OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,433
- 104,771
Hakuna shaka wanafanya kazi kubwa kuokoa maisha yetu. Mungu awabariki sana kwenye hilo. Lakini kama binadamu wengine nao wana mapungufu. Wengine mapungufu makubwa zaidi mpaka unajiuliza huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiri. Ninayo machache ya kushangaza kwa hawa ndugu wakiwa anga zao;
1. Baadhi hawataki kusikiliza ushauri wowote toka kwa mgonjwa kama yeye ni mungu mdogo.
Wapo madaktari wamewaletea madhara makubwa wagongwa kutokana na kutowasikiliza. Mgonjwa mmoja alimwambia daktari asimchome hiyo sindano humletea madhara. Dr akakaza shingo, leo hii mgonjwa kavimba mwili mzima.
2. Kulazimisha ndugu asisogee wakati wa round wodini. Kwangu huu ni utoto. Mimi ndiyo ndugu nina haki ya kusikiliza maelekezo na hali ya mgonjwa wangu. Nina haki ya kusema juu ya maendeleo yake na hata kutoa ushauri. Kwanza mgonjwa mwingine unakuta hajiwezi, hana uwezo wa kujieleza. Daktari anakwambia toka nje.
Kuna siku nikamgomea kutoka akawa mpole.
3. Ubishi wa kijinga
Yupo daktari aliwahi kuacha kitambaa tumboni wakati wa operesheni. Mama yule akamweleza daktari baada ya maumivu kuzidi. Daktari hakufanya uchunguzi wowote. Mama akaenda hospitali ya rufaa wakakuta kitambaa. Akamrudia daktari mkuu basi wamrudishie gharama, wakakataa. Mama akasikiwa na wakili kesi ikaenda mahakamani wanadai 100m.
Vuta nikuvute ikaamuliwa walipe 50m.
4. Muda wa kuona wagonjwa
Wakati huu wa masika unakuta mvua inanyesha huwezi kuleta msosi kwa wakati. Unakutana na nesi anakaza hakuna kupita. Sasa mgonjwa afe njaa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
Ongeza na zako....itaendelea
Ushauri
Usimuone daktari kama mdogo wake Mungu ukamuamini kwenye kila kitu, hasa hawa dot.com. Hakikisha unachanganya na zako au unakuwa na mtu wako pembeni wa kupima mwenendo wa matibabu