LHRC: Vyombo vya Haki Jinai vitekeleze mapendekezo ya tume

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kimetoa witu kwa vyombo vinavyohusika na Haki jinai nchini vianze kutekelezeka Mapendekezo ya Tume hasa Yale yasiyohitaji matumizi ya fedha au kubadilisha sheria.

Aidha wamewataka wadau wa Haki Jinai nchini k a kushirikiana na serikali watoe elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migogoro isyo ya lazima na vyombo vya Dola.

Wito huo aliutoa Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Mapendekezo muhimu yaliyowasilishwa na Tume ya Haki jinai kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Anna.jpg

Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Anna Henga

"Kwa muda mrefu LHRC imekuwa ikipigania uwepo wa mfumo huru na unaojitegemea juu ya uchunguzi na upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini kutokana na ukweli kwamba mfumo wa sasa kuwa sehemu ya jeshi la polisi Kitendo kinachopelekea uwepo wa uwezekano wa watuhumiwa kubambimiwa kesi na wakati mwingine kuharibuwa au kuingiliwa kwa ushahidi na upelelezi kuchukua muda mrefu, hili ni Moja ya pendekezo la LHRC lililotolewa kwa Tume"

Kutokana na hivyo, LHRC imeishauri serikali kutekeleza pendekezo la Tume la kuanzisha na kuanzishwa kwa Mamlaka mpya na huru inayojitegemea itakayojulikana kama ofisi ya Taifa ya upelelezi (OUT) itakayokuwa na Mamlaka ya kupeleleza kesi zote za jinai.

Mbali na hayo, LHRC imeiomba serikali ipeleke miswada ya sheria katika Bunge la mwezi Septemba katika Mapendekezo ambayo yanahitaji mabadiliko ya sheria

Pia LHRC imesena ni vyema kukawa na mfumo wa kufanya tathmini juu ya utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume.

Kuhusu Dhamana, Henga alipendekeza kupelekwa kwa mswaada wa sheria ya Dhamana kama ilivyopendekezwa na Tume ili kutoa mwanya kwa masuala yote yanayohusu kuwa chini ya sheria Moja tofauti na sasa ambapo suala la Dhamana linaongozwa na sheria tofauti tofauti kulingana na kosa husika.

"LHRC inashauri serikali kufanyia kazi Mapendekezo haya kutokana na ukweli kwamba tayari uamuzi wa aina hii nulikwisha tolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu katika shauri la Legal and Human Rights Centre & Another dhidi ya serikali ya Tanzania maombi Na 039/2020"

Kwa upande wa adhabu ya kifo LHRC imependekeza adhabu hiyo kufutwa.

"Kwenye mfumo wa Haki jinai ulio na changamoto nyingi kama zilivyoainishwa ni rahisi kumhukumu mtu adhabu ya kifo asiyekuwa na hati"

Kadhalika LHRC imeishauri serikali kurudisha majukumu yote ya ukamataji mikononi mwa Jeshi la Polisi huku Taasisi nyingine zilizoundwa kwa mujibu wa sheria kama vile TAKUKURU ambazo kwa namna moja ama nyingine Zina Mamlaka ya kufanya uchunguzi na ukamataji kufanya hivyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi pale zinapotekeleza majukumu yake ya kioperesheni.

LHRC pia imependekezwa kuundwa kwa chombo huru kitakachoshughulika na malalamiko ya wananchi kuhusu vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi la Polisi kutoenenda kwa mujibu wa sheria.

Aidha, LHRC imependekeza chombo hilo kijengewe uwezo ikiwa ni pamoja na kutembelea nchi mbalimbali kama vile Kenya na Afrika ya Kusini kuona namna wenzao wanavyofanya kazi.
 
Tume imejazwa maaskari polisi sijaona hata sehemu moja polisi wametajwa uchafu wao kwa kifupi hiyo tume ya Chande ni uchafu mtupu
 
Kuna watu wanazaidi ya wiki 3 wapo ndani na haijulikani wameshtakiwa kwa kosa lipi, dhamana hakuna, wakaanzie huko (Morogoro kituo kikuu )
 
Back
Top Bottom