Lipumba aondoka nchini baada ya kujiuzulu

Lipumba aondoka nchini baada ya kujiuzulu

UKAWA asili yake sio Lipumba, Mbowe, Mbatia na Makaidi bali ni wananchi waliojaribu kuking'oa CCM toka 1995, 2000, 2005 na 2010 bila mafanikio. Wananchi hao wamegundua kuwa kwa kutumia chama kimojakimoja hawawezi kutimiza adhima yao ya kuleta mageuzi hivyo wakajikusanya nyuma ya ukawa kwa kusaidiwa na akina Lipumba, Mbowe, Mbatia na Makaidi. Hivyo wananchi watamchukia na kumpuuza mtu yeyote atakaeonekana kuipa nguvu CCM kwa namna yoyote na watamshangilia na kumsifu kwa mapambio na vinubi mtu yeyeto atakayeonekana kuidhoofisha CCM kwa namna yoyote ile. Lipumba atawekwa kwenye list ya watu ambao wapenda mageuzi nchini wanawaona kama watu wanaoipa nguvu CCM ili iendelee kutawala nchini, hivyo Prof. Lipumba amejiingiza kwenye orodha mbaya sana katika taifa hili. Hataonja amani ya moyo akiwa nchini au nje ya nchi kutokana na kisa alichowafanyia wapenda mageuzi nchini ambao idadi yao inazidi kuongezeka kila kukicha. Watu watamuita kwa majina yote kama vile pandikizi, kafika bei, mroho wa madaraka, kapokea rushwa, msaliti, n.k. Hii itamkosesha amani popote atakapokuwa
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Wasalamu wanandugu,

Habari nilizozisikia hivi punde ni kwamba Prof. Ibrahim Lipumba ameondoka nchini na ndege ya Rwanda jana baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari.

==========================================



Chanzo: Mtanzania
Amekuwa mkimbizi bila ya sababu za msingi, maana ukawa itakuwepo hata kama yeye akiondoka
 
Acha aondoke maana raia walivo na hasira wangeweza kumfanyia umafia.

Lipumba ni mtu cheap sana kumbe, na ameonyesha siyo mtu makini na ni mtu asiyejiamini, huwezi ukashiriki kufanya jambo baya baadaye ukaamua kuachana na hilo jambo baya kwa kuachia wadhifa wako badala ya kukaa na wenzako mezani uwashawishi kwamba tufanyacho siyo sahihi, unaishia kutoa tamko kama mwanamama 'mkuna mba' eti "roho yangu imenisuta"
 
Unajua mwananchi wa hali ya chini anapolia shida na kumtazama kiongozi wake kwa matumaini kiongozi huyo hupata thawabu kubwa sana, ila yule kiongozi anayewasaliti watu wa chini kwa fedha za kifisadi ana balaa!
 
kama yesu mwana wa mungu pamoja na miujiza yake yote mpaka aliweza kufufua watu yuda aliweza kumuuza kwa vipande 30 vya pesa itakuwa mabilion yaliyotengwa na lumumba kwa ajili ya kubomoa upinzani? sasa lipumba amesha kamilisha mission imposible 1 phase 2 itakuwa kwa dr na wengne secret member waliopandikizwa ktk ukawa toka day 1 bahati mbaya intellgence ya ukawa inapoteza nguvu kuchunguza wengne bt imeshindwa kuwachunguza wale wanaowatuma wakachunguze wengne
 
Katimiza alicho tumwa na ccm lakini as long as mpambanaji wa kweli Maalim Seif yupo... CUf ni imara zaidi na impact ya Lipumba sio kubwa sana.... mwenyekiti msomi ameidumaza kabisa CUF upande wa bara.... msomi gani kashindwa ongeza idadi ya wabunge... wabunge wawili kwa CUF ni fedheha... kaidumaza CUF... mwache aende tu......
 
Yaani Prof alinikwaza sana. Eti huyu hakuwa ukawa kwa hiyo anatetea katiba iliyopendekezwa kwa hiyo roho inamsuta.

Hata babu yangu kule upareni anajua kuwa ukihama dhehebu au chama maana yake unaacha ya huko ulikotoka unajivisha mapya ya huko ulikohamia. Sasa hivi Lowasa ni UKAWA. Nguvu imeongezeka UKAWA halafu Prof. anasema roho inamsuta kwa maana alishiriki uamuzi mbovu. This can not come from a learned person like Lipumba. Na hayo aliyoongea ndio yatamsuta kweli kweli maisha yake yote. Amekisalit chama chake kwa vipand vya fedha.

Nakumbuka aliwahi kusema yeye alimsaidia JK kushinda unchaguzi, na hilo bado analo , bora kasepa.
 
Hongera Lipumba,kwenda mapumziko ni pesa yako sijui wengine kinawauma nini,tujifunze kuheshimu maamuzi ya mtu binafsi.kama hakuna shida hata akitoka matusi ya nini
 
Back
Top Bottom