Life begins at 40 Vs Midlife crisis

[emoji23] hapana... Unajua hatujui kuzimu kupoje... Sasa unapokufa unaacha madeni badala ya mali... Unaenda kutana na kitu usichokitegemea
Ukifa ndio imeisha hiyo mkuu, kuzimu na mbinguni ni hapahapa duniani, kama unaishi kwa kutegemea kuna better life baada ya hapa duniani, basi hauishi utakua unasubiria kufa
 
pole sana ERoni

mimi nadhani niko kwenye 'quarter life crisis' ndo namalizia teens zangu mseleleko wa kuhudumiwa na wazazi ndo unaisha, shule ndo namalizia, nawaza maisha yatakuwaje kujitegemea ndo kunaanza na I'm starting from almost zero...
Ni wakati wa kujiweka sawa, ili depression zisikupate.
 

Hapo kwenye kufurahia life kila siku ni mtihani kweli kweli. Unajua wengi wetu tunaona kama furaha ni kitu cha kukipata ukifanikisha jambo flani lakini ukilifikia, bado unaweka vigezo vingine na mwisho wa siku unakuwa si wa kuyafurahia maisha..

Sometimes nawish ningekuwa na mindset kama ya wamama wa uswazi, unakuta anakaanga mihogo ya kuuza asubuhi ili apate hela ya unga na fungu la dagaa. Baada ya hapo anasindikiza jua kwa umbeya na kama mlevi anakunywa double kiki yake. Maisha yanaenda bila stress

Ila haya ya kuangalia huna gari, nyumba, stable career mara utengeneze image ya kuendana na wenzio, yaani expectations kubwa kubwa ni stress tupu hadi tunashindwa enjoy simple things in life.
 
Kila msemo duniani una tabia za kibaguzi kwa watu ipendayo.Tusing'ang'anie misemo isiyoendana na uhalisia tulionao.Mmiliki wa KFC afufuke atupe miongozo.
 
Kwamba mtu akiwa 40+ awe tayari amewekeza na pesa zinamfuata tu mkuu? Sasa mbona wengi wetu ndio tunaanza kujitafuta, tulichelewa either kusoma, kupata watoto, kuwekeza...

Do we still have another chance?
Nyie ndo toeni ushuhuda mnajionaje onaje
 
maamuzi magumu haya,

umewaza nini, au ndo ile 'ndoa ni utapeli'😂
Kama binaadamu kuna vitu vingine unaona kabisa havikuumbwa kwaajili yako. Na enjoy sana nikiwa mwenyewe na uhuru wangu binafsi, labda nikilewa ndo napenda kuwa na watu karibu, ila nikiwa sober sipendelea kabisa social life wala mambo ya kuwa na wanawake/mwanamke wa kuniganda
 
Kwamba mtu akiwa 40+ awe tayari amewekeza na pesa zinamfuata tu mkuu? Sasa mbona wengi wetu ndio tunaanza kujitafuta, tulichelewa either kusoma, kupata watoto, kuwekeza...

Do we still have another chance?
Imagine unamaliza chuo at 25 years
 
Very confusing
 
Binafsi sikuwah kufikiri kama umri ungekuja kuwa kitu serious cha kunichanganya moaka pale nilipo realize my life purpose.Yan toka nimekuja kujua ni wapi ninatakiwa kutulia na kuwekeza akili na nguvu zangu hapo, basi huwa naona kama muda unakimbia balaa mpaka kichwa kinauma.
Imefika hatua ya kutamani hata siku 1 ingekua angalau na masaa 30.

Huwa kuna time najilaumu kwamba akil hii nilionayo sasa kwanin sikua nayo nikiwa at around 26 years??

Anyway, cha msingi wakuu tupambane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…