Limbwata na faida zake

Wana JF,
Nafikiri kwenye kila madawa kuna madawa makali, ya kati na ya chini. Yote yanakuwa madawa. Sasa katika hayo msemayo, kuna yanayoharibu kweli mtu uwezo wake wa kufikiri na anakuwa zezeta. Kuna yale yanayomfanya kupunguza ukali na kuna mengine ni kuaminishwa tu na mwanamke kwa kufikiri anapendwa, anaacha complex za kijinga na hapo mapenzi yanakolea/
Huko kwetu nilishasikia mifano kadhaa kwenye familia yetu. Mbili ni wanawake walioolewa kwenye familia na hawa walikuwa MBOGO kwa waume zao na cha kutisha walikuwa wakitembeza KIPIGO kwa waume zao. Sasa kwa sababu wanaume nao hawakuwa legelege, kwa kweli mkono ulitembezwa, meno yalirushwa, miiko, vyungu na "MPANTI" , sijui mnaita kibanio kwa kiswahili? ule mti umekaa kama Y ili kudhibiti sufuria au chungu cha ugali. Kesi ya kwanza sijui ila kesi ya pili nakumbuka marehemu baba yangu alihusika katika kutafuta dawa ya kumpoza huyo dada. Hadi leo hii wako pamoja.
Nyingine nilisikia ilikuwa ni kutoka familia ya shemeji yangu. Kwenye familia hiyo, anatoka Mwalimu Juma. Huyu Mzee alikuwa anasifika Tabora kuwa unaweza kumwacha Sikonge na ukaondoka na gari, ukifika Tabora mjini unamkuta anacheza bao. Na wanakuambia kaanza kucheza zamani tu. Katika hiyo familia, kuna jamaa aliolea humo. Ila huyo mke (dada ya shemeji yangu) alikuwa KICHAA/Mbogo sana kwa mumewe. Vurugu, matusi, ngumi nk ikawa kitu cha kawaida. Ndugu zake huyo dada kuona hayo, wakaamua kumfuata shemeji na kumuuliza kama anahitaji msaada. Jamaa akakiri kuwa maji yako shingoni na kibaya ni kuwa anampenda mkewe. Basi Mwalimu Juma alitengeneza dawa na jamaa akapewa ili amuwekee mkewe. Dada yule alituliza hayo maguvu yake na hadi leo wanaishi pamoja.
Nafikiri kila dawa ina ubaya na uzuri wake na inategemea tu unaitumia vipi. Moto, maji, Kisu nk vyote ni vizuri na muhimu kwa binadamu ila ukitumia vibaya, madhara yake .......
 
Huyu Mwl Juma bado yupo? isije kuta ndo huyu nilipiga picha hii huko Urambo mwaka jana!!!


3567d1234296805-limbwata-na-faida-zake-dr.juma.pdf
 
Duu, huyo kweli ni Dr.Juma na huyu nisemaye ni Mwalimu Juma. Sidhani kama anaishi na sidhani hata atakuwa anajua CASINO ni nini. Yaani kabla ya kwenda kwa Obama, itabidi nimtembelee na nikitoka hapo ni moja kwa moja LAS VEGAS. Nafikiri Mkapa atakuwa alimtembelea ndiyo maana HATUWEZI KUMSHITAKI mahakamani. Na hii atakuwa aliambiwa na Rostam Aziz ambaye na yeye wala haguswi.
 
Duu, huyo kweli ni Dr.Juma na huyu nisemaye ni Mwalimu Juma. Sidhani kama anaishi na sidhani hata atakuwa anajua CASINO ni nini. Yaani kabla ya kwenda kwa Obama, itabidi nimtembelee na nikitoka hapo ni moja kwa moja LAS VEGAS. Nafikiri Mkapa atakuwa alimtembelea ndiyo maana HATUWEZI KUMSHITAKI mahakamani. Na hii atakuwa aliambiwa na Rostam Aziz ambaye na yeye wala haguswi.

Huyo Dr Juma ni balaaa aisee kuna viongozi kibao huenda pale, wake kwa waume eti ana dawa ya kufunga ndoa mzee hutoki nje!!! Labda naye analibwata advanced!! Pia alikuwa Dr Juma wa Urambo ni mjasiliamali kweli kweli ona tangazo la kiswahili
3569d1234297945-limbwata-na-faida-zake-mganga.jpg
 
Last edited:
Ikiwa haijapasuka wangu, naisokomezea tuu. Tena hiyo ndo itakuwa inanipa na advantage ya pili kupasha K yangu moto...ufikapo mlangoni, unapokelewa na joto kali la nyuzi gredi sijui ngapi hivi! Utaacha kudata tuu. Bahati yako sikujui, ungesahau S.L.P ya kijijini kwenu.

...khaaaaaaa :eek: yaani adhabu yote hiyo almuradi niwe zezeta tu? ama mwanamke akikusudia lake...
Hushindwi wewe ku spike-drink ya mumeo kwa blue pills (viagra) iwapo anakuletea longo longo... duh!
 
Nasikia hizo libwata huwa ziko serious sana katika kufuata maagizo, ukisema “nataka mume wangu asitoke nje” ndio hatoki kabisa hata kazini/kanisani haendi. Ukisema “nataka mume wangu asiwe na hisia na wananawake” basi ndio hata wewe jihesabu out, ukisema “asiingize wanawake ndani” basi ujue hata mama yako mzazi akija akimkuta yeye hafunguliwi mlango.....libwata ni dawa za kupumbaza akili na kuwafanya wanaume wawe wajinga wajinga, ambazo mara nyingi hutolewa na wachawi wa kienyeji
 
hiyo inamajina mengi sana upande wa ziwa magharibi inajulikna kama CHUNTAMA au GENDAUGALUKE, lakini ubovu wa hizi ngoma zetu za kiasili hazina kipimo maalum, mzee unawza ukatandikwa na ukawa zuzu kabisa, na mkeo anajiachia anavyopenda lakini mzee ata ukiambiwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa
tuwe makini wajameni
 
Huyu Mwl Juma bado yupo? isije kuta ndo huyu nilipiga picha hii huko Urambo mwaka jana!!!


3567d1234296805-limbwata-na-faida-zake-dr.juma.pdf
Ndio maana nawapenda dada zenu.....wana skills i see......kuanzia ile limbwata ya kuweka nyama kuleee....mpaka huku kwa mwalimu jumah.....hok me one pls
 
...halafu baada ya ya yote hayo juu, unapoendelea kumsamehe Mkeo ambaye kila anapo cheat anakuja na visingizio kama, "shetani tu alinipitia mume wangu", hapo ujue LIMBWATA limekukolea haswa!


....Nilijua tu kuna mtu ataharibu..teh teh teh!!!:)
 
Ndio maana nawapenda dada zenu.....wana skills i see......kuanzia ile limbwata ya kuweka nyama kuleee....mpaka huku kwa mwalimu jumah.....hok me one pls

Hahahah dogo ngoja uje upate CHUNTAMA, GENDAUGALUKE na Limbwata total mix, lazima udate hata kazi hutafanya....shauri yako!!
 
...Mwanaume unamuachia mamaa 'ajilimbwatishe' mwenyewe! :D
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom