Ligi isiyo rasmi, inayoshabikiwa na trafiki na abiria Sauli vs Golden Deer

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,818
Miaka nenda rudi Njia ya Dar es Salaam - Mbeya ndio imekuwa njia ambayo ni gumzo kwa mabasi yake kwenda mbio.

Umbali wa safari ni zaidi ya kilometre 800, na njia imekuwa ikipita kwenye Milima mikali, kona kali, mbuga ya wanyama, hali ngumu ya hewa Ikiwa ni Pamela na uwepo wa ukungu mzito na upepo Mkali.

download (1).jpeg

Hiyo ndio njia ya Dar Es Salaam- Mbeya ilivyo.
Na uwepo wa changamoto hizo Kuna wanyama wenye miili ya watu, wakikakaa Kwenye usukani wao wanawaza jambo Moja tu, nitawafikishaje abiria mapema na salama.
images.jpeg

Hapo ndipo unapokutana na ligi ngumu isiyo rasmi kati ya kampuni mbili, Golden Deer (New Force) na Sauli a.k.a Mnyama Mkali.

Golden Deer wao wakitumia mabasi ya kutoka China na Sauli wakitumia mabasi ya Ulaya, Ujerumani na Sweden. Sauli wana Mercedes Benz na Scania na Golden Deer wakitumia Zong Tong Climber.
download.jpeg

Magari haya yametengeneza mashabiki wengi huku mashabiki wao wakijigawa upande mmoja na mwingine, na askari pia wana timu zao kwenye ligi hii.
Golden Deer.jpeg

Mwendokasi ni Hatari kwa usalama na maisha ya abiria, watumiaji wengine wa Barabara, mazingira na hata vyombo vyenyewe.
 
TAHADHARI KWA MADEREVA KONA HIZI ZA IYOVI NI KALI ZAIDI EPUSHA MAISHA YA ABIRIA CHUKUA TAHADHARI DHIDI YA AJALI‏
wewe ni dereva wa basi la abiria ama gari binafsi ?hebu chukua hatua ya kupunguza ajali leo kwa kujihadhari na kona hizi na Iyovi na Kitonga na kona nyingine kali kama hizi nchini kwani maisha yako ni dhamani kubwa na uhai wake bado tunautamani

Vema kuheshimu alama za barabarani na kuacha mbwembwe uwapo barabarani katika kona kali kama hizi

Katika kona kama hizi zingatia alama za usalama barabarani usiwe na haraka ya kulipita gari la mbele


Kulipita gari la mbele katika kona kama hizi ni kutafuta ajali
Hapa ni eneo ambalo watu 19 walipoteza maisha kwa fuso kugongana na basi na Nganga na kisha kuwaka moto uzembe ukiwa ni wa dereva wa basi aliyetaka kulipita gari la mbele katika kona kali



Usilipite gari katika kona

Alama zote za barabarani ni msaada kwa maisha yako lazima uziheshimu

Kona zote ni hatari kwa usalama wako hivyo usihame saiti yako ili kukimbia ajali

Lazima unapotaka kulipita gari la mbele uwe una uwezo wa kuona mbali zaidi ya mita 100 ama zaidi

Dereva makini halipiti gari la mbele katika kona

Kumbuka ni heri kuchelewa ukafika salama kuliko kuendesha kwa haraka na ukafika majeruhi ama maiti tambua Taifa linakuhitaji familia inakuhitaji na wewe dereva ni msaada wa abiria wote katika gari lako na msaada wa maisha yako jitambue ,watambue abiria wako , jilinde utulinde abiria wako maisha yako ni yetu na uhai wako ni tegemeo letu epuka ajali zingatia sheria za barabarani
 
Back
Top Bottom