Tatu, amesema kuwa Chadema siyo malaika, na pia huko nyuma chama kimeumizwa sana na rushwa kwa viongozi wake. Akasema kuwa Makatibu wakuu watatu wa chama huko nyuma wamewahi kununuliwa, akamtaja Walid Kaborou, Mashinji, Dr Slaa ( Kwa huyu sikubaliani naye, Slaa ni mzalendo aliyekataa rushwa ya Lowasa). Kwa hiyo ni muhimu kuipiga vita rushwa ya CCM dhidi ya CHADEMA sana maana ikiachwa inaweza kuumiza chama zaidi.
Alipotoa hoja hizi, wananchi waliokuwa wametulia wakimsikiliza walionywsha kumuelewa kwa kupiga makofi.
Kazi iendelee