Leo nimemkumbuka member wa JF Folk (RIP)

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,045
Tukiwa humu tunakorofishana tunatukanana muda mwingine na muda mwingine tunafurahi pamoja, ni kama vile tuko kwenye metaverse. Unaweza pretend you have it all, umefanikiwa, umesoma sana you can be anybody.

Lakini ukweli tunaujua sisi wenyewe.

Leo nimekutana tena hii thread ya aliyekuwa member mwenzetu Folk (Rip) Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nikakumbuka enzi zake kuanzia 2013 alikuwa anajaribu kutueleza anachopitia, lakini wengi wetu tulimbeza.

Hata 2018 aliweka thread yake ya mwisho kutuambia kuwa siku zake kuishi zimefika ukingoni bado kuna ambao hawakuamini akaendelea kubezwa.

Lakini huwezi kulaumu watu kwa kufanya vile maana utapeli mtandaoni umekomaa.

Ila ikitokea mtu kaomba msaada kama unaweza kumsaidia msaidie tu kama akiwa tapeli basi atajuana yeye na Mungu wake.

Kuna watu wengi wanakuwa na shida kweli sema tunawakatisha tamaa zaidi.

Rip Folk, Rip Warumi, only the dead have seen the end of war.

Thou apart, we are still a team

In the end life signifies nothing
 
Tukiwa humu tunakorofishana tunatukanana muda mwingine na muda mwingine tunafurahi pamoja, ni kama vile tuko kwenye metaverse. Unaweza pretend you have it all, umefanikiwa, umesoma sana you can be anybody...
Life is unknown journey.

Mungu ndy ajuaye mkuu.

RIP members wote waliotangulia ktk safari ya lazima kwa kila chenye uhai.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
“Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;”
‭‭Ayu‬ ‭14:1-2, 5‬ ‭
 
“Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.

Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.

Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo. Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka. Maana tumetoweshwa kwa hasira yako, Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa. Umeyaweka maovu yetu mbele zako, Siri zetu katika mwanga wa uso wako. Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.

Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.

Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako? Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako? Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.”
‭‭Zab‬ ‭90:1-12‬
 
“Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.”
‭‭Mhu‬ ‭9:9‬ ‭
 
Back
Top Bottom