Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Siku zote mtu asiye na busara, hata akitembea kwingi huko duniani, hutokea kuona mengi, kuvutiwa na mengi zaidi na HUSAHAU MENGI vile vile kisha mwisho wa siku HUKOSA MENGI ya kujifunza kwa namna yoyote ile.Mtoa mada usitake kupotosha watanzania; ukweli ni kwamba yaliyotokea Tunisia na Leo Misri ni somo la kutosha kwa viongozi sio tu wanaong'ang'ania madaraka lakini pia MAFISADI. Nikuulize; hivi utakaa meza moja na mafisadi mjadili kitu gani; hivi kama tuliowachagua kuongoza wamegeuka waporaji na wafilisi wa watanzania unakaa nao meza moja ili arudishe alivyopora au kumtaka mwizi CCM na serikali yake wageuke waungwana?.Hii siyo rahisi na ukikaa meza moja utacheleweshwa tu na porojo na kuahirisha miaka nenda rudi na utabaki palepale. Dawa pekee ya hawa viongozi wa kizazi hiki hasa wale walevi wa madaraka na wezi ni kuwatoa kwa lazima wakae pembeni ili waadilifu wapewe nafasi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa ufupi tunahitaji kupata uhuru kutoka katika mikono ya viongozi wezi na wabadhilifu wasiojali wananchi wao ikiwamo CCM na serikali yake
HATA NA MIMI NINGEKUWA NAJUA UTAMU WA UFISADI KUTOKA HATA KWA NYUMBA
YA JIRANI TU WALA NISINGERUHUSU KUFUNGUA AKILI YANGU KUJIFUNZA LOLOTE
TOKA TUNISIA NA MISRI - NI AMANI ALIMRADI KULA YANGU INA UHAKIKA!!!
Wala sijashtuka kitu baada ya kusoma kwamba KISHINDO KILICHOTETEMESHA BARA LOTE LA AFRIKA NA GHUBA kiutawala bado na hapa kwetu Tanzania kuna watu ambao HAWAKUJIFUNZA CHOCHOTE KITU.
Huyu mpenda amani wa nchini kwetu lakini bila halki aonekana kustaajabu sana kinachowakereketua watu mpaka kwenda kuandamana mtaani. Napenda nimhakikishie kwamba kwenda mtaani si kama uamuzi wa kwenda disko Billcanas na wala haalikwi mtu huko.
Njaa, dhuluma, maonevu yakija kukufikia pomoni --- sawa na jinsi ambavyo MTU FULANI MWENYE BUSARA FUPI ALIVYOJIPANGA HIVI SASA kila idara Bungeni Dodoma akiinuia kuziba njia zote za UMMA KUSIKIKA WALA KUPITISHIWA MATAKWA YAO (Juhudi hizo wengine tunaziona kama kujaribu kujuia jua vile na ungo mwanga wake usifike duniani), kiburi, visasi, upendeleo, ujanja ujanja wa kuzuiya kusikilizwa --- mwenyewe tu utajikuta msitari wa mbele ukiongoza na kusema; aheri ya kufa kishujaa kwa sababu ya msingi kwa taifa kuliko kuishi kwa aibu kwa maslahi ya ma-mishenitauni wa kwenye misuti ma-ofisini!!
Usinisbughudhi na swali kutaka kujua kama huyu MLETA HOJA ni miongoni mwao MAFISADI wa nchi hii amba usiku huu wa leo wataelekea kitandani kulala huku mioyo ikidunda kuhusu MWELEKEO WA KAULI YA MAMA CLINTON JUU YA 'PERFECT STORM OF CHANGE' na jisi vijana wadogo wadogo walivyofanya maajabu huko Tunisia na Misri kuleta mabadiliko wanayoyataka.
Ni kweli kabisa kwamba huyu mwenzetu 'MPENDA AMANI BILA HAKI' asingeweza hata kidogo kujifunza kitu huko kaskazini mwa Afrika. Kwa wenye maono haba, usiku wala huwa hauna tofauti na mchani - kwani yote si ni majira tu katika siku!!!