Leo ninepigwa roba ya mbao na Panya Road

Duh kama wana hio michezo ni hatari. wazazi muhimu sana kulinda watoto kipindi hiki.

Hicho kikundi hatari
 
Sasa hayo majina yao uliyajuaje???
 
Pole sana, hangaya amewaomba hao panya rodi waache hayo mambo, au hawakusikia...
 
Hili kundi la Vijana, huenda Ktk kupambana nalo , mawazo ya haraka haraka ni "Wachomwe moto tuuu, wapigweee ,wauwawe n.k"

Lkn ukiwatizama Hawa Vijana ni miaka Kati ya 15--24.

Rais Magufuli , Alipambana sana na Madawa ya kulevya yote Kwa aina zake !!!

Rais Magufuli, kupitia Aiyekua Mkuu wamkoa Paul Makonda, walihakikisha Wajane wote walokimbiwa na waume zao, walotekezwa wanapata haKi zao.

Rais Magufuli kupitia Aliyekua Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, waliwawajibisha kisheria wale wanaume walokimbiwa majukumna kutelekeza na kuzalisha ovyoovyo

Rais Magufuli Kipenzi Cha Hawa Vijana Wanyonge, alihakikisha Jeshi la Polisi inafanya kazi Masaa 24, licha ya kutowaongeza Mishahara, Polisi walipewa nguvu, Moyo, na Uhuru wa kutumia weledi wao Kwa kuelimisha na kutumia nguvu palipohitajika.

Nyie Wanaume wa Dar, mkiongozwa na Makala, na Mama,. Jitafakarini,,,kwann haya hayakuwepo wakati wa Chuma JPM????
Yalikuwepo sema kwa uchache

Mfano kama mmoja wao akiuliwa na wakienda kuzika basi wakitoka mazikoni lazima watembeze paratuni au wakitoka kwenye mechi

Sema saizi kama imekuwa waziwazi sana
 
Kama ni kweli; suluhisho pekee ni kuwepo na operation ya siku tano tu, mtaa kwa mtaa, usiku na mchana kwa jeshi, tatizo lote litakuwa limeisha
 
Mimi nakaa kipati. Juzi katika shughuli zangu maeneo ya Mbagala Rangi Tatu nikasema ngoja niende kwanza stand kuu nikanunue mazaga zaga ya kula ili bachela mimi nije kula geto.

Ile kufika tu nikanunua mazaga yangu ya kumwaga hadi hela nilizoenda nazo zote nikaishiwa.

Nikaanza safari yangu kutoka rangi tatu hadi kipati kwa mguu ila nikasema ngoja nipite mitaani njia za shortcut, kupita vikona kona nikakutana na vikundi vya watoto watoto wanabishana. sema nilikua na mishe zangu sikuwatilia maanani ile napita walivyoniona mmoja wao akanifata akaniambia bro nitoe mia. nikamwambia kwa hapa sina akatokea mwingine akaniambia mbona unapita sehem za alafu sisalimii ile nataka kumjibu nikashitukia roba la mbao tayari hadi siwezi kufurukuta ikabaki napiga kelele huku sauti haitoki macho yashakua makubwa mikono inazunguka tu.

Wakanipora mazaga zaga yangu niliyoyanunua wakanipiga kinyama mtu mzima mimi na mindevu yangu. mmoja akatoa kisu akataka kunichoma ila ashukuriwe mwenzao anaitwa mohamed ndo akamzuia ila yeye akatoa wazo wanipake mafuta nilivyosikia hivyo sikuamini macho yangu[emoji27][emoji27][emoji27]

Mohamed akamwambia mwenzake anaitwa Yohana akanunue mafuta. na wengine wanibebe wanipeleke kwenye jumba bovu. sijui nilipata nguvu wapi nilikimbia kama mwehu yani[emoji22][emoji22][emoji22][emoji26][emoji26]

Nilivofika geto ikabidi nianze kujicheka tuu kwa yaliyonikuta ila kwa nini haya mambo yamekuja sanaa kipindi kama watoa figo, watekaji watoto, hamza na panya road na mbwa mwitu wamefufuka kwa spidi mwaka huu

[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji22][emoji24]
haya
Screenshot_20220503-145725.jpg
 
Siku nikikutana nao,Nasali sala ya mwisho Nakufa na wawili tutajuana Kwa Sir God!
 
Kwa hii trend ya matukio ya panya road siku hizi,wacha tu nianze kurudi kwenye mazoezi makali ya martial arts

Siku tukikutana kwenye 18 na hao watoto na mapanga Yao atajulikana Nani bwana butcher na Nani atakuwa kitoweo..Hakuna namna sasa

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Uhakikishe una train jinsi ya kupoka silaha, nankicheza nazo. Maana huo mziki Nimeamkia kucheza nao,

Kuzipangua na kuzipora kuzitumia na kukwepa, sometimes hata kurusha Ili ikamchome mkorofi wao, matumizi ya silaha ni muhimu sana.

Nimeamua kutafuta gongo na mti kama bakora na namna ya kucheza nazo.

Tatizo najifunzia nyumbn peke angu Sina trainer, na Wala sijawahi kuJifunza, nimeonaga kwenye movie tu
 
Nilikuwa nafanya,majukumu yalkawa mengi nikaacha Kung fu..

Km unataka kujifunza tafuta mwalimu,kujifunza mwenyewe Kwa kupitia muvi huwezi kumaster chochote Mzee
 
Mkuu hao madogo walikukaba maeneo gan maana rangi tatu mpka kipati shotcut hamna ni road kwa road tena usiku.. na sizani kama kuna madogo wa hivyo maeneo hayo maana kutoka Tudo mpka kizuiani ni full viwanda hamna hata nyumba maeneo hayo kizuian kuna kituo cha polisi pale sio rahisi kufanyiwa tukio kwa wakati huo na kituo kimachofuata ni kipati ambapo ndio mtaan kwako umekabwa maeneo gani mkuu? msukule mzembe
 
Pole sana na inasikitisha sana... walitaka wakupige hamza kanuni...

Wamekubia wamekupiga na bado wamekutamani...
 
Mimi nakaa kipati. Juzi katika shughuli zangu maeneo ya Mbagala Rangi Tatu nikasema ngoja niende kwanza stand kuu nikanunue mazaga zaga ya kula ili bachela mimi nije kula geto.

Ile kufika tu nikanunua mazaga yangu ya kumwaga hadi hela nilizoenda nazo zote nikaishiwa.

Nikaanza safari yangu kutoka rangi tatu hadi kipati kwa mguu ila nikasema ngoja nipite mitaani njia za shortcut, kupita vikona kona nikakutana na vikundi vya watoto watoto wanabishana. sema nilikua na mishe zangu sikuwatilia maanani ile napita walivyoniona mmoja wao akanifata akaniambia bro nitoe mia. nikamwambia kwa hapa sina akatokea mwingine akaniambia mbona unapita sehem za alafu sisalimii ile nataka kumjibu nikashitukia roba la mbao tayari hadi siwezi kufurukuta ikabaki napiga kelele huku sauti haitoki macho yashakua makubwa mikono inazunguka tu.

Wakanipora mazaga zaga yangu niliyoyanunua wakanipiga kinyama mtu mzima mimi na mindevu yangu. mmoja akatoa kisu akataka kunichoma ila ashukuriwe mwenzao anaitwa mohamed ndo akamzuia ila yeye akatoa wazo wanipake mafuta nilivyosikia hivyo sikuamini macho yangu[emoji27][emoji27][emoji27]

Mohamed akamwambia mwenzake anaitwa Yohana akanunue mafuta. na wengine wanibebe wanipeleke kwenye jumba bovu. sijui nilipata nguvu wapi nilikimbia kama mwehu yani[emoji22][emoji22][emoji22][emoji26][emoji26]

Nilivofika geto ikabidi nianze kujicheka tuu kwa yaliyonikuta ila kwa nini haya mambo yamekuja sanaa kipindi kama watoa figo, watekaji watoto, hamza na panya road na mbwa mwitu wamefufuka kwa spidi mwaka huu

[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji22][emoji24]
mkuu nina mashaka ujapakwa mafuta kwel...!!!
 
Back
Top Bottom