Leo nimemkumbuka member wa JF Folk (RIP)

Mimi nimesoma na imani ya Kiislamu na Kuswali pia, japo nimezaliwa katika imani ya Kikristo. Now napenda soma mambo ya Kihindu in my free time.
Uko kwa ajili ya kutafuta ukweli huko au ni more of adventure?
 
Mkuu, katika kusoma soma nilikuja soma kwenye vyanzo mbalimbali kuwa Jehanamu yani Hell limetokana na Jamaa anaitwa Dante wala halikuwa kwenye Biblia.
Dante unamaanisha inferno? Dante ni mtu wa karne ya 14 na Yesu aliongelea Jehanamu karne ya 1 hii ni tofauti ya karne 13, yaani miaka 1300.

Ni kwamba kwenye toleo la mwanzo la Biblia ya Hebrew kwenye Agano la kale "Hell' ilikuwa ni "She'ol" ambapo ina maana ya "grave" yani kaburi
Kuna sehemu Hell ni Sheol na kwa Biblia ya kiswahili imetafsriwa ni kaburi. Lakini sio maana pekee ya Hell
"abyss" shimo refu. Katika kutafsiri ikatafsiri kama "Hades" kwa Kigiriki ambapo hilo neno Hades katika hadithi za Kiimani za Kigiriki limeambatana na mambo ya kuzimu na stori za kutisha.
Uko sahihi kwa kiasi fulani. Labda nikupe mifano. Ya Jehanamu ambayo aka yake ni Ziwa la moto

Marko 9:43-44
"Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki"

Hapa Yesu alikuwa haongelei Sheol, au abyss. Hapa alikuwa anongelea sehemu ambayo ni mbaya kiasi kwamba bora upoteze viuongo vyako lakini uiepuke. Haiwezi kuwa kaburi ambapo mwili unalala na ku disintegrate kwa sababu amei qualify kuwa ni sehemu ambayo kuna moto usiozimika, na funza wa huko hawafi.

Yesu alikuwa anaongelea sehemu ambayo binadamu hawajawahi kuiona na haina mfanowe hapa duniani. Kwa hiyo kuwalezea alitumia mfano wa bonde la Hinomu ila akawaambia kule moto hauzimi wala funza hawafi. Unaweza kujifunza juu ya bonde la Hinomu kupata picha ambayo Yesu alitaka tuione.

Lakini pia kuna sehemu nyingine zinaelelezea ikiwemo Ufunuo 20: 11-15
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Unaona hapa ni utimilifu wa kile Yesu alikuwa anaonya. Hapa linatajwa kama ziwa la moto. Kaburi haliwezi kuwa ziwa la moto. Kuna ziwa la moto limeandaliwa na inatupasa kuliepuka. Njia ya kuliepuka ni moja tu, Kristo Yesu.

Kuna Selo ya muda kwa wafu wakisubiri hukumu ya mwisho, nayo kiingereza wanaita hell. Kiswahili tunaita kuzimu. Huko nako sio kuzuri hata kidogo. Ukiweza soma Luka 16, utaiona hii

 
Nikiwa natafta ukweli uwa sitaki kuacha any stone unturned.
Ni vyema sana. Nikutakie heri kwenye safari yako hiyo. Kama utahitaji any information on any topic send me email raccqa@gmail.com

Kuna kipindi nilikuwa nikipata muda naandika kidogo, zilivykuja zile sheria za kutubana nikaacha. Angalia kama unaweza kupata kitu
 
Ni vyema sana. Nikutakie heri kwenye safari yako hiyo. Kama utahitaji any information on any topic send me email raccqa@gmail.com

Kuna kipindi nilikuwa nikipata muda naandika kidogo, zilivykuja zile sheria za kutubana nikaacha. Angalia kama unaweza kupata kitu
Asante mkuu ngoja nipitie na ntakutafta nikikwama
 
“Ila ikitokea mtu kaomba msaada kama unaweza kumsaidia msaidie tu kama akiwa tapeli basi atajuana yeye na Mungu wake.”
 
Doh Warumi nae alishafariki.


 
Nadhani maswali ni mengi na mengine kuandika hapa itachukua muda. Kama utakuwa willing tunaweza kuwasiliana kwa email raccqa@gmail.com ili kuweza kuwa na mtiririko wa maswali na majibu. Ni rahisi maana hapa kuna comments nyingi na zinatembea haswa.

Ila swali la mbing nimegusa hapo ju, pamoja na Jehanamu. Kuhusu ulimwengu ujao ni wakati ambao historia itafikia mwsho. Wakati kuna kipindi haukuwepo then ukawepo na kuna kipindi utafika mwisho. Na hapo ndipo Utakuja ulimwengu wa umilele. Ambao kila mtu kwa uamuzi wake ataishi huko pasi na mwisho. Ukisoma ufunuo sura ya 21 na 22 itakupa hint ya ulimwengu ujao.
Asante.nitasoma kwanza ufunuo hizo sura.
 
Nililia kwa sauti nilipo soma huzi wa jamaa kuanzia pale maisha yangu yalibadilika namlilia Mungu nimalize mwendo salama
 
Back
Top Bottom