Wakuu,
Huu ndiyo wakati mzuri wa kuwatambua watu waliopo kwenye chama kwa mapenzi na moyo wa dhati wa kuhakikisha kuwa ukombozi wa watanzania maskini walio wengi unapatikana na wale waliopo kwa nia moja na kwa gharama yoyote ili wawe viongozi. Huyo dada amedhihirisha kuwa ni mwenye tamaa ya madaraka na hana subira. Watu wa namna hiyo ni bora wanapoondoka kwenye chama kuliko wakibaki kwani ni sumu mbaya sana. Ni bora uwe na wanachama waaminifu na wenye mapenzi mema wachache kuliko kuwa na wanachama wengi (kama ccm) ambao agenda au nia yao kubwa ni maslahi binafsi kama wanavyofanya mafisadi ambao wanaitumia ccm kama maficho ya biashara zao haramu.
Chama cha
demokrasia na maendeleo lazima kionyeshe demokrasia kwa vitendo. Inawezekana kweli alikuwa anatafuta madaraka ama ulaji, vyovyote utakavyoita lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba wanasiasa wote wako after ulaji. Hata Mh. Mbowe, Zitto, Dr. Slaa na wengineo wako after ulaji.
Ni haki ya kikatiba kila mtu kuchagua na kuchaguliwa, sasa kama ndani ya chama cha kidemokrasia hakuna demokrasia ya kuchaguliwa bali kuna demokrasia ya kuchagua tu, basi hapo kuna tatizo kubwa na lazima liangaliwe kwa jicho la tatu na kutafutiwa ufumbuzi. Hili tatizo la viti maalum liligonga sana vichwa mwaka 2005 na haikutegemewa kwamba mwaka huu tena lingeendelea kugonga vichwa vya watu.
Ingawa kunaweza kuwepo na sababu ya msingi ya chama kumtumia mtaalam (consultant) kuona namna bora ya kupata wabunge wa viti maalum lakini bado haiondoshi ukweli kwamba hapa demokrasia imefinyangwa.Kama akina mama wa chadema walimuona anafaa kuwaongoza basi kama hao hao wangemuona kuwa hafai kuwa mbunge basi hapo mama leticia asingekuwa na nongwa kwakuwa demokrasia ingekuwa imechukua mkondo wake.
Tusipende kuwa washabiki bila kufikiria, si kila jambo linalofanywa na viongozi wa chadema ni sahihi kwa kuwa hata wao ni binadamu wanakosea kama wanavyokosea wengine na kwa hili la viti maalum, mimi nasema wamekosea na wanatakiwa waandae utaratibu wa kidemokrasia wa kuwawezesha wananchama kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa, hapa hatuhitaji kuendeleza sera ya kuteuana kwa kisingizio kwamba mchakato wa kidemokrasia uliingia dosari.
Kama mchakato wa kidemokrasia uliingia dosari chama kiliwajibika kuweka mazingira ya demokrasia kuchukua mkondo wake na si kuuwekea kufuli. Na wala tusidanganyane hapa, hakuna mwanasiasa hapa tanzania anayefanya siasa bila kuangalia maslahi, hiyo haipo na kama kuna mtu anaamini hivyo, nampa pole.
Kwa maoni yangu sioni sababu yoyote ya kuanza kumshambulia mama wa watu kwa kuwa tu kaamua kujiondokea chadema baada ya kuona kwamba ndoto yake haitatimia, kila mwanasiasa natafuta nafasi ya kufikia malengo, mojawapo ikiwa ni ulaji kama anavyosemwa mama leticia,na tukimuangalia kwa mtazamo huo basi tusiishie kwake, twende mbele na tuwaone wote waliohama vyama kwa jicho hilo hilo moja la kutafuta madaraka na ulaji.