Uchaguzi 2020 Lipumba: Mgombea Ubunge Temeke (CUF) alipata kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na familia yake walienda kupiga kura

Aliyekuwa mgombea Kenya Jeremiah Kioni (Makamu wa Rais) hakumpigia kura mgombea Urais Musalia Mudavadi katika uchaguzi. Kituo hicho Mudavadi alipata ziro kabisa.

Huyo mtu wa Lipumba aliipigia CCM asemi ukweli.
 
Huu uchaguzi ufutiliwe mbali, kama kwa urais haiwezekani basi kwa ubunge na udiwani, waluovuruga ndio hao wenye kujinasibu kuhubiri amani huku wakiivuruga wenyewe
 
Kuna kura ziliharibika kwasababu waliweka tiki kwa mgombea wanayemtaka na ili kuonyesha hasira wakaweka alama ya "X" kwa CHADEMA ili kupoza machungu ya matusi ya Lissu, matokeo kura ikaharibika, nawapongeza wagombea wa vyama ambao walikuwa na mfano wa karatasi ya kura ili kuwafundisha wapiga kura wao.

Kuna wakati nilimpgia kura mtu mwingine na kumuacha kaka yangu kwenye uchaguzi wa kiranja mkuu shuleni (nilijua kaka akishinda mama atamsifia sana nyumbani) jiulize kama kaka alidhani naweza kumyima kura...kura ni SIRI ya mtu!
 
Wizi kitu kibaya maana kinakukosesha amani katika maisha yako. Nilifikiri ukiwa na elimu unaelimika na kufuata haki au mtu kama amefikia kuwa level ya judge anaweza kujua haki maana yake nini.

Nilifikiri ukiitwa Askofu au mtumishi wa Mungu unaweza kujua haki. Kumbe kuwaza kwangu si kweli. Wasomi wazuri tu, watumishi wa Mungu wazuri tu, lakini inapofika mahali pa kutenda haki wengi tunashindwa. Shetani akishamwiingia mwanadamu anatoa utu wake na kufanya mambo ambayo hata wanyama hawafanyi hivyo. Hii ndiyo hali ya mwanadamu.

Siwezi kujisifu wala kuwalaumu wengine maana hata mimi inawezekana ningekuwa katika nafasi hiyo ningeweza kufanya hayo hayo wanayofanya. Tukubaliane tu kwamba hiki kizazi ni cha uovu ndiyo maana mtu anafanya uovu mchana kweupe bila kuwa hata na chembe ya aibu.

Na huko tuendako siku za mbeleni, kama Mungu hatarudi na kutufutilia mbali kama Gomora na Sodoma na kuweka kizazi kingine basi tutakulana sisi kwa sisi kama tunavyoanza kulana sisi kwa sisi. Mungu turehemu na wasaidie wenye mamlaka waweze kujifunza kutenda haki.
 
Nimecheka sana hiyo video ya Lipumba, Lipumba anasema jamaa ni hatari zaidi ya Corona.
 
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.



====​

Idadi ya kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa nafasi mbalimbali zina tofauti kubwa na uhalisia. Kwa mfano, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF alipata kura sifuri (0) katika kituo ambacho yeye na wanafamilia yake ya watu 7 walipigia kura.

Aidha, ukichunguza matokeo ya uchaguzi kwa kuzingatia vyama utabaini kwamba matokeo yaliyotangazwa yalikuwa yameshapangwa, na hayatokani na yale ya wapiga kura. Mfano, rejea matokeo ya majimbo ya Dar es Salaam ya Mbagala, Temeke, Segerea na Ubungo. UBAKWAJI huu wa demokrasia ni kinyume na ibara ya 15 (1), ibara ya 16 (1) na ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha UBAKWAJI huu unakwenda kinyume cha maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama nchi imeyaridhia ikiwa ni pamoja na Azimio la Jumiya ya Madola la Harare la mwaka 1991 na itifaki ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika.

Huyu ni wakumuacha sijawai nini anasimamia
 
Back
Top Bottom