TAKUKURU kuchunguza madai ya Rushwa ndani ya CHADEMA

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
18,848
13,227
Ndugu zangu Watanzania,

Gazeti la Mwananchi limeripoti ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Hamduni amesema ya kuwa watachunguza na kufuatilia tuhuma za rushwa ndani ya CHADEMA.

Rai yangu ni kuwa ni muda sasa Lissu akatoe ushahidi wake wa Vitendo vya rushwa. Maana Lissu ndio amesikika akitoa kauli za kudai kuwa kuna Vitendo vya rushwa ndani ya CHADEMA. Kama alikuwa anaongea bila ushahidi kwa lengo la kuchafua tu watu,basi ajuwe anakwenda kuumbuka sana na kupata aibu isoyofutika.

Sina mengi na sitaki kuwachosheni kwa andiko refu wakati huu ambao mmepumzika baada ya pilika pilika za kutwa nzima. Kwa undani zaidi kamata gazeti lako la mwananchi ulisome vizuri.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

===

Pia soma: TAKUKURU imesema bado inaendelea kuchunguza madai ya fedha chafu CHADEMA yaliyotolewa na Lissu
 
TAKUKURU wenyewe njaa tu huyo Hamduni nae ni pongo tabia zake ni kubambikiza watu bangi na huko TAKUKURU anavuta Sana file za uchunguzi anauza mama anamlea ni uchafu tupu wengine wanakula rushwa wake za watu ili kuzima Masood yao au ya waume zao
 
Kaa kwa kutulia maana naona umeanza kupaniki baada ya kusikia TAKUKURU wanatia timu ndani ya CHADEMA kuchunguza madai ya Rushwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Gazeti la Mwananchi limeripoti ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Salum Hamduni amesema ya kuwa watachunguza na kufuatilia tuhuma za rushwa ndani ya CHADEMA.

Rai yangu ni kuwa ni muda sasa Lissu akatoe ushahidi wake wa Vitendo vya rushwa. Maana Lissu ndio amesikika akitoa kauli za kudai kuwa kuna Vitendo vya rushwa ndani ya CHADEMA. Kama alikuwa anaongea bila ushahidi kwa lengo la kuchafua tu watu,basi ajuwe anakwenda kuumbuka sana na kupata aibu isoyofutika.

Sina mengi na sitaki kuwachosheni kwa andiko refu wakati huu ambao mmepumzika baada ya pilika pilika za kutwa nzima. Kwa undani zaidi kamata gazeti lako la mwananchi ulisome vizuri.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Vipi kuhusu ripoti ya CAG juu ya wizi na upotevu wa mabilioni ya pesa za walipa kodi serikalini, hao TAKUKURU wameshughulikia vipi?!
 
Muziki wa TAKUKURU ni mnene sana... bora ufuatiliwe na polisi kuliko Takukuru.. balaa lao ni zito. CHADEMA kazi wanayo.
 
TAKUKURU wenyewe njaa tu huyo Hamduni nae ni pongo tabia zake ni kubambikiza watu bangi na huko TAKUKURU anavuta Sana file za uchunguzi anauza mama anamlea ni uchafu tupu wengine wanakula rushwa wake za watu ili kuzima Masood yao au ya waume zao
🤣😅😂🤣
 
Ngoja wapewe receipts za tuhuma za rushwa ndani ya CCM zikitoka kwa wana CCM wenyewe tuone kama waliwahi kuchunguza au watachunguza.
 
Inasikitisha sana. Duh.

Yani hata kabla ya Mabilionea wa CHADEMA kujipanga, Takururu ndani🤦🏾‍♂️

Wakishika dola itakuwaje?

Chagua kwa umakini 2025
 
Atajibizana na TAKUKURU huko huko watakapokuja. Msianze kuruka ruka hapa.
Wewe hujielewi. Bahati mbaya sana wewe mwenyewe unajiona mwerevu.

TAKUKURU kama zilivyo taasisi nyingi za Serikali, utendaji kazi wake ni duni sana. Kama hii taasisi ingekuwa inafanya kazi kama inavyotakiwa, mahakamani zingekuwa zimejaa kesi za wala rushwa.

Kwa sasa, sijui utamwondoa nani, maana kuanzia mawaziri mpaka kiongozi wa chini kabisa, karibia wote ni wala rushwa. Kama hajapokea rushwa ni kwa sababu amekosa mazingira ya kudai rushwa. Juzi tu, maofisa wa TRA wamekwenda kwenye kampuni moja na kudai kodi zaidi ya sh milioni 200 iliyotakiwa kulipwa miaka 10 iliyopita, na kampuni ililipa wakati huo milioni 80. Wanadai risiti leo, wakati kikanuni unatakiwa kutunza vielelezo kwa miaka 5, wao wanataka vya miaka 10 iliyopita. Kwa fikra zao wanadhani hakuna vielelezo. Na jamaa wamekataa kuwapa vielelezo kwa madai kuwa muda wa kisheria ulikwishapita, na kuna kaguzi nyingi zimefanyika toka wakati huo, na walikwishapewa tax clearance certificates 3 tomea wakati huo. Hawa wala rushwa nadhani wanaamini kuwa vielelezo havitakuwepo kwa sababu ni muda mrefu. Mmojawao kishawaambia kuwa wampe milioni 30 eti ili wafute hiyo kodi. Kampuni imegoma kulipa hiyo kodi ya 223m, na imegoma kuwapa 30m. Wanawawaangalia waone watafanya nini. Wanasubiriwa angle sahihi, waumbuliwe. Lakini hawawezi kuwaripoti TAKUKURU kwa sababu TAKUKURU nayo imejaa wala rushwa. Ukiripoti tukio la rushwa, nao wanaona wametengenezrwa ulaji.

Nchi hii taasisi nyingi za Serikali zimeoza kama ilivyooza Serikali yenyewe, na uthibitisho ni report ya CAG ya kila mwaka.
 
Back
Top Bottom