Ligi isiyo rasmi, inayoshabikiwa na trafiki na abiria Sauli vs Golden Deer

Yaani basi inatoka DSM saa 12 alfajiri,inafika Mbeya karibia saa moja usiku,ni zaidi ya masaa 12+ barabarani kwa umbali wa kama kilometa 790 hadi 800 na bado unasema dereva amekimbia sana??
Mabasi ni ya kisasa kabisa, miundombinu imeboreshwa vizuri tofauti kabisa na miaka ya 90 huko kweli kuna kitu cha kushangaza hapo?
Sehemu ipi hatarishi kwa njia ya Mbeya ukiitoa hapo Iyovi,Kitonga?
Wanatembea mwendo wa kawaida tu tusiwafitinishe bhana
Miaka ya 90s ilikuwepo Kiswele na Tawakal Gari zinaingia mbeya saa 9 kutoka Dar,miaka ya akina Giriki
View attachment 1886205View attachment 1886206
 
Napenda Scania, Nissan diesel na Isuzu ndo Gari huwa napanda Yan nikifika stend nafanya uamuzi huo.

Sihu hz za karibuni niliamua kupanda hyo loliondo baada ya kapricon kujaa ilkua mza - ars, aisee sikuamini jinsi yutong tena sio hz mpya zilivyokuwa zinamwaga moto, the same case from Iringa to ars nikajichanganya nikapanda machame Mambo Ni yale yale Ile milima ya kukutafuta mtera tumeongozana na higer ya kimotco, na Scania ya kapricon Ila machame aliwaosha wote.

Tunatoka stend Dom tupo karibu nz round about ya shabiby ndo kimotco anaenda stend, Babati hotel kula angalia nyuma hola, stend hola mpaka ars hakuna mtu, juz pia hvyo hvyo sema ligi ilkua n Yutong vs Higer.

Dar express Jana kaleta nne soon Asante rabi, kapricon na kimotco watapokea punguzo la Bei kutoka Scania vinginevyo mzungu anatoweka kwenye uso wa mabasi Tanzania.

Kuna kitu wengi hawakiongelei humu ndani, Hizi basi nyingi za kichina huwa zikichoka engine wanafunga za Scania. Ndo maana unaweza kuta basi namba B la kichina linatembea kama karatasi.

Wengi hawarudishi engine za cummins
 
Hapo zishabadilishwa mpaka gear box mdau kubali tu hakuna mchina mwenye cxx na engine ile ile nenda pale maning nice huwa anafanya overhaul ya gari zima kuna siku nilikuta kashusha engine sita za climber na kaweka mpya ila bodi ni ileile..........tukio kama hili la kushusha engine kwa scania piru utalisahau mdau ila kwa mchina miaka minne mingi

Hii ni ukweli mtupu
 
Jamani mzungu aheshimiwe na msimfananishe kabisa na basi za kichina. Ijumaa nilikua humu toka Johannesburg to Lusaka, build quality ya hii chuma ni next level,gari iko kimya na inapanda milima huku inavuta trailer imejaa mzigo mpaka nashangaa.

Baada ya hapo leo nimepanda Zhong Tong climber toka Lusaka to nakonde hapa naumwa mgongo, bara bara yote naifeel mpaka zile small imperfections za kwenye lami. Build quality bado haijafikia lever ya irizar,upande wa engine performance naona bado Scania yuko mbali sana.
IMG-20210807-WA0051.jpg
20210806_130503.jpg
Screenshot_20210809-231857_Chrome.jpg
 
Asante
TAHADHARI KWA MADEREVA KONA HIZI ZA IYOVI NI KALI ZAIDI EPUSHA MAISHA YA ABIRIA CHUKUA TAHADHARI DHIDI YA AJALI‏
wewe ni dereva wa basi la abiria ama gari binafsi ?hebu chukua hatua ya kupunguza ajali leo kwa kujihadhari na kona hizi na Iyovi na Kitonga na kona nyingine kali kama hizi nchini kwani maisha yako ni dhamani kubwa na uhai wake bado tunautamani

Vema kuheshimu alama za barabarani na kuacha mbwembwe uwapo barabarani katika kona kali kama hizi

Katika kona kama hizi zingatia alama za usalama barabarani usiwe na haraka ya kulipita gari la mbele


Kulipita gari la mbele katika kona kama hizi ni kutafuta ajali
Hapa ni eneo ambalo watu 19 walipoteza maisha kwa fuso kugongana na basi na Nganga na kisha kuwaka moto uzembe ukiwa ni wa dereva wa basi aliyetaka kulipita gari la mbele katika kona kali



Usilipite gari katika kona

Alama zote za barabarani ni msaada kwa maisha yako lazima uziheshimu

Kona zote ni hatari kwa usalama wako hivyo usihame saiti yako ili kukimbia ajali

Lazima unapotaka kulipita gari la mbele uwe una uwezo wa kuona mbali zaidi ya mita 100 ama zaidi

Dereva makini halipiti gari la mbele katika kona

Kumbuka ni heri kuchelewa ukafika salama kuliko kuendesha kwa haraka na ukafika majeruhi ama maiti tambua Taifa linakuhitaji familia inakuhitaji na wewe dereva ni msaada wa abiria wote katika gari lako na msaada wa maisha yako jitambue ,watambue abiria wako , jilinde utulinde abiria wako maisha yako ni yetu na uhai wako ni tegemeo letu epuka ajali zingatia sheria za barabarani
 
Yaani basi inatoka DSM saa 12 alfajiri,inafika Mbeya karibia saa moja usiku,ni zaidi ya masaa 12+ barabarani kwa umbali wa kama kilometa 790 hadi 800 na bado unasema dereva amekimbia sana??
Mabasi ni ya kisasa kabisa, miundombinu imeboreshwa vizuri tofauti kabisa na miaka ya 90 huko kweli kuna kitu cha kushangaza hapo?
Sehemu ipi hatarishi kwa njia ya Mbeya ukiitoa hapo Iyovi,Kitonga?
Wanatembea mwendo wa kawaida tu tusiwafitinishe bhana
Kwanza kuwabana sana ni kudhoofisha taaluma ya udereva
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom