Li Wapi Azimio La Songea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Li Wapi Azimio La Songea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Sep 18, 2008.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Sep 18, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Takribani mwaka mmoja sasa umepita toka Azimio la Songea litangazwe na kupigiwa debe sana katika vyombo vya habari na lile kundi lililokuwa linajiita 'Marafiki wa Zitto Kabwe'. Maadam Mheshimiwa ni mjumbe wa humu JF na naamini kundi hili pia limo humo basi naomba tuelimishane kuhusu Azimio hili, hatua ambazo zimekwishafikiwa katika kulinadi na maendeleo ya utekelezaji wake. Itakuwa vyema pia kama tutapata historia fupi ya Azimio hili na kuelewa tofauti yake na maazimio mengine kama vile Azimio la Arusha lililopelekea kuwa na wahanga kama Seti Benjamini Mpinga. Nawasilisha.
   
Loading...