Lini kampuni ya vodacom itaanza kulipa corporate tax (income tax)

Dear All,

Ni matumaini yangu kuwa wote mnafahamu kuwa kampuni ya VODACOM ilianza shughuli zake rasmi hapa nchini mwaka 2000. Mpaka sasa ina wateja wasiopungua milioni 6.

Kitu cha kushangaza ni kuwa kampuni hii haijawahi kulipa kodi ya mapato (corporate tax) toka ianze shughuli zake hapa nchini kutokana na msamaha ambao imekuwa ikipewa na Serikali yetu kila baada ya miaka mitano kuanzia mwaka huo wa 2000.

Kutokana na faida kubwa ambayo wanaipata kila mwaka tunaomba VODACOM ianze kulipa Kodi ya Mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha 2010/2011 (asilimia 30 ya faida ya mwaka).

Tunaomba sana wabunge wetu watusaidie katika suala hili zito na kuhakikisha kuwa VODACOM (T) LTD wanalipa kodi ya mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2010/2011.

Makisio ya kati yanaonyesha kuwa kama taifa tunapoteza shilingi kama bilioni 240 kwa mwaka kwa kuwaruhusu VODACOM kutokulipa kodi ya mapato.


Hivi unajua VODACOM ya nani na ana maslahi gani kwa Mafisadi?? RA ndio jibu analo bye
 
Back
Top Bottom