Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Kibongobongo ni hivyo hivyo 40 Mwili unaanza kukukataa lazima uwekeze mapema ukifika 40 uanze kula pension yako ya kile umeweka before 40 Ila tafsiri yake nmekuelezea vizuri

Hujaelewa kwanini wanasema unapoomba kazi usivuke 45? Hapo Mwili tayari ushaanza kukukataa Ila unaulazimisha hivyo hivyo tu utafanyaje na wewe unataka upige maokoto
Nimekuuliza hivyo coz maisha ya kibongo yanatuchelewesha sana, at 30 bado tunasoma, at 35 hatuna stable income, at 40 tunawaza kuoa...unadhani kweli life begins at 40 mkuu?
 
Kuna vingine vigumu 🤭 havibalansiki kwa uharaka… lazima ubaki nyuma kidogo, ama utangulie.
True, na hapo ndio tunakutana na midlife crisis at 40. Havikwepeki..
 
Kuna kuishi na kuishia, nafikiri ukifika 40 unaianza safari ya kuishia duniani. Ila ukifika 30 unatakiwa kuwa umeanza kufanya kilichokuleta duniani.

Na ukiwa 20-29/30 hapo unatakiwa kuishi, huna stress, unazo nguvu zakutosha kuzurura, una uwezo wa kupata furaha kwa jambo dogo (mizuka).

Japo hii sio kwa wote maana kuna watu wana muaka 16 na wana stress zakutosha plus majukumu, ila kwa wengi au standard ya kidunia huo nivumri wa kuishi yaani kufurahia uwepo wako hapa duniani bila stress kali.

True mkuu, kuna wengine hapa maisha hayakuturuhusu kuwa watoto ama reckless kwenye balehe ndio maana naona dalili nyingi tajwa nimekuwa nazo toka nikiwa late 10's .

I wish hii mada niwatumie watu wengi zaidi maana kwa vijana wa sasa pressure ya maisha ni kubwa japo kwa walioishi enzi za kazi zikitafuta watu. Hawawezi kuelewa
 
True mkuu, kuna wengine hapa maisha hayakuturuhusu kuwa watoto ama reckless kwenye balehe ndio maana naona dalili nyingi tajwa nimekuwa nazo toka nikiwa late 10's .

I wish hii mada niwatumie watu wengi zaidi maana kwa vijana wa sasa pressure ya maisha ni kubwa japo kwa walioishi enzi za kazi zikitafuta watu. Hawawezi kuelewa
Yeah, walioishi kipindi kazi zikitafuta wat(80s na early 90s) hawawezi kuelewa.
 
Niko 77 na ndiyo kwanza kunakucha huniambii kitu ng'wanawane 😁💪

Hizi ni perception za jamii tu ili pengine kuwatia hamasa na kuwaasa walioko huku nyuma wasikakawane kwenye nira za ujana bali wamakinikie zaidi kuanza maandalizi mapema maana ukifika huko 40+ hata process nyingi za mwili zinaanza kukuwashia indiketa kuwa sasa tunahama kwenye msimbo wa ujana na tunaingia kwenye utu uzima sasa.

Hii ni sawa tu na ile perception kwamba eti binti akivuka miaka 30 hajaolewa basi jua lake jema na lililong'aa sana hapo nyuma sasa linaingia machweoni. Na kuna mabinti wasiojitambua ambao kweli wakivuka 30 na bado hawajaolewa wala kuwa na familia wanapaniki badala ya kutulia na kuwekeza katika wao kama wao. Hata katika hili wapo wengi tu wanaofikia hiyo 40+ huku ramani za maisha bado zipo zigzag wanapata sonona hasa wakijilinganisha na waliosoma nao ambao wanakuwa wameshapiga hatua kubwa.

Binafsi kama ningeambiwa leo hii muda urudishwe nirudi huko kwenye 40s kitu pekee ambacho ningekirekebisha ni kuutunza mwili na kujali afya yangu sana. Nisingekunywa mipombe kupindukia na minyama choma hii. Japo ukiwa kijana huwezi kuona madhara yake, ukivuka 45 huku ndiyo sasa utaona kosa ulilofanya - na hapo kama una bahati hujapata presha, kisukari, matatizo ya figo, magonjwa ya moyo na ishu zingine kibao.

Miaka ya 40....kijana linda sana afya yako. Kila kitu kifanye in moderation (ikiwemo ulaji wa mbususu). Mengine yote ni madogo tu hasa kama unajitambua.

Hint: Usijilinganishe na classmates wako. Hypertension itakuhusu 😁😁🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🖐

View attachment 2760494
Hapo kwenye 77 nimepata ukakasi maana umempiga gap hadi mshua wangu na huwa nakuita bro 😁😁

Ila huwa una madini sana kuhusu life na huwa hubanii kuchangia. Shukrani na ubarikiwe sana kwa hilo "brother" 🙏🏽
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom