Uchaguzi 2020 Lipumba: Mgombea Ubunge Temeke (CUF) alipata kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na familia yake walienda kupiga kura

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
493
1,000
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.

====​
Idadi ya kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa nafasi mbalimbali zina tofauti kubwa na uhalisia. Kwa mfano, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF alipata kura sifuri (0) katika kituo ambacho yeye na wanafamilia yake ya watu 7 walipigia kura.

Aidha, ukichunguza matokeo ya uchaguzi kwa kuzingatia vyama utabaini kwamba matokeo yaliyotangazwa yalikuwa yameshapangwa, na hayatokani na yale ya wapiga kura. Mfano, rejea matokeo ya majimbo ya Dar es Salaam ya Mbagala, Temeke, Segerea na Ubungo. UBAKWAJI huu wa demokrasia ni kinyume na ibara ya 15 (1), ibara ya 16 (1) na ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha UBAKWAJI huu unakwenda kinyume cha maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama Nchi imeyaridhia ikiwa ni pamoja na Azimio la Jumiya ya Madola la Harare la mwaka 1991 na itifaki ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika.
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
7,852
2,000
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.
Kama ziliharibika ulitaka zihesabike kura halali?
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,698
2,000
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.
Anashangaa nini? Maana kuna maeneo wao cuf waliwapa CCM uwakala kwa jina lao. Sasa kweli unampa chui mwana mbuzi akulelee? Amevuna alichopanda.

Huu anaosema ni usanii wake ule ule alioupanga na CCM. Eti anaitisha mfungo wa maombi. Ha ha ha ha ha akaombe mwenyewe nasi tutaomba wenyewe. His a traitor
 
hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,890
2,000
Shabashiiii. CCM hawataiona pepo ya Mungu.
Inawezekana kabisa wapinzani wamesalitiana wenyewe. Usije shangaa ukakutana na masela kibao wa CCM kwenye pepo ya kwanza wamekaa wanatabaruku na malaika kadha wa kadha.

Siasa hizi zinaishia hapa hapa duniani ndugu yangu. Huko mbele Rais ni mmoja tu na hakuna uchaguzi wala kampeni za kisiasa. Either you are in a cool place or hot place. Period.

Msihangaike na ya huku duniani mkasahau ya kule tunakoelekea. Luku vere.
 
Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,041
2,000
Wizi wa mwaka 2020 umekuwa wa kijinga sana. Yaani zile kura za vituoni zilikuwa replaced zote na kura walizoamua kupiga wasimamizi wa NEC.
Yaani kura zote zilizopigwa zilikuwa hazina maana:

Kula zilizokuwapo NEC kimaandishi za kubuniwa zilikuwa million 15
Magu 12 million

Wapinzani wagawiwe zile million 3
Ukijumlisha zote za wapinzani kweli million 3

Lissu alitwambia hili siku ya tarehe 27 pale Kawe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom