Leo nimemuacha mpenzi wangu rasmi

Huyu dada nilikuwa nampenda Sana na kwa muonekano alikuwa ni wife material.

Licha ya kuwa nilimpenda na nimekuwa natoa hela ya matumizi Ila akawa ananipikia ugali na mboga za majani, yeye na mwanaye wanakaanga ndizi, viazi ulaya na nyama wanaweka na kachumbari. Siku akinipikia wali nyama, wao wanakula wali nyama na matunda/ juice. Yaani Ni lazima aweke utofauti kwenye mlo wangu na wa kwao. Nimemuonya mara nyingi aache ubaguzi maana hela ya chakula siyo yake iweje wananibagua? Lakini hakusikia

Nikaona niwafukuze tu

Tumezozana usiku wa kuamkia Leo hataki kutoa vitu nje lakini nimemshinda.
Niamini mimi hamuwezi kuachana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Bahati yako, hapo amekufanyia wewe mtoaji pesa!

Ndo unaoa sasa, hafu hafu ndugu zako, ama Mama yako Mzazi katoka Kijijini kuja kuwasalimia Mjini.......!
 
Pole gentleman,
ungemtuma akapumzike au akapate kalikizo kidogo kwao , then akirudi mnakaa na kukubaliana jinsi ya utaratibu wa kula hapo nyumbani, na unampa utaratibu mathalani wa kula chakula pamoja mfano chai, lunch au dinner..

Ni ngumu kukutana kwenye milo hiyo mitata but ile ambayo unaweza..

Hii ingesaidia kuondoa hiyo changamoto kidogo
Kama ana tabia hizo hata mkae Vikao vikisimamiwa na UN hawezi kubadilika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom