Lindi mbona pamepoa sana jamani?

Lindi mbona pamepoa sana jamani?

Siku za kazi ni kama jumapili pamepoa sana,huko angalau jioni kuanzia saa 12 ndo utaona milupo inatoka vitu bei juu.Kuna sehemu zina umaarufu kama Nangurukuru lakini hamna kitu bora Somanga japo padogo.Umbali kutoka Lindi mjini mpk Mitwelo(makazi mapya)ni km10 tu usiku ni milio ya fisi wenyeji washazoea!
Hivi mitwero Kuna sifa ipi mkuu, maana nasikia sana Mitweromitwero.. Nako ni town kama pale Lindi Mjini kati..?
 
Huko Kunafaa mkuu, maana hiyo miradi ikikamilika kutanoga zaidi..
Hebu nitafutie kiwanja huko
Ndio mzee, pia ndipo imejengwa hospital ya Rufaa ya mkoa. Pia itajengwa stendi kuu ya mabasi na soko kuu.
 
Huyuo Binti Lindi wa clouds naona anaenda kulamba Ubunge wa wanawake Lindi 😁
 
Ndio sehemu mazuri za kutulia huko na kufuga vimbuzi vyangu..
Hakuna maeneo hapo mkuu au yameisha watu washacheza na fursa..?
Maeneo yapo ya kutosha na sasa serikali ina mpango wa kuhamishia hospitali na mahakama ya mkoa huko
 
Back
Top Bottom