Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Status
Not open for further replies.
Hivi Watanzania tumekuwa WAJINGA kiasi hiki? Badala ya mtu kujadili hoja anachomekea hoja nyingine juu ya hoja (kama sio viroja ni nini sasa!). Kwanini mtu usianzishe thread nyingine ijadiliwe ama sivyo utuambie kuwa na wewe pia ni MSHABIKI na MNUFAIKA wa UDINI hapa nchini. Namshangaa sana mtu anayeshabikia huu ujinga kwamba Dr slaa alitumia udini mwaka 2010 kwa mantiki hiyo anataka kusema zamu hii ni ya Prof Lipumba?.

Mathalani tuchukulie Dr Slaa aliungwa/anaungwa mkono na wakristu na ni adui wa waislam, then Prof Lipumba anaungwa mkono na waislamu na ni adui wa wakristu the same to JK et al; hivi ni hoja kweli? Ukiwa kama mtanzania hilo ni jambo la kufurahia na kujengea hoja kweli? Hatutekelezi usemi ule kwamba ukimwaga ugal na mwaga mboga? ambao kimsingi ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu! WHAT A SHAME? Badlikeni wakuu, Watanzania tubadilike na tupende kubadilika.

HIVYO basi kama kuna mwanasias yeyote yule anafanya au anatarajia kufanya siasa hizi za kijinga kabisa (KIDINI) anapaswa kupingwa kwa nguvu zote, kukemewa na kuzomewa popote pale alipo, iwe ni Slaa, Lipumba, JK, Lowasa, Membe, Zitto n.k. Hawatufai kabisa. Hoja kwamba flani alifanya hivi mara vile (kutumia udini) sio hoja ni ULIMBUKENI wa ajabu kabisa.

Narudia tena ni UJINGA na ni ULIMBUKENI wa kiwango cha juu kabia. Watanzania wenzangu tuwe tunakemea makosa na kuyakataza na sio tuwe tunahalalisha makosa kwa ushahidi wa kosa. KOSA halihalalishi KOSA kamwe. Tuangalie Tanzania ijayo na tuache kuangalia Tanzania ya miaka 53 iliyopita.
 
Anayosema kweli na ni ujinga kwa kwa kutomsikuliza nchi itauzwa kweli na mafisadi
Awe anaongea msukituni au kanisani ukweli wa kuwepo makuhani wa vibaraka upo
 
Lipumba is no more in politics, kafilisika, kaisha, na atatuletea machafuko kwa tamaa zake za madaraka
 
Lipumba ana matatizo makubwa.Mtatiro bado kijana na amepoteza uelekeo kwasababu ya hawa wafia dini.
Wanaomjua Mtatiro enzi hizo inasikitisha.CUF hawana uelekeo tena.
 
Hivi Mtatiro kapigwa jini????
Anafanya nini CUF?
Je ana mapenzi ya dhati na chama, au ndio ana mapenzi mazito na fungu zito la mahela anayopewa na CUF?
 
Kwa nini awashambulie madj wa Chadema badala ya magaidi wa CCM walioshika nchi?kwa nini azungumzie matatizo yajayo ya kufikirika(ya serikali mpya chini ya Chadema)badala ya kuzungumzia haya yaliyopo sasa chini ya CCM na tunayaona?wenye akili tushamwelewa.akachukue buku 7 Lumumba!
Mkuu, hapa umenena; huu ndiyo ukweli halisi. Na, kwanini Msajili wa Vyama vya Siasa awe kimya licha ya sumu iliyomwaga na huyu bwana alipokuwa kwenye ule msikiti wa awali- msikiti wa Idrisa kama sijakosea; jeshi la polisi wanataka kutueleza kuwa hawaoni hatari ya maneno ya huyu bwana mpaka wawe kimya kiasi tunachoshuhudia!
 
CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!
Tofautisha Maaskofu na Chadema..! Mashekh siyo ccm wala cuf ila Lipumba ni cuf, tean cus asilia
 
Nchi mapande mawili na waloanza ni chadema na maaskofu 2010
Lipumba usirudi nyuma wako waislam bado wamelala tuwamshe ujinga wa kuamini usichanganye dini na siasa haupo tena maaskofu walisha uondoa si mnajua chadema marafiki zao ni vyama vya siasa kali vya kikristo huko ulaya
 
Mmh kazi ipo unaweza ukasoma na usielimike kuitwa profesa na mambo ufanyayo hayalingani na kiwango chako cha elimu unajidhalilisha mwenyewe unadhlilisha Taifa lako unadhalilisha asili yako na imani yako, Lipumba anadhihirisha wazimu kuwa pamoja na elimu yake lakini matendo yake na maneno yake hayaakisi kila alisemalo
 
Lipumba ameishiwa sera na hana mwelekeo wowote zaidi ya kutumika kwa maslahi ya CCM, wengi wanaounga mkono CUF hawayajui mambo haya.Nawashauri ndugu zangu, kama hata aliyepo madarakani ni Mwislamu lakini bado maisha ni magumu kwa wote yaani Wakristo, Waislamu na wapagani bila shaka mtakubaliana nami kwamba suala siyo dini bali malengo ya Viongozi hao na namna walivyokuwa committed.Ngoma anayoicheza Lipumba ni kwa faida ya CCM wala siyo Waislamu!
 
Hii chadema na Hili gazeti la tanzania daima kwa kweli ni janga kwa waislam na uislam tanzania.
Sipendi hata kidogo.
 
Japo naona wengi wanajadili kwa mzaha masuala ya udini,binafsi naona tayari LAANA imeshaikumba nchi na mzimu unaotaka damu ya watanzania umeshika kasi!Katika mioyo ya wafia dini ambao wanazidi kuongezeka kadri ya umaskini unavyoongezeka,kumejaa chuki inayochochewa na viongozi muhimu katika jamii,ni muda mfupi tu unakaribia,watanzania maskini watatolewa kafara wengine wakijifariji wanafia dini,wengine watalazimishwa kujitetea bila kujua wanapigania nini!Wachochezi wote naamini watakuwa salama wakiishi vizuri nje ya nchi wakifaidi utajiri waliojipatia kwa kuwanyonya hao ambao wataachwa wakichinjana.Wale wasiotegemea nguvu ya mabomu na risasi,wanapaswa kumlilia Mungu sana sasa kwa ajili ya taifa hili.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Sina hakika na kiwango cha uwezo wa kuchambua mambo kwa wale wanaoshabikia udini katika siasa za nchi hii. Nikianza na CCM ambao wamekuwa wakijaribu kudhoofisha vyama vya siasa kwa kuvitangaza kuwa vina udini; najiuliza swali gumu moja kwamba hivi mahubiri ya CCM kwamba CDM ni chama cha kidini (KIKRISTO) na ikiwa mahubiri haya yatawaingia wakristo wote na kuyabeba positively kuielekea CDM, CCM itasalimika nchi hii? Labda nifafanue ninachojiuliza; ni kwamba nchi hii ina watu wake wengi katika aidha ukristo au uislam, na ikiwa CCM walishahubiri enzi zile kwamba CUF ni ya waislamu na sasa wanatumia maguvu kusema CDM ni ya wakristo, na makundi haya mawili yakishikilia mahubiri haya ya kuvifuata vyama wanavyoambiwa kuwa ni vyao na watawala wa sasa, CCM itabaki wapi?

Hivi pengine udini walioipakaza CUF ndio unaowatesa CCM kila uchaguzi kule ZNZ? Maana ZNZ kwa asilimia 90 au zaidi ni waislamu!

Nawashauri watu wote wenye mapenzi mema na nchi yao Tanzania tuachane na propaganda za kidini maana tutaigawa nchi hii na kuzaa mataifa angalau matatu tusipokuwa makini! Maana Tukiwaelekeza wakristo wote kwamba nyumbani kwao ni CDM na waislamu wote kwamba kwao ni CUF ni wazi hata JK hatasalia huko CCM atelekea CUF na hakuna hata mmoja kati ya CDM na CUF atakayepata kura za kutosha kuitawala nchi hii kwa amani na kwa kuwa hizi ni dini mbili tofauti basi tutagawana nchi maana hatutahitaji kukaa katika meza moja kuitawala Tanzania iliyo moja!

Wale wasiokuwa wakristo wala waislamu kama Kingunge ndio watabaki CCM pamoja na free masons, wahindu, na wapagani; je, ccm itaishi?

Tuache jamani kushabikia haya mambo, mleta uzi huu sina hakika alikusudia nini lakini mtazamo wangu hajakosea ila ni tahadhari kwamba tusiende huko anakotaka kutupeleka Lipumba. Na hata kama viongozi wa CDM, nasema tena viongozi wa CDM wakibainika kuyafanya haya kule makanisani, kama alivyofanya Lipumba msikitini, tutahitaji kuwakemea kwa nguvu zetu zote. Viongozi wa dini wakiyasema makanisani na misikitini tuwatake viongozi husika kutueleza misimamo yao hadharani...

Niishie hapa tu kwa sasa
 
Mbona siwaelewi? Tatizo sio CCM, TATIZO NI UISLAMU. Ifahamike kwamba, endapo masuala haya ya UDINI ndiyo yanayoingia zaid kwenye siasa za Tznzania, basi si muda mrefu Amani ya nchi hii itatoweka. Enyi Chadema, kama kweli mnadhan Udin ndiyo utakaokipa ushindi chama, hapo mmechemka. Waislamu wa sasa hv, sio wale wa enzi za mwalimu, wanajitambua zaidi.
 
Na wasiwasi na usalma wa taifa pamoja na msajili wa vyama vya siasa. Cdm wakitaka kufanya kitu huwa wanapata vikwazo vingi toka intelijensia ya polisi, usalama wa taifa na hata msajili wa vyama vya siasa, lakini cuf na ccm wapo juu ya sheria hata pale wanapovunja sheria huungwa mkono na vyombo vyote vya siasa
 
CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!

Hapo kwenye red umesema vizuri lakini umeshindwa kulinganisha. Sheikh na Padre/Mchungaji/Askofu wapo kwa ajili ya maslahi ya dini zao, hivo wakisema lolote juu ya upendeleo kwa dini zao ni jambo la kawaida. Lakini mtu anayetarajiwa kuwa kiongozi wa wote kama Lipumba tungetegemea ahimize umoja wa kitaifa si kuwa mshiriki wa kubomoa utaifa wetu. Kama unashabikia kauli ya Lipumba maana yake unataka kutuambia wakristo waliopo CUF wamepotea njia kwa kuwa hawana chao pale isipokuwa waislam?
 
Tofautisha Maaskofu na Chadema..! Mashekh siyo ccm wala cuf ila Lipumba ni cuf, tean cus asilia
Huwezi tofautisha CHADEMA na maaskofu. CDM ni political wing ya KANISA. Nani asiyejua 99% mko CHADEMA kwa sababu Ukristo wake. You can fool nobody!
 
Ziheshimuni dini zetu. Kunyamaza kwetu kusiwafanye mfikiri kwamba hatuoni kwa undani uhuni mnaotufanyia mkijificha nyuma ya dini. Tunataka tuende msikitini kumwabudu Mwenyenzi Mungu. Tunataka tuende kanisani kumwabudu Mungu tu. msituletee propaganda zenu za kisiasa humo.
 
CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!
Weka ushahidi kuthibitisha haya madai yako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom