LHRC: Upinzani ulionewa uchaguzi mdogo Kinondoni, Siha

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287

Dar es salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," amesema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana. Lakini mawakala wa CCM walipewa mapema na walikuwa vituoni."

Henga pia amesema kitendo cha kuwa na idadi kubwa ya polisi katika vituo vya kupigia kura kiliwatisha wananchi kujitokeza vituoni.

Pia ameeleza jinsi viongozi wa Serikali walivyotumia magari ya umma katika kampeni za uchaguzi huo kwamba haikuwa haki.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni lini mkurugenzi wao atastaafu?Baada ya kumuuliza hili swali naona bibi helena kaamua kujiondoa kwenye press na sasa Anna Henga anaanza kupewa nafasi.
Bado nasiitiza kuwa Mama helena tenda haki kwa vijana na uwaachie ukurugenzi fully usije ukawa kama mbowe.
Staafu ubakie kuwa mshauri tu!

Swali dogo....je chadema kuandamana nje ya muda wa kampeni tena bila kibali ilikuwa sahihi?
 
LHRC.jpg

Dar es salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," amesema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana. Lakini mawakala wa CCM walipewa mapema na walikuwa vituoni."

Henga pia amesema kitendo cha kuwa na idadi kubwa ya polisi katika vituo vya kupigia kura kiliwatisha wananchi kujitokeza vituoni.

Pia ameeleza jinsi viongozi wa Serikali walivyotumia magari ya umma katika kampeni za uchaguzi huo kwamba haikuwa haki.

Gazeti la Mwananchi
 
Naileta kama ilivyo pasina kuongeza neno.Yote yaliyotokea yamewekwa wazi.Tunaweza kuwapinga leo lakini nafsi zetu zitatusuta mpaka siku ya kuingia kaburini.

Hakuna Uchaguzi uliowahi kuwa huru na haki katika jicho la mshindwa...hata USA wanalalamika uchaguzi ulichezewa!
 
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ,Anna Henga

Kwa ufupi
  • Uchaguzi katika majimbo ya Kinondoni na Siha ulifanyika Februari 17, 2018
By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchipapers.co.tz
Dar es salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimedai uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17, 2018 ulikuwa huru, lakini haukuwa wa haki kwa sababu vyama vya upinzani vilionewa.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 1, 2018 Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, Anna Henga amewaeleza waandishi wa habari kuwa kulikuwa na upendeleo kwa CCM, kwamba mawakala wa vyama vya upinzani walinyimwa viapo katika vituo vingi na kusababisha vyama hivyo kukosa waangalizi.

"Sisi hatuogopi kuitwa Chadema wala chama kingine cha upinzani kwa sababu tunafuata sheria. Kama uonevu ulikuwepo lazima tuseme," amesema Henga.

"Kulikuwa na uonevu kwa vyama vya upinzani, mawakala wao walinyimwa viapo au kupewa nakala. Tuliwashuhudia mawakala wao wakihangaika kutafuta viapo, wengine walipata saa 8 mchana. Lakini mawakala wa CCM walipewa mapema na walikuwa vituoni."

Henga pia amesema kitendo cha kuwa na idadi kubwa ya polisi katika vituo vya kupigia kura kiliwatisha wananchi kujitokeza vituoni.

Pia ameeleza jinsi viongozi wa Serikali walivyotumia magari ya umma katika kampeni za uchaguzi huo kwamba haikuwa haki.

LHRC yadai upinzani ulionewa uchaguzi mdogo Kinondoni, Siha
 
Hao CHADEMA si walisuria Longido, Songea na Singida, nani aliwalazimisha Kino na Siha?
 
Back
Top Bottom