Ligi isiyo rasmi, inayoshabikiwa na trafiki na abiria Sauli vs Golden Deer

Miaka nenda rudi Njia ya Dar es Salaam - Mbeya ndio imekuwa njia ambayo ni gumzo kwa mabasi yake kwenda mbio.

Umbali wa safari ni zaidi ya kilometre 800, na njia imekuwa ikipita kwenye Milima mikali, kona kali, mbuga ya wanyama, hali ngumu ya hewa Ikiwa ni Pamela na uwepo wa ukungu mzito na upepo Mkali.

View attachment 1879605
Hiyo ndio njia ya Dar Es Salaam- Mbeya ilivyo.
Na uwepo wa changamoto hizo Kuna wanyama wenye miili ya watu, wakikakaa Kwenye usukani wao wanawaza jambo Moja tu, nitawafikishaje abiria mapema na salama.
View attachment 1879606
Hapo ndipo unapokutana na ligi ngumu isiyo rasmi kati ya kampuni mbili, Golden Deer (New Force) na Sauli a.k.a Mnyama Mkali.

Golden Deer wao wakitumia mabasi ya kutoka China na Sauli wakitumia mabasi ya Ulaya, Ujerumani na Sweden. Sauli wana Mercedes Benz na Scania na Golden Deer wakitumia Zong Tong Climber.
View attachment 1879608
Magari haya yametengeneza mashabiki wengi huku mashabiki wao wakijigawa upande mmoja na mwingine, na askari pia wana timu zao kwenye ligi hii.
View attachment 1879609
Mwendokasi ni Hatari kwa usalama na maisha ya abiria, watumiaji wengine wa Barabara, mazingira na hata vyombo vyenyewe.
Kwaa njia ya Kyela -Dar, mfalme ni Kyela Express, anawaacha mbaali akina Majinja ,Newforce na Rungwe, yeye nae anatumia Scania ambazo hapo nyuma zilikuwa malori. Ni balaa kubwa.
 
Huu ni upumbavu na sijui polisi wanapoona hizi clip wanachukua hatua gani.

Tunajiuliza zile speed governor zenye ving'amuzi haziyahusu hayo mabasi au?

Waziri wa mambo ya ndani na IGP waelezeni makamanda wenu wa mikoa ,bus likipata ajali wajihesabu hawana Kazi.
Nao ni mashabiki wa mbio za mabasi
 
😄😄😄 Kuna siku nikikuwa naangalia kipindi cha AIBUUU YAO cha ITV aisee walionyesha iyo bus ya iman plus dereva wake ali over take sehemu mbayaaa yaan hatariii alafu sasa mbele kukikuwa na trafik akalisimamisha dereva aka nyooshaaa nzimaaa ....ila siku si nyinginyule dereva alisitishiwa leseni yake kwa miezi kadhaa... Iyo njiaa ina makasheshe kumbee
Duh
 
Screenshot_20210807-075947.png
 
Roho inaniuma jamani
Mie ilishaniuma mpaka nikazoea saiz nikifika stend nikiona Higer naenda kusimama mbele yake naskilizia muungurumo wake baadae napanda Yutong nasepa zangu.

Team Scania inabidi tuwaombe Scania tz wafanye namna au Yale na malori ya 93 yakachongewe bodi ya Basi na kazi iendeleeeee
 
Bahari iyo ni ligi ya pili nyuma ya hao jamaa ila sauli aiseee january to december gari imejaa daaah anapiga mno pesa........hii biashara utaiona tamu hapa tu
Wikibili zilizopita nilisafiri na SAULI ya tunduma haikuwa na abiria nusu ya gari.
 
Back
Top Bottom