Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,770
- 121,825
Wanabodi,
Declaration of interest. Mimi ni mwandishi wa kujitegemea, kule newsroom tunaitwa freelance lakini sasa wanatuita wapiga dili za habari!, na kufuatia ukame wa habari, tumepigika kweli kweli hadi tunatunga habari za mayalla (njaa)!.
Kufuatia kupigika sana Januari hii, Usingizi ulinikatikia usiku manane, nimegala gala wee kitandani mwisho nimeshuka JF ndio nikakutana na topic iliyonifanya kupandisha uzi huu.
Kiukweli kabisa Tanzania hapa tulipo sipo, kuna mahali tulipaswa tuwepo lakini bado hatujafika, iii tuweze kufika pale tunapaswa, tunahitaji nguvu ya Mungu kututoa hapa na kutufikisha kule tunakopaswa kuwa, kama Mungu alivyo watoa wana wa Israel utumwani Misri na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi, nchi ya Caanani, nchi ya maziwa na asali.
Vivyo ilivyo, Tanzania sio masikini!, Tanzania ni tajiri!, Tanzania ni nchi ya ahadi, mabomba nchi nzima yalipaswa kutoa maziwa na asali. Ili kufika kule tulikopaswa kuwepo, taifa linahitaji mtu sahihi wa kutuongoza kwa Mungu Baba kututumia nabii wa kweli wa kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwapo.
Japo kwa sasa rais wetu ni Rais John Pombe Joseph Magufuli, hadi sasa bado sina uhakika sana kama rais Magufuli ndiye nabii aliyeletwa na Mungu, ili kutufikisha kule kwenye nchi ya ahadi tunakopaswa kufika kwa sababu, mara kwa mara bado mnamsikia rais wetu Magufuli akituomba Watanzania tumuombee, kuashiria hata yeye bado hana uhakika kama ndiye yeye au siye yeye, ndio maana bado anahitaji nguvu za Mungu ili kumpatia unabii wa kuifanya kazi ya Mungu kwa taifa hili na Mungu kuweza kumpigania ili aweze kuishinda vita iliyo mbele yake ya kuifikisha Tanzania kule inapaswa kuwa, Tanzania ya neema kwa mabomba nchi nzima kutoa maji, maziwa na asali, huku mana zikishuka kutoka mbinguni!. Hii maana yake Rais Magufuli ni Musa wetu tuu, Joshua wa kutufikisha nchi ya Caanani bado yuaja!.
Awamu ya Tano ilipoanza kwa kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tuu" ikaanza kwa Mhimili wa Serikali kuisigina katiba, huku mihimili ya Bunge na Mahakama yenye the role of Checks and Balances under the principle of "the separation of powers" imekaa kimya ikiangalia tuu!. Ukaja mhimili wa Bunge ulioridhia ile "Open Goverment Initiative" kwa nchi yetu kufanya kazi kwa uwazi, sasa badala ya kufanya kazi kwa uwazi, sasa Bunge linaendeshwa behind the closed doors kwa kuzuia matangazo ya moja kwa moja, na kupitisha miswada ya muhimu kwa mtindo wa "fast track" kwa hati ya dharura, bila kujadiliwa na wadau ili kutimiza hapa kazi tuu!..
Baada ya mhimili wa serikali kufanya mambo ya kiimla, sasa ni zamu ya Mhimili wa Mahakama tukishuhudia danadana ya kuchezea haki ya mtu, ambayo imetolewa kama right kwa mujibu wa katiba lakini sasa mhimili wa mahakama, unazigeuza haki zilitolewa na katiba kuzifanya sasa ni hisani, yaani inazifanya ni favour!.
Jana tumeshuhudia mahakama imeanza kutoa hukumu za "fasta fasta", hukumu za "hapa kazi tuu" kwa kuanza na Mbunge wa Kilombero, huku Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema anaeozea mahabusu akisubiri kufuatia!, kosa la Lema ni kuota ndoto na kuisema!. Kiukweli kuna ndoto nyingine ni ndoto tuu za mtu kuota na kuna ndoto nyingine ni ndoto za unabii!. Mtu unapoota ndoto ya unabii inakupasa uiseme, ili wahusika wausikie huo unabii na kuufanyia kazi kama ile ndoto ya Farao, Yusufu akaitafsiri ikaiokoa dunia!.
Kwenye hili la mhimili wa mahakama kuchezea haki za raia, mhimili wa Serikali utanyamaza na mhimili wa Bunge utanyamaza!. Where is the doctrine of separation of powers?!, where is the checks and balance?. Who will check who na bila kuwepo balance mambo si yatakuwa vululu vululu na vurugu mechi kwa jahazi letu kwenda mrama huku likinesa nesa?, jee hatuna hatari kweli ya jahazi kuja kupinduka au kuzama kabisa huko mbele ya safari na nahodha kuja kujitosa baharini?, au aliyemleta nahodha huyu, atamtosa baharini kama Musa, na kukabidhi jahazi kwa nahodha mwingine kutufikisha salama safari yetu ya kuelekea nchi ya ahadi?.
Ukijumlisha na huu ukata wa fedha mtaani, maisha ni shida juu ya shida, taabu juu ya taabu na dhiki juu ya dhiki, kila siku ni afadhali ya jana kwa watu wa hali ya chini!, ukijumlisha na hili tishio la baa la njaa linalonukia, japo wenyewe wanakanusha ila kama kweli kuna njaa, then soon ukweli utadhihiri!.
Hali hii imenifanya nimemkumbuka mwandishi mmoja wa vitabu aliyetumia pen name ya Prince Kangwema aliandika kuhusu "Quo VadisTanzania?". Na mimi pia ninakiri kuwa Tanzania sasa hapa tulipofika, tuko kwenye situation ya "Quo Vadis Tanzania". Mungu tusaidie!.
Watu wa kulisaidia taifa letu hili wapo!, ila kama ilivyo kawaida, nabii huwa hakubaliki nyumbani! lakini humu JF, tunao manabii wetu, tukiwakubali tukawasikiliza, watatusaidia na jahazi letu litatia nanga salama u salmini kwenye nchi ya ahadi!, tusipowasikiliza, tutaendelea kutanga tanga na njia bila kufika nchi ya ahadi!.
Someni hapa kumhusu huyu jamaa.
Nimeota ndoto kuna Mbunge atakula mvua wiki ijayo
Kitu kikubwa kuhusu wewe ni you have the powers!, use them!.
Kwa msio jua, ndoto za kweli huwa zipo na zinaitwa lucid dreams.
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, Wewe Unazo?
"Will Powers!", "Faith Healing!"-NgMiujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. -Kila Mtu Anazo!
Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?
Kuna siri gani kwenye ulimwengu wa kiroho ukilala chali?
Mambo mengi ninayo yawaza au kuyaota huwa yanatokea kweli tangu Nina mika 12 na sasa Nina mika 18.

Tusiwadharau kabisa watu kama hawa waota ndoto na kuzisema, hivi ni vipawa kutoka kwa Mungu, tuwatumie, tuwasikilize, watatuepushia na mengi na kulisaidia taifa kusonga mbele kwa kuisikiliza sauti ya Mungu ikileta ujumbe kupitia ndoto!, tukidharau yatatukuta ya kutukuta, akina sisi watu wa kummbukumbu kazi yetu itakuwa ni kukumbusha tuu!.
Najua hata kwa bandiko hili bado kuna watu humu mtabeza sana kama mlivyombeza kule huyu muota ndoto, lakini ndoto yake imetimia, tutakapofika mwaka 2020 na zile ndoto za waota ndoto wengine zitakapotimia, ndipo wenye kumbukumbu watalikumbuka bandiko hili!.
Naomba msishangae kwa waota ndoto kuwa persecuted, hata Yusufu "Mzee wa Ndoto", alifungwa gerezani, kwa ajili ya ndoto tuu!, hata Shadraki, Meshaki na Abednego walifungwa gerezani kwa ajili ya ndoto!, hata wale watabiri waliposhindwa kuitafasiri ile ndoto ya Mfalme Belshaza ya "Mene Mene Takeli na Peresi " pia walifungwa gerezani!, hata Paulo na Sila nao walifungwa gerezani!, hadi milango ya gereza ikafunguka!, na mimi pia nina ndoto, iko siku milango ya gereza letu hili tuliomo ikafunguka na watu tutaziheshimu baadhi ya ndoto za kweli ikiwemo ile ndoto ya Lema!.
Paskali

Mkuu mzushi , kwanza honger sana kwa unabii huu!, pili mimi nakuamini, na tatu jikubal nabii huwa hakubaliki nyumbani ila endelea kutuletea unabii siku ukitimia utaheshimika!.Wakuu nimeota ndoto kuwa kuna Mbunge atakula mvua wiki ijayo Na bahati mbaya imejirudia zaidi ya Mara 3 na kila nikilazimisha ndoto isikate ili ning'amue ni nani usingizi unakata ,tuombeane uzima kukuche salama labda kitendawili kitateguka.