Lini kampuni ya vodacom itaanza kulipa corporate tax (income tax)

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
409
31
Dear All,

Ni matumaini yangu kuwa wote mnafahamu kuwa kampuni ya VODACOM ilianza shughuli zake rasmi hapa nchini mwaka 2000. Mpaka sasa ina wateja wasiopungua milioni 6.

Kitu cha kushangaza ni kuwa kampuni hii haijawahi kulipa kodi ya mapato (corporate tax) toka ianze shughuli zake hapa nchini kutokana na msamaha ambao imekuwa ikipewa na Serikali yetu kila baada ya miaka mitano kuanzia mwaka huo wa 2000.

Kutokana na faida kubwa ambayo wanaipata kila mwaka tunaomba VODACOM ianze kulipa Kodi ya Mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha 2010/2011 (asilimia 30 ya faida ya mwaka).

Tunaomba sana wabunge wetu watusaidie katika suala hili zito na kuhakikisha kuwa VODACOM (T) LTD wanalipa kodi ya mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2010/2011.

Makisio ya kati yanaonyesha kuwa kama taifa tunapoteza shilingi kama bilioni 240 kwa mwaka kwa kuwaruhusu VODACOM kutokulipa kodi ya mapato.
 
Duh! Kazi kweli kweli. Moja ya mashirika makubwa nchini yahalipi tax! DUH!
 
yaani hapa bongo waajiriwa ndo walipa kodi wazuri kwani wafanyabiashara hulipa kidogo sana pamoja na kuwa na mapato makubwa.
 
Naunga mkono sana hoja yako!cha kushangaza sana TRA ilitoa list ya LARGE TAX PAYERS ya kwanza TBL ya pili ikawa ZAIN,vodacom haipo ktk 5 bora ingawa VODACOM wanatamba wanawateja wengi kuliko mitandao mingine!ndugu SABODO J SABODO aliwahi kutoa takwimu sahihi iwapo income tax itatozwa ktk makampuni ya mitandao ipasavyo basi hatuna haja ya kuomba misaada ya ruzuku toka kwa wahisani!AMA KWELI WATANZANIA BONGOLALA
 
Kutokana na faida kubwa ambayo wanaipata kila mwaka tunaomba VODACOM ianze kulipa Kodi ya Mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha 2010/2011 (asilimia 30 ya faida ya mwaka).

Tunaomba sana wabunge wetu watusaidie katika suala hili zito na kuhakikisha kuwa VODACOM (T) LTD wanalipa kodi ya mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2010/2011.
Hatuwaombi ni suala la lazima kabisa. Mbona sisi wafanyakazi hatuombwi kulipa kodi na kila mwezi wanatukata kodi kubwa sana tena isiyoendana na maisha yetu kabisa. Walipe ni lazima na sio tunawaomba. Huu ni uzembe na udhaifu wa watendaji wetu kwa makampuni ya wakubwa ila sisi wenye vibanda tunafutwa kila kukicha kudaiwa kodi
 
uwiiii!!!!! lord have mercy on us. yani vodacom hawalipi kodi??? kwa nini watumiaji wa huduma zake msigome tu ili kusisitiza walipe kodi? hii no mojawapo ya mass support nzuri inayowezesha kuwafanya hawa watu walipe kodi bwana.
 
MMMM bONGO KILA KITU KINAWEZEKANA.Yaaaani PAYE ilivyo kubwa ktk mishahara yetu midogo.halafu unasikia kampuni kubwa zote,hazilipi kodi kweli inaudhi sana nchi hii.Hivi Caspian inalipa kodi kweli?
 
Dear Next Level,

Bahati nzuri suala hili sio siri. Kama una mashaka, nakuomba uwasiliane na TRA au Wizara ya Fedha au VODACOM wenyewe. Ukiwapata VODACOM waombe wakupe Taarifa zao za Hesabu za kila mwaka (Annual Audited Accounts & Reports) na uzisome kwa ukamilifu wake kisha tutaarifu wana JF. Chanzo changu si TRA wala Wizara ya Fedha wala VODACOM bali Bunge letu.
 
Dear All,

Ni matumaini yangu kuwa wote mnafahamu kuwa kampuni ya VODACOM ilianza shughuli zake rasmi hapa nchini mwaka 2000. Mpaka sasa ina wateja wasiopungua milioni 6.

Kitu cha kushangaza ni kuwa kampuni hii haijawahi kulipa kodi ya mapato (corporate tax) toka ianze shughuli zake hapa nchini kutokana na msamaha ambao imekuwa ikipewa na Serikali yetu kila baada ya miaka mitano kuanzia mwaka huo wa 2000.

Kutokana na faida kubwa ambayo wanaipata kila mwaka tunaomba VODACOM ianze kulipa Kodi ya Mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha 2010/2011 (asilimia 30 ya faida ya mwaka).

Tunaomba sana wabunge wetu watusaidie katika suala hili zito na kuhakikisha kuwa VODACOM (T) LTD wanalipa kodi ya mapato kuanzia mwaka ujao wa fedha, 2010/2011.

Makisio ya kati yanaonyesha kuwa kama taifa tunapoteza shilingi kama bilioni 240 kwa mwaka kwa kuwaruhusu VODACOM kutokulipa kodi ya mapato.
Got any data to substantiate this? Data will be uesful to push for this claim .
 
Ndo maana unapoona wanajifanya wanatumia vodacomfoundation eti wanantoa misaada.....hiyo ni kodi ambayo walitakiwa kulipa na wala hatuhitaji vimisaada vyao kama watalipa kodi inayostahili.

Tatizo kubwa la viongozi wa CCM na serikali yao hata wakipewa pipi na hao makaburu wanashangilia, mbona haya hayatendeki nchi nyingine??? Nchi kama India ukifika wewe mwekezaji unapewa kablasha la sheria za uwekezaji ukiziweza endelea na uwekezaji ukishindwa wanakwambia nenda afrika.
 
NCHI HII VIPI? Hivi kuna wabunge kweli if this is true!!
 
Msishangae kuja kusikia vodacom imebadilisha jina na kujiita jina lingine kwa kisingizio kuwa imeuzwa kwa kampuni nyingine kama ilivyokuwa celtel kwenda ZAIN, halafu hiyo kampuni mpya nayo inaanza kuhesabiwa miaka upya mpaka ifikishe mingine mi 5
bongo bwana yaani watu wanacheza na serikali vitenesi tu.
Viongozi woote mabogazi tu.. wamejazana kwenye payroll ya voda kufunikwa vinywa
 
Back
Top Bottom