Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Mnaruka ruka tu. Nchi hii ina wanamaombi makini ambao tangu mwaka umeanza wao ni kufunga, kupiga goti na kuomba usiku na mchana ili Mungu Yehova, Mungu mwenye nguvu, Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, Roho Mtakatifu aivushe nchi hii salama salimini. Mungu wa Utatu anajua rais tutakayempata. Tuungane kuiombea nchi yetu
 
BARAZA LA MAWAZIRI LA LOWASSA
  1. Waziri Mkuu Professor Juma Kapuya
  2. Waziri Maliasili na Utalii Mghana Msindai
  3. Waziri wa Nishati na Madini William Ngereja
  4. Bunge Sera na Uratibu Hamis Mgeja
  5. Wanawake na Watoto Sophia Simba
  6. Habari Michezo na Utamaduni Beatrice Shelukindo

Jazeni wengine, halafu eti hawa ndio tunategemea kutuletea mabadiliko Tanzania, utani mwingine umepitiliza!

Nilitaka hizi opinion zitolewe na watu wengi zaidi ili watu wajue nchi hii inakoelekea! Thanks ingawa mods wameondoa uzi uliotaka majibu haya! Pasco vipi hapa, kuna maskini atabaki kweli?
 
Last edited by a moderator:
..hivi Mkapa naye akiwa Raisi na Mwenyekiti wa CCM si alijiapiza kwamba atawakomesha wanamtandao?

..nini kilimtokea na dakika za mwisho kabisa akabadili msimamo na kumuunga mkono mgombea "anayependwa" na wananchi?

..najua CCM imepata kuwaengua watu wazito kama Cygwiyemwisi John Malecela, lakini sidhani kama Lowassa na wanaomuunga mkono are push overs kama Malecela.

cc Nyamizi, Pasco
Mkuu nakuhakikishia jina la Lowasa halitafika kwenye vikao vinavyoweza kulipitisha. Unafikiri nje ya hao wajumbe wake aliowanunua ndani ya ccm, nje ya ccm nguvu yake kisiasa ikoje? Anaweza kukimbia chama chake bado akatikisa kama ilivyokuwa kwa mrema? Usimlinganishe Kikwete na mkapa, Kikwete anazifahamu vyema siasa chafu anazocheza Lowasa, na bila shaka kesha andaa dawa yake.
 
OMBI KUU LA UKAWA NI CCM IKOSEE TU,""kwa kuwasikiliza akina nape!""hivi ccm haikomi tu kwa kuwawekea WATANZANIA MIDUDE ISIYOFAA,ombi CCM msikosee tena! kwani mara nyingi kosa hili limesha ikost ccm sehemu nyingi sana! "kuwapa watu product isiyofaa"
 
Mkuu nakuhakikishia jina la Lowasa halitafika kwenye vikao vinavyoweza kulipitisha. Unafikiri nje ya hao wajumbe wake aliowanunua ndani ya ccm, nje ya ccm nguvu yake kisiasa ikoje? Anaweza kukimbia chama chake bado akatikisa kama ilivyokuwa kwa mrema? Usimlinganishe Kikwete na mkapa, Kikwete anazifahamu vyema siasa chafu anazocheza Lowasa, na bila shaka kesha andaa dawa yake.

..mimi sidhani kama Kikwete anaweza kumtupa Lowassa.

..hawa wametoka mbali mno, tangu mwaka 95 na inawezakana kabla ya hapo.

..Lowassa ametoa mchango mkubwa sana kumfikisha Kikwete hapo alipo.

..hata ile kashfa ya Richmond, Lowassa took the hit kuwakinga wengine.

..kumbuka Dr.Mwakyembe alisema kuna mambo hawajayatoa ili kutoiabisha serikali. Lakini ripoti hiyo ilifikia mpaka kumuaibisha Waziri Mkuu, sasa huyo aliyefichiwa mambo yake alikuwa nani?

..Nakubali kwamba JK anazijua sana siasa za nchi hii, lakini sidhani kama ni mtu katili mwenye kuweza kumdhulumu mtu waliyetoka naye mbali na aliyemhangaikia kama Edward Lowassa.

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
Kusonga mbele kwa hii nchi kuko mikononi mwa Lowasa.
Akitoswa kwa mizengwe ya kampeni alizoanza Nape kwa muda mrefu.
Nchi itanusurika na kuokoka kutoka kwenye mikono ya joka kuu linaloitwa CCM.
Demokrasia itastawi vema kwani wapinzani watapaa sana.

Hali kadhalika akipitishwa na CCM mahasimu wake japo hawana nguvu na mbinu za kuwashawishi watanzania lakini wapinzani pia watapaa kwa kupata wabunge na madiwani wengi.

Tumuombe Mungu ili Lowasa awe na uzima ili atukomboe tuondokane siasa za chuki na maji taki ndani ya CCM.
 
..mimi sidhani kama Kikwete anaweza kumtupa Lowassa.

..hawa wametoka mbali mno, tangu mwaka 95 na inawezakana kabla ya hapo.

..Lowassa ametoa mchango mkubwa sana kumfikisha Kikwete hapo alipo.

..hata ile kashfa ya Richmond, Lowassa took the hit kuwakinga wengine.

..kumbuka Dr.Mwakyembe alisema kuna mambo hawajayatoa ili kutoiabisha serikali. Lakini ripoti hiyo ilifikia mpaka kumuaibisha Waziri Mkuu, sasa huyo aliyefichiwa mambo yake alikuwa nani?

..Nakubali kwamba JK anazijua sana siasa za nchi hii, lakini sidhani kama ni mtu katili mwenye kuweza kumdhulumu mtu waliyetoka naye mbali na aliyemhangaikia kama Edward Lowassa.

cc Pasco
Mbona kishamtupa kitambo! Muulize Pasco akueleze ni mara ngapi lowasa ameomba kukutana na Kikwete akashindwa. Hukushangaa alivyowaomba masheikh wake feki toka Bagamoyo wamfikishie ujumbe kwa mheshimiwa rais bila kujua kwamba alikuwa anaongeza mafuta kwenye moto aliotakiwa kuuzima?
 
Njaa ni mbaya inafumba macho, huwezi tena kujali taifa lako ila tumbo... Baadaye hawa hawa huwa wanaanza kulalamikia ooh huyu rais aah rushwa imezidi mara eeeh uwezo mdogo wengine mafisadi waliotoa hela za kampeni ndio wanaongoza nchi kwa mikataba na zabuni nono .. #yatafuata
 
Mbona kishamtupa kitambo! Muulize Pasco akueleze ni mara ngapi lowasa ameomba kukutana na Kikwete akashindwa. Hukushangaa alivyowaomba masheikh wake feki toka Bagamoyo wamfikishie ujumbe kwa mheshimiwa rais bila kujua kwamba alikuwa anaongeza mafuta kwenye moto aliotakiwa kuuzima?

..mbona mbinu hizi anazotumia Lowassa ndizo alizotumia JK kupata huo Uraisi.

..si ni huyu huyu JK aliyekuwa akichafua wenzake wakina Sumaye, Salim Ahmed Salim, kwenye vyombo vya habari?

..je, mmesahau tuhuma za wajumbe wa mkutano mkuu kanda ya ziwa kupewa bahasha wakati wakielekea Dodoma?

..pia mmesahau utetezi wa Lowassa kuhusu Richmond ktk kikao kilichoongozwa na JK, mpaka ikafikia Mzee Mkapa kuokoa jahazi?

..mimi nitaendelea kuamini kwamba JK na Lowassa ni wamoja mpaka pale vikao rasmi vya chama vitakampomchinja Lowassa.

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza

kazi tunayo wa Tanzania, njaa ni mbaya sana inamtakatisha hata jambazi na anang'ara na kuwa kama askofu, kisa fedha anazopora anakugawia na wewe. mlaaniwe wote wenye njaa zenu.
 
..mbona mbinu hizi anazotumia Lowassa ndizo alizotumia JK kupata huo Uraisi.

..si ni huyu huyu JK aliyekuwa akichafua wenzake wakina Sumaye, Salim Ahmed Salim, kwenye vyombo vya habari?

..je, mmesahau tuhuma za wajumbe wa mkutano mkuu kanda ya ziwa kupewa bahasha wakati wakielekea Dodoma?

..pia mmesahau utetezi wa Lowassa kuhusu Richmond ktk kikao kilichoongozwa na JK, mpaka ikafikia Mzee Mkapa kuokoa jahazi?

..mimi nitaendelea kuamini kwamba JK na Lowassa ni wamoja mpaka pale vikao rasmi vya chama vitakampomchinja Lowassa.

cc Pasco
Ndiyo maana kwenye post #163 nimesema usimlinganishe mkapa na Kikwete. Tuombe uzima, Lowasa atatupwa nje ya kinyang'anyiro na atalazimishwa kumsapoti na kumfanyia kampeni atakayepitishwa na chama. Hatakuwa na chaguo isipokuwa kutekeleza.
 
watanzania hii ni laana au ujinga au nn??huyu fisadi anayehonga kila mtu ili awe rais ndio unamuita kipenzi cha watu? umekosea sana ni kipenzi chako na mkeo! rubbish!
 
Back
Top Bottom