Lessons from Egypt and Tunisia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lessons from Egypt and Tunisia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Askari Kanzu, Feb 11, 2011.

 1. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Waungwana, ninapendekeza tuanzishe mjadala kuhusu ni mafunzo gani tunaweza kujifunza hapa Tz kutokana na mapinduzi yaliyotokea Tunisia na Egypt. Je mabadiliko ya namna hii tunaweza kuyaleta hapa kwetu?
   
 2. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kwa sasa waTZ tusione umuhimu, ila maisha magumu ndiyo yatakayotufanya kufuata ya Misri na Tunisia, na ukimya wa serikali ya Mzee JK kushindwa kuona umuhimu wa malalamiko ya wananchi haswa kwa kupewa taarifa zisizo sahihi na wasaidizi wake kama alivyofanyiwa Mzee Pinda juu ya inshu ya Arusha bungeni.
   
 3. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ni sawa hayo usemayo. Nimeona watu wengi wanasema viongozi wetu dniyo wajifunze na yatokeayo Tunisia na Misri lakini nafikiri ni sisi wananchi ndio haswa tunalo jukumu kubwa la kujifunza, kama kweli tunataka kujikwamua kutoka kwenye utawala mbovu!
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  :twitch:Naona kama Tunachelewa vile maana tukichelewa sana tu Watajilipa kupitia Dowans:target: Tulianzisheni na sisi tuwatimueni Mafisadi wote hata kama kuwachoma live poa ili mradi tusibakiwe na hata fisadi 1. :horn: ni muda wa kukutana na kufanya mabadiliko katika nchi yetu. Enough with CCM:laser: Can someone gim a date for revolution in Tanzania or link ya :A S 11:book or tweeter. Lini inaanza Revolution Tanzania?
   
 5. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kwa bahati mbaya huu ndio ukweli wa mambo. Tuko wazuri sana kwa maneno lakini vitendo hatuna. Na tutazidi kukandamizwa milele ingawa tumeshaona "live" matokeo ya nguvu za umma!
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi ni kati ya watu wanaopinga njia za fujo , vurugu na aina nyingine ya uhasama katika kutatua matatizo ya kijamii sehemu yoyote duniani haswa matatizo yanayohusu Jamii zinazokaa ndani ya mpaka mmoja zinazoongea lugha moja , tamaduni zinazofanana na pengine hata asilimia kubwa wale wanaoamini imani moja .

  Katika kipindi cha miezi miwili sasa tumeona jinsi Raia wa Tunisia walivyoandamana na kufanya fujo mbalimbali kwenye miji yao mpaka raisi wao aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 23 kuachia ngazi tukumbuke kiongozi huyu aliingia madarakani kwa umwagaji damu nae akatolewa kwa umwagaji damu vile vile .

  Tukio la pili ni hili Kiongozi wa Misri inayesemekana amekimbia nchi muda huu aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30 hivi inasemekana ana akiba ya dola bilioni 70 kwenye hifadhi yake ya fedha nchi kadhaa pamoja na vitega uchumi kwahiyo anaweza kuwa ndio mtu tajiri kuliko wote ulimwenguni .

  Wakati tukio la Tunisia lilianzishwa na Mmachinga aliyepigwa na kuswekwa ndani baaada ya bidhaa zake kukamatwa kwa kosa la kutembeza matunda hovyo barabarani tuchukulie mmachinga wa kwetu hapa Tanzania ana hali gani haswa .

  Wenzao wa Misri ni kama waliiga tu na walichochewa zaidi baada ya kuona mafanikio ya Tunisia kwa siku hizo 17 za maandamano yao inasemekana walikuwa wanapoteza dola mil 300 kwa siku moja kama hasara ingawa benki ya dunia imeahidi kusaidia kuipa misaada nchi hiyo zaidi kwa siku zinavyozidi kwenda .

  Kuondoka kwa viongozi wote hao huko Tunisia na misri sio suluhisho la matatizo ya kudumu ya nchi hizo zote mbili , wameshauwa watu mitaani na kusababisha hasara kubwa kwa baadhi ya jamii zingine na hata wenyewe wanaweza kuanza kupigana na kufungua mipaka ya ugaidi katika nchi hizo .

  Wakati marekani na Israel inahofia usalama wao endapo Islamic brother hood mshirika mkubwa wa hamas akishika nchi ya misri napo nchi za ulaya zinahofia kundi la alquida ukanda wa afrika kaskazini kujipanua zaidi nchi hiyo ya Tunisia na nchi jirani

  Kwetu chama tawala ndio kiko madarakani kwa kipindi kirefu zaidi toka kupata uhuru kuundana na Zanzibar na kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995 lakini mara zote uchaguzi umekuwa ukifanyika ingawa kumekuwa na matatizo ya hapa na pale ambayo yanaweza kutatuliwa kwa watu kukaa na kupanga mikakati imara kwa ajili ya maisha yajayo .

  Kwa watanzania wakawaida kilichotokea Misri na Tunisia sio cha kujifunza wala kuiga angalau kwa sasa , historia ya nchi yetu inaonyesha jinsi tulivyokuwa imara ndani ya nchi hata pale tulipoenda kusaidia nchi zingine kujikomboa toka kwa wakoloni na viongozi wengine walioshikilia madaraka kwa njia ambazo si halali na siku za karibuni tu tulienda kuwapatanisha Wakenya .

  Kwetu bado tuna njia nzuri na rahisi ya kufanya tukiamua kuacha tofauti zetu na ubinfsi tuna nafasi kubwa ya kufanya kazi pamoja na kushiriki uchaguzi ulio huru na haki na kuleta mabadiliko kwa njia hiyo lakini hiyo haimaanishi kwamba maisha ya mtanzania yatakuwa mazuri au wale walioingia na vyeti bandia makazini watakuwa na vyeti vya kweli .

  Bado tunakazi za kuipa elimu idadi kubwa ya watanzania na kuwaweka tayari katika ushindani wa kibiashara na masuala mengine katika eneo la afrika mashariki na kusini kwa afrika bila kusahau dunia nzima kwa ujumla .

  Hatuna cha kujifunza kutoka nchi hizi mbili pengine wao ndio watuige sisi katika masuala kadhaa ambayo yanazungumzika .
   
 7. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kaka ilo suala la kusema ana utajiri wa $70 billioni napingana nalo
   
 8. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa mtaji huo wa hiyo article yako unamaanisha watanzania watulie, wawe wapole na kuendeleza amani, na wasiwe na kero yoyote kwa serikali yao na waendelee kuwa mazuzu na kuendelea kuibiwa mchana kweupeeeee? Akina Rostam/Dowans na wengine waendelee na kuibomoa na kuiibia hii nchi kama shamba la bibi halafu wadanganyika waendelee kukaa kimya? Mwisho wa tunakoelekea hii nchi itakuwa kama Haiti!

  Unamaanisha nini unaposema hatuna cha kuwaiga Tunisia/Egypt ila watuige sisi? Watuige sisi kwa yapi? Ujinga na uzuzu wetu?

  Kumbuka: Freedom/Liberty comes with a price.
   
 9. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naona hujui unalosema ama umetumwa!
  Au utakuwa ni kati ya wale misukule ya mheshimiwa 'sijui'
   
 10. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matatizo yaliyosababisha kutokea kwa mabadiliko kwenye nchi hizo ni sawa na haya tuliyonayo! Hakuna uchaguzi wa huru na wa haki, Tume ya taifa ni ya CCM, maisha yanazidi kuwa magumu wakati JK anawakumbatia mafisadi na kupora rasilimali za taifa kupitia Dowans, Meremeta, etc, Bei za vyakula na utilities zinazidi kupaa na serikali haina strategies zozote, Polisi wanaua raia na wanapongezwa na serikali na CCM.

  Ki msingi tuna mambo mengi ya kujifunza kama wananchi na serikali pia. Kwa wananchi, huu ni mfano mzuri kuwa nguvu ya umma inahitajika kuiondoa madarakani serikali hii jeuri, katili na inayo wakumbatia mafisadi akina ROSTAM AZIZ (ambaye ni raia wa Iran). Kwa upande wa serikali inabidi wajue kuwa utawala wa kiimla una mwisho mbaya na risasi, na mabomu wanayojivunia, si chochote kwa nguvu ya umma!!.
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  SHY,

  HAPANA, nasema hapana.

  Tunayo mengi sana ya kujifunza kama nchi/wananchi kwa kilichojiri katika nchi za kaskazini mwa afrika. miaka ya awamu ya tatu na awamu ya nne kumetokea hali ya wimbi zito la ufisadi na rushwa, huku hali ya pato la mtanzania ikiwa ni chini ya dola 1. Elimu yetu inazidi kudorora, miundombinu na nishati (umeme) pia ni kubahatisha kwa miezi inakimbilia mitatu sasa. Uchumi unayumba, nidhamu hakuna serikalini, bungeni ndio usiseme na hatujui sijui hili bunge la kumi kitaishaje kama haitokuja kupigwa kura ya kutokuwa na imani na viongozi fulani.

  KUNA MENGI SANA YAPO HAPA, YANAHITAJI COMPREHENSIVE CHANGES ....mbona pale Libya yule Muammar ameifanyia mazuri saaana kwa wananchi wake, japo ameitawala nae takriban miongo minne kama si mitatu waila NCHI YAKE IPO VIZURI SAANA KIUCHUMI NA MIFUKONI.
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kwa ufupi watu wazima ndivyo wanavyosema lakini si kweli!!.

  Mwandikaji ni lazima ana miaka isiyopungua 40 kwani vijana wengi Africa nzima hawafikirii hivyo. Mubarack ameweza kukaa miaka 30 kwasababu ya fikra kama hizo, hata hapa Marekani watu wa makamo walikuwa wanasema Obama hawezi kushinda!!. Vijana wako tofauti na kama panga ndiyo njia pekee ya kukata rushwa na kuleta maendeleo bali panga litatumika kwani kuna sababu gani ya kuishi kama kizazi kijacho kitakuwa katika wakati mgumu kuliko sisi??. Ni bora ufe kwa kitu unachokiamini kuliko kuishi kwa majonzi na kulalamika kila siku.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kuna mengi kujifunza kutoka zote Misri na Tunisia. Viongozi ni lazima watawale kwa ridhaa ya watawaliwa. Consent, wanaita wenzetu Waingereza. Pili, viongozi wasitumia nafasi za uongozi kujitajirisha wao na familia zao. Ndiyo yaliyompata yule wa Tunisia na familia yake. Tatu viongozi tumewachagua kushughulikia matatizo yetu kwanza.

  Tunawalipa vizuri na kuwapa makazi mazuri ili watutumikie. Ikifika wakati viongozi wanajiona sisi ndio watumishi wao, mali zetu ni mali zao, matatizo yetu si matatizo yao, basi yale yaliyotokea Tunisia na Misri kwa hakika yatatokea kwetu. Hilo ni somo kwa viongozi wote.
   
 14. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Cha kujifunza ni kwamba Hosni ametawala miaka 30! Hiyo pia ni sawa na miaka ya ccm madarakani! Kama wamisri wamesema Mubarak enough is enough hata sisi karibia tutasema ccm enough is enough ! Kwa sasa bado tunasubiria na kungojea muanzilishi! Hii ikitokea mafisadi lazima wajisaidie ndani ya kaptula zao
   
 15. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wewe Shy umelewa au umevuta? Naona ni kweli kama jamaa mmoja alivyosema, inaonekana unayo mawazo ya kizee. Sawa mzee, sikulaumu. Endeleza fikra za kidumu. Lakini elewa umepitwa na wakati!
   
 16. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
 17. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada usitake kupotosha watanzania; ukweli ni kwamba yaliyotokea Tunisia na Leo Misri ni somo la kutosha kwa viongozi sio tu wanaong'ang'ania madaraka lakini pia MAFISADI. Nikuulize; hivi utakaa meza moja na mafisadi mjadili kitu gani; hivi kama tuliowachagua kuongoza wamegeuka waporaji na wafilisi wa watanzania unakaa nao meza moja ili arudishe alivyopora au kumtaka mwizi CCM na serikali yake wageuke waungwana?.

  Hii siyo rahisi na ukikaa meza moja utacheleweshwa tu na porojo na kuahirisha miaka nenda rudi na utabaki palepale. Dawa pekee ya hawa viongozi wa kizazi hiki hasa wale walevi wa madaraka na wezi ni kuwatoa kwa lazima wakae pembeni ili waadilifu wapewe nafasi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa ufupi tunahitaji kupata uhuru kutoka katika mikono ya viongozi wezi na wabadhilifu wasiojali wananchi wao ikiwamo CCM na serikali yake
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naomba nikurekebishie tu kakipengele kwamba Mubarak anashika nafasi ya saba duniani akifungamana na wafanyabiashara wengine watatu maarufu duniani.
   
 19. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  For me:


  1. This revolution was leaderless! When wananchi decide that enough is enough, there is no power of oppression or coercion that can defeat them.
  2. During the great time of a nation's self determination and revolution such as that we have seen in Egypt, it is neither the NGOs nor the political parties that are at forefront, it is the people. People themselves become the leader and the lead.
  3. It is not possible in the contemporary world that you can cling to power undemocratically. Democracy is the only way. Yes, African leaders will fake and manipulate the people, but this will never continue for ever. They have no option but to truly democratize their countries or else they will face a shameful defeat by the people. In today's world, you only lead so long as you have the public confidence and support.
  4. Every struggle requires some sections of people to sacrifice, as Steve Biko once said: there is no struggle without casualties. This revolution has taken a 30 year old Wael Ghonim, to lie to his employer, the Google, that he was returning home in Egypt for what he called ' a personal problem'. He left his lucrative career to return home to join the unemployed and downtrodden youth to oust a dictator.

  I salute Wael Ghonim, I salute the people of Egypt
   
 20. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  So Tanzania tutulie kama mashoga tu sio? hivi huwa sheria na mazungumzo yapi unayoyazungumzia acha upuuzi..
  mie niko tayari kuanza na tahira kama nyinyi haiwezekani usiwe unatumiwa wewe! au kama si mwendawazimu basi una lako jambo.

  Haiwezekani nchi imepigwa gia ya reverse gia za gari kwenda mbele zimengolewa wakati majirani zetu wanaongeza gia na gari zao zina speed nzuri wewe bado unangangania sie tu ndo gari iwe na gia moja ya reverse sio ..mamae zako na waambie hata TZ tunatamani kichizi iibuke the Tunisia na Egypt ...u gonna fool no one here..Mrs someone...
   
Loading...