Dear Next Level,
Bahati nzuri suala hili sio siri. Kama una mashaka, nakuomba uwasiliane na TRA au Wizara ya Fedha au VODACOM wenyewe. Ukiwapata VODACOM waombe wakupe Taarifa zao za Hesabu za kila mwaka (Annual Audited Accounts & Reports) na uzisome kwa ukamilifu wake kisha tutaarifu wana JF. Chanzo changu si TRA wala Wizara ya Fedha wala VODACOM bali Bunge letu.
Vodacom tangia last year wanalipa corporate tax na tangia wanaanza wamekuwa wakilipa other taxes kama excise duty, VAT, Service Levy,SDL,W/taxes etc isipokuwa Corporate tax.Vodacom Tanzanias operating profit was R615 million and EBITDA was R1 049 million for the year, up 33.6% and 37.0% respectively on the prior year with an EBITDA margin of 35.3% compared to 32.5% a year before. In Tanzanian shillings, profit from operations and EBITDA increased by 10.9% and 13.7% respectively. The margin increase was supported by cost containment measures, and lower management fees and fuel consumption.
Vodacom wanalipa corp tax muda sasa.....fanya utafiti....zaidi
Mkubwa SS,
Ulitakiwa ufanye homework kidogo! Nijuavyo mimi, VODACOM wameanza kulipa corporate tax tangia mwaka wa fedha 2007/2008 na mpaka sasa wanalipa kodi hii. Hata Celtel (zain) nao walianza kulipa corporate tax kati ya mwaka 2006 na 2007, mwanzoni walikuwa wanautilize tax losses kutoka miaka ya mwanzoni zilizotokana na capital expenditure kubwa hasa kny minara na mitambo mingine ya simu!
So sio fair kuweka claims ambazo sio sahihi kwa wakati uliopo mkuu! Hata ungetembelea tovuti yao, ungeweza ona wanareport EBIT (Earnings before interest and tax) ambayo ni +ve....though hawaonyeshi ni kodi kiasi gani wamelipa!....ona kwa mfano kaextract haka;
Vodacom tangia last year wanalipa corporate tax na tangia wanaanza wamekuwa wakilipa other taxes kama excise duty, VAT, Service Levy,SDL,W/taxes etc isipokuwa Corporate tax.
Mzee EBITDA ni general terminology ya kihasibu kwenye hesabu zao, kuweka hii haina maana wamelipa Tax au kuna Corporate tax, corporate tax inaweza kuwa ZERO lakini bado ukaweka EBIT au EBITDA.
On the other hand pia bado hakuna uthibitisho kama wanalipa kodi au hawalipi.
Bado sijaelewa kama wanalipa au hawalipi, na kama hawalipi kwa ajili ya ku recoup investments zao (Machineries and equipments) sioni tatizo kwa kuwa income tax act inaruhusu kwa makampuni yote, kufuatana na taratibu zilizopo.
Tufanyeni research ya kutosha kabla ya kukurupuka humu.
Dear All,
Ni matumaini yangu kuwa wote mnafahamu kuwa kampuni ya VODACOM ilianza shughuli zake rasmi hapa nchini mwaka 2000. Mpaka sasa ina wateja wasiopungua milioni 6.
Kitu cha kushangaza ni kuwa kampuni hii haijawahi kulipa kodi ya mapato (corporate tax) toka ianze shughuli zake hapa nchini kutokana na msamaha ambao imekuwa ikipewa na Serikali yetu kila baada ya miaka mitano kuanzia mwaka huo wa 2000.
Kutokana na faida kubwa ambayo wanaipata kila mwaka tunaomba VODACOM ianze kulipa Kodi ya Mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha 2010/2011 (asilimia 30 ya faida ya mwaka).
Tunaomba sana wabunge wetu watusaidie katika suala hili zito na kuhakikisha kuwa VODACOM (T) LTD wanalipa kodi ya mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2010/2011.
Makisio ya kati yanaonyesha kuwa kama taifa tunapoteza shilingi kama bilioni 240 kwa mwaka kwa kuwaruhusu VODACOM kutokulipa kodi ya mapato.
Huenda wana enjoy tax holidays na hata reliefs as a result of the many contributions they are making to communities....
nenda kwenye link hapo chini, halafu chagua statement ya mwaka unaotakaDear Semilong,
Asante kwa hiyo taarifa. Naomba pia utusaidie kujua kiwango cha mapato cha VODACOM Tanzania walichopata kwa mwaka wao wa fedha wa 2007/2008 na 2008/2009. Tutashukuru sana kwa hizo taarifa.
WTZ tuache mawazo ya kutaka hizi kampuni zilipe kodi. Hawa jamaa wanatoa ajira kwa watu kibao, ambao wanalipa kodi. Hii corporate tax ni dhulma kwa wafanyabiashara. Tuwe na mawazo ya kutafuta resources zengine ambazo serikali inaweza ikawa inapata mapato; na si kuongeza kodi. Kumbuka, uchumi mzuri wa nchi ni kuwa na lower taxes, low inflation and low unemployment.
hii siyo kweli mbona wafanyabiashara wadogo walilipa? mbona wafanyakazi hata mwenye mshahara 200k analipa kodi ya mapato? yaani mtu mwenye duka alipe na mwenye kampuni asilipe!
WTZ tuache mawazo ya kutaka hizi kampuni zilipe kodi. Hawa jamaa wanatoa ajira kwa watu kibao, ambao wanalipa kodi. Hii corporate tax ni dhulma kwa wafanyabiashara. Tuwe na mawazo ya kutafuta resources zengine ambazo serikali inaweza ikawa inapata mapato; na si kuongeza kodi. Kumbuka, uchumi mzuri wa nchi ni kuwa na lower taxes, low inflation and low unemployment.