Leticia Musore wa CHADEMA ahamia NCCR

Leticia Musore wa CHADEMA ahamia NCCR

Wakati juzi mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, akitangaza kuachia ngazi kupisha uchunguzi wa tuhuma kwamba ameuza chama, jana mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Taifa (Bawacha), Leticia Mosore, alijiondoa kwenye chama hicho baada ya kukosa ubunge wa Viti Maalumu, akajiunga na NCCR-Mageuzi.
Akijibu hatua za Shitambala na Mosore, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, jana alitoa kauli mbili, moja ikimzuia Shitambala kujiuzulu uongozi; na nyingine ikiainisha vigezi vilivyotumika kuwapata wabunge wa Viti Maalumu baada ya Bawacha, chini ya Mosore, kushindwa kuendesha uchaguzi huru na wa haki.
Dk. Slaa, alimtaka Shitambala kubaki katika nafasi yake, huku chama kikichunguza tuhumu dhidi yake za ‘kuuza ubunge’ wa Mbeya Vijijini, zikiendelea kufanyiwa kazi. Shitambala alituhumiwa na wanachama wenzake mkoani Mbeya kwamba alikosa ubunge kwa sababu aliuza nafasi hiyo kwa CCM. Juzi alitangaza kujiuzulu ili uchunguzi ufanyike dhidi yake.
“Hakuna haja ya wewe ndugu Shitambala kujiuzulu na kuruhusu makao makuu kufanya uchunguzi. Ofisi yangu itaendelea na uchunguzi wake kadiri, kwa wakati na, jinsi itakavyohitajika.
“…Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Ibara ya 6.3.4(a) sababu na msingi wa kujiuzulu kwako havijitoshelezi, hivyo unatakiwa kuendelea na nafasi yako kama unavyoelezwa na Katiba kisha kufafanuliwa na kanuni ya 7.71(i)-(iv),” ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Dk. Slaa.
Kuhusu Mosore, aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu wa Tarime, Mara, alijiunga na CHADEMA miaka mitano iliyopita akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM), vongozi wenzake wa Bawacha mkoani Mara, walisema hawakushtushwa na Leticia kuhama chama hicho, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa anasaka uongozi na maslahi binafsi, badala ya maslahi ya chama.
Mosore alitangaza azma yake ya kujivua uongozi na uanachama wa CHADEMA, mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi, Ilala, Dar es Salaam. Baadaye kidogo, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alimkabidhi kadi na katiba yao.
Mosore aliwalaumu viongozi wa juu wa CHADEMA kwamba ndio waliomkosesha ubunge. Hata hivyo, uongozi wa CHADEMA ulisema Mosore alishindwa kuandaa uchaguzi wa kuwapata viti maalumu, hadi chama kikalazimika kuweka vigezo vipya.
Ingawa Mosore alidai kuwa kwa wadhifa wake wa mwenyekiti wa Bawacha alistahili kuwa Mbunge, viongozi wa CHADEMA na kwa mujibu wa vigezo vilivyotumika, hiyo haikuwa sifa pekee ya kumwezesha kuwa mbunge.
CHADEMA kilivunja uchaguzi wa Bawacha kikidai yalijitokeza mazingira ya rushwa na vurugu, hivyo kikaamua utafutwe utaratibu mpya wa kuwapata viongozi.
Awali, chama kiliamua kuweka kaulimbiu ya “asiyefanya kazi na asile” kwa maana kuwa wanawake wangepata ubunge huo baada ya kushiriki kikamilifu katika kampeni kwenye kata, majimbo na taifa.
Lakini wakati kampeni zinaendelea, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilikitaka CHADEMA kuwasilisha majina ya wateule wake siku 30 kabla ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria; hivyo kikaunda utaratibu wa kitaalamu wa kuwapata kwa kumtumia Dk. Kitila, aliyeweka vigezo vilivyowapa alama kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho.
Dk. Willibrod Slaa, alisema Leticia hakubahatika kuwa miongoni mwa wanachama 25 wa kwanza walioomba Viti Maalumu, kwa sababu wenzake walimzidi katika vigezo sita (6) viliyowekwa, na mtaalamu elekezi; na kwamba haikuwa kazi ya viongozi wa juu kuteua majina ya wagombea.
Alisema kulingana na alama walizopewa wagombea, wa kwanza alipata 94 na wa mwisho mwiongoni mwa wanachama 105 waliopendekezwa, alipata alama 16. Wanawake wa CHADEMA walioomba nafasi za Viti Maalumu walikuwa 147, na nafasi zote kwa vyama vyote ni 105.
Idadai ya wabunge wa Viti Maalumu ilitegemea idadi ya wabunge wa majimbo, na kwa kuwa CHADEMA ilipata wabunge wa majimbo 24 kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilipatikana nafasi 25 za Viti Maalumu na alama za Mosore hazikutosha – labda kama wangepata wabunge wengi zaidi.
Dk. Slaa alisisitiza pia kuwa si viongozi wa chama waliohusika na kuteua majina ya wagombea, bali wagombea walichujwa kwa vigezo vilivyowekwa na mtaalamu elekezi aliyeombwa na chama kuwaandalia mchakato wa kuwapata wagombea, Dk. Kitila Mkumbo.
Vigezo vilivyotuma ni kiwango cha elimu, uzoefu wa uongozi ndani na nje ya siasa, mchango katika chama, umri katika chama, uzoefu wa uongozi wa siasa, uzoefu wa uongozi nje ya siasa, mchango wa hali na mali katika operesheni za chama na kampeni.
Ingawa Mosore, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA taifa alisema kuwa kwa nafasi alizokuwa nazo alistahili kupata ubunge wa viti maalum lakini kwa madai yake alinyimwa nafasi hiyo kwa ubinafsi wa viongozi, wenzake walisema hivyo ni vigezo vya CCM, si CHADEMA.
Wakati hayo yakiendelea, CHADEMA inajipanga kuweka mpango mkakati wa kujiimarisha kutoka chini hadi taifa, na kukiimarisha chama kwa kazi kueleka 2015.
Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kujadiliwa katika vikao vitakavyofanyika siku chache zijazo, mahali patakapopangwa, ni jinsi ya kutumia nguvu iliyopatikana kujenga chama na kusahihisha kasoro zilizojitokeza mwaka huu.
Azima ya CHADEMA ni kuwasha moto wa mabadiliko makubwa ya Kikatiba na kisheria ambayo kimekuwa kinayalilia kwa miaka zaidi ya 18 iliyopita; na ambayo kimeanza kuyashinikiza kwa njia mbalimbali ikiwamo kumsusa Rais Jakaya Kikwete Bungeni, kwa madai kuwa amerejea madarakani kwa uchakachuaji wa kura.
 
huyu mama nimesikia kwenye magazeti ana mahusiano na viongozi wa nccr
 
Lengo hasa la viti maalumu ni kutrain baadhi ya wakina mama ambao ni potential leaders lakini wamemiss political experience, hivyo 5 years will give them political hedge to compete majimboni kwao. Sasa kama tutaendeleza tamaduni za kina Rita Mlaki na CCM kwamba naachia kugombania lakini nitarudi bungeni. Then tunachofanya ni kubadilisha kanzu lakini shekh ni yule yule.
Nakubaliana nanyi kwa asilimia 100....Chadema inatakiwa kuweka utaratibu mzuri ili kila mwanamke anayepewa nafasi ya viti maalum ni kwa sababu anaandaliwa kusimama kugombea Ubunge baada ya miaka mitano, hivyo hata vigezo vyake ni lazima vifuate nguvu ya mhusika jimboni, uwezo wake wa kuwakilisha na kadhalika.
 
NAOMBA CV ZA HUYU MAMA ZIWEKWE HAPA ILI TUJUWE ELIMU YAKE NA MENGNEYO. MAANA USIKUTE NI ELIMU YA NGUMBALU.:hungry:
 
Hamna lolote,anadhani na yeye ataukwaa ubunge kama*****.IlaYou never know bwana,kila la heri Leticia.
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.
 
hivi jamani jina lako likiteuliwa likagombee uongozi inamaana ndio umepita?maana yeye anasema jina lilikuwepo lakini likakatwa,dada inategemea na vigezo kama hukutimiza hawana budi kukuondoa. ASIYEKUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI,KWA HALI HIYO INAONYESHA NI JINSI GANI UNAVYOPENDA MADARAKA KULIKO MAJUKUMU YA KUTETEA WANANCHI
 
Wana JF tuliza kichwa ila Kama huyu dada kahama ahame watahama wengi yeye si wa kwanza. Hatuna hakika Lakini tumeona huyu dada ni mtu wa aina gani kwa nini asiweke mambo hayo wazi chamani mwka? Kumbuka CDM is going strong na haitabomoko we know the trck let her travel in peace there is no room for opportunists in CDM.

pamoja kaka
 
Muda si mwingi redio Maria imeripoti kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa amekihama chama hicho na kuhamia NCCR Mageuzi kisa anasema CDM kinaongozwa kindugu na kibaguzi kwani yeye alikuwa kati ya wabunge ishirini wa viti maalumu lakini jina lake likakatwa.

Mwenyekiti Mbowe shutuma hizi ni za kweli au za mfa maji?.

Inawezekana kabisa alikuwa Chadema akisubiri cheo Ila sio kuwatumikia wananchi bora na aende tu.
 
Jamani mmeiibua hii habari ya November 2010!mi nilidhani kuna mapya kumhusu huyu mama, kumbe...!?
 
huyu mama tamaa zilimponza. ndiye aliye takiwa kuchukua nafasi ya Regia Mtema. alitamani kurudi chadema.
 
Hili jambo sio dogo kisiasa kwa chama cha CHADEMA;

Iweje mama huyu AWE NA SIFA YA KUWA MWENYEKITI TAIFA WA WANAWAKE CHADEMA lkn asiwe na sifa ya kuwa Mbunge wa viti maalum ktk wanawake zaidi ya 20 walioteuliwa na CHADEMA?
Uroho wa madaraka unamsumbua huyu mama!kwani huo uenyeketi ulikuwa haumtoshi kutumikia chama?let her go!!
 
Hili jambo sio dogo kisiasa kwa chama cha CHADEMA;

Iweje mama huyu AWE NA SIFA YA KUWA MWENYEKITI TAIFA WA WANAWAKE CHADEMA lkn asiwe na sifa ya kuwa Mbunge wa viti maalum ktk wanawake zaidi ya 20 walioteuliwa na CHADEMA?

Tume ya uteuzi ya CHADEMA iliyoongozwa na Dr Kitila Mkumbo itolee ufafanuzi jambo hili muhimu;Mama huyu amekosa sifa walizo nazo akina Miss Mashishanga,Mama Abwao,Miss Regia,Miss Ruhonga na wengineo?

Ye alitaka awe na vyeo vyote? hyo nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Wanawake halikumtosha?
 
ukwaju acha tuseme!
Hivi hao wanaojiuzuru wanafikiria hiki ni chama cha mafisadi cha kupeana vyeo?Waache upumbavu kama vp wakauze bangi!

lazima tuseme ukweli,chadema ni chama cha kihuni tu,ni chama kilichojaa ukabila,hasa uchaga!wanaokihama wanaona mbali sana,acha watz wadanganyike,wachague hk chama 2015,wengi mtakuwa wapagazi wa wachaga,enzi za manamba zitarudi,mi niko ethiopia,kazi kwenu ndugu.
 
Bora mnaosema CHADEMA ni chama cha wachaga ila sio tulio ndani yake tunajua Uchaga unatokana na uanzishwaji wake tu. lakini sasa kina uongozi ulioenea nchi nzima.
Sasa niulize NCCR, CCM, TLP na CCJ asili yake wapi?

Hivi vyama vinamsaidia nani?
NCCR mwenyekiti wake kahamia CCM japo anaendesha vikao NCCR.
CCM inamilikiwa na majambazi wa nchi hii
TLP Mrema anakaa nayo mfukoni kwake (Naye ni Mchaga) japo ubunge kapewa na CCM
CCJ nape na sitta waliianzisha halafu akaiweka pending ili akusanye hela CCM kwanza

Kwa kuwa CHADEMA kinaonyesha msimamo wa kiutawala na kutetea Watanganyika, wengine mnaumia.
Ni bora tuongozwe kama manamba ili maendeleo yetu (wananchi) yapatikane kuliko kukaa na chama ambacho watu wakiiba mabilioni, mkuu anatabasam na ukienda jela wamejaa wezi wa kuku na bata
 
UKABILA CHADEMA.....! Umezungumziwa na CHACHA WANGWE....SHIBUDA.....KAFULILA.... .etc LISEMWALO LIPO,NA KAMA HALIPO LAJA!!!
 
chadema hakuna ukabila

kinachowashinda wengi ni zile siasa za kubabaisha!!

Sasa wewe kama utataka cheo wakati huna maadili ya uongozi nani atakupa??!!

Hebu wanaotaka kuhama wahame haraka maana tupo wengi tuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
lazima tuseme ukweli,chadema ni chama cha kihuni tu,ni chama kilichojaa ukabila,hasa uchaga!wanaokihama wanaona mbali sana,acha watz wadanganyike,wachague hk chama 2015,wengi mtakuwa wapagazi wa wachaga,enzi za manamba zitarudi,mi niko ethiopia,kazi kwenu ndugu.

Kwani Sugu, Silinde, Mbasha, Zito, Mnyika wote wachagga? Kule Magamba ikoje, mbona majina yale yale? Nyerere, Mwinyi, Karume, Malecela, Mzinda, Nchimbi, huo ukabila au usisi? Acha hizo, Ethiopia njaa tu.
 
UKABILA CHADEMA.....! Umezungumziwa na CHACHA WANGWE....SHIBUDA.....KAFULILA.... .etc LISEMWALO LIPO,NA KAMA HALIPO LAJA!!!

Huyo Shibuda kafukuzwa huko kusiko ukabila, Kafulila alilia NCCR walipomfukuza sizungumzii CDM kwani ni watuhumiwa.. Uroho wa madaraka.
 
Back
Top Bottom