Leo nimekuletea historia ya 'AIFOLA' kutokea hapa mkoani Kigoma

Kigoma Region Tanzania

JF-Expert Member
May 25, 2021
229
593
Katika picha hii utapaona 'Aifola Beach' ambayo ipo hapa mkoani Kigoma.

Kwa muonekano utaona kwenye ufukwe wa ziwa kuna miti mirefu imejirundika karibu na ziwa Tanganyik maeneo ya Burega.

1689931901500.png

Burega, muonekano wa mbali

Miti hiyo imepandwa miaka mingi sana na imepandwa kwa mstari ulionyooka japo kwasasa haipo tena kama hapo zamani kutokana na ongezeko la kina cha ziwa kilichosababishwa na mabadiliko ya kimazingira. Iliangushwa na kung'olewa kabisa na maji.

1689932053039.png

Muoenekano wa karibu

Naanza kuandika makala hii kwa kibwagizo cha mashairi ya Wimbo wa Aifola, sio ule wa Linex! hapana.
Haya ni mashairi ya wimbo wenyewe wa Aifola tangu miaka ya 1994-1995

''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
''Kidudu chamfata nani? chamfuata mwenda salama!

Mashairi hayo yalitamba sana mkaoni Kigoma Mwaka 1995.

'Je yanamaanisha nini? nani aliyatunga? kwa kusudio lipi haswa?
...............
Nakurejesha kwenye kampeni za uchaguzi za mwaka 1995, kulikua na kijana mashuhuri kutokea Kigoma aliyeisha Marekani takriban miaka 20, kijana huyu alikuja kwa nia ya dhati kulikamata jimbo la Kigoma mjini, 1995. Huyu si mwingine ni mtaalamu 'Lukuga' maarufu kama 'Dr. Aman Walid Kabourou'

1689932387266.png

Kaburu 1995

Awali kulikua hakuna jina la 'Aifola' bali jina hili lilianza tu wakati wa ujio wa Aman Kabour wakati wa harakati zake za kisiasa miaka ya 1990's. Katika kutafuta umaarufu na idadi ya vijana akaona afadhili burudani ya vijana kwenda kuogelea Ziwa Tanganyika.

Kilichompelekea kufanya hivyo ni kama alivyoona beach zingine za huko Marekani ambako ameishi huko kwa takriban miaka 20.

Kipindi hicho kulikua hakuna burudani zaidi ya vijana kwenda kuogelea ziwani, na hapo ndipo akawakusanya watu ziwani na eneo hilo akalipa jina kama ''I Fall Beach'' ikimaanisha naanguka beach, ni kutokana na mchezo uliobuniwa hapo.

Tangu enzi hizo vijana walikuwa wakienda kuogelea waliendeleza tabia zilizokua zikifanyika 'I Fall Beach'

Ambapo kulikua na mashindano ya kuogelea hadi kwenye 'Msalala' (muinuko wa ardhi ndani ya maji). Ukifanikiwa kufika hapo kwenye 'msalala' basi wadada ambao wapo nchikavu hukupigia makofi na kukuimbia ikiwa utashindwa kufika katika msalala kutokana na kuanguka. 'I Fall'

1689932702388.png

Mwenda salama
Hiyo mwenda salama ni wakati ule mnashindana kufikia msalala, sasa mashindano hayo yawe ni yenye salama, mwendo huo wa safari kutoka nchikavu kwa kupiga mbizi uwe wenye salama kwenu na ufike eneo la msalala ukiwa salama.

Nini kilikua kinatokea katika haya mashindano?

Ni kwamba wakati wewe unajitahidi kusonga mbele kwa kuogelea, wenzako wanaruhusiwa kukuzuwia kwa kukupiga 'Mikambi' mfano wa mamba ndani ya maji' na wewe pia unaruhusiwa kuwapiga wenzako mikambi ambao mnashindana nao kwenda katika msalala.

Wakati huo sasa mnashindana na kupigana mikambi ndio likaja neno
'Kidudu chamfata nani? Likimaanisha yule anayekupiga mikambi ndio anafananishwa na kidudu au mnayama mfano wa mamba.
Sasa hiyo mikambi inamfuata nani wanamaanisha 'chamfuata mwenda salama!'' Huyoo ambaye anagombania kufika huko.

1689932805526.png

'Hili shindano lilikua kubwa sana na waimbaji walikua ni wadada, na wewe kidume uko ndani ya maji, basi juhudi zote zinaishia hapo ili upate ubingwa wa kufika katika msalala.

Kutokana na lugha na kurahisisha ladha, wakajikuta hawaimbi ''I Fall'' wakaanza kuimba 'Aifola' wakimaanisha 'I Fall'

1689932887978.png

Hivyo ikawa inaimbwa
''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
(Ikimaanisha = Naanguka, naanguka, naanguka mimi mwenda salama baada ya kupigwa mkambi)
''Kidudu chamfata nani?'
(Ikimaanisha = Mkambi kapigwa nani)
'Chamfuata mwenda salama!'
(Ikimaanisha = Mkambi kapigwa mwenda salama)

1689932943009.png

Wimbo huo ukawa maarufu, na mchezo huo ukawa mashuhuri na ukapendwa mkoa mzima wa Kigoma, hadi huko kwenye mto Mungonya watu wakawa wanacheza michezo hiyo ya Aifola.
....................
Vyanzo vingine vinadai kwamba hii ''I Fall'' sio sahihi, bali asili yake lilikua ni jina la mrembo wa Kimanyema aliyeitwa 'Aifola' huyu binti aliolewa huko jijini Dar es salaam, kisha aliachana na mumewe na hivyo Mume wake akawa anahaha kumfuatilia sana, akafika hadi Kigoma kumtafuta na kumuulizia sana. Ndipo vijana wa mtaa wakaanza kumtania mume wa Aifola kila wamuonapo walikua wakiimba

''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
''Kidudu chamfata nani? chamfuata mwenda salama!

Wakimaanisha, Aifola amekwenda salama, lakini kidudu (mume wake) anaendelea kumfuata Aifola.
Na kwakua watoto wengi walipenda kwenda kuogolea Ziwani basi wimbo huo ukawa ni wimbo pendwa na ndipo eneo hilo likaitwa 'Aifola Beach'

Na hapo ndipo msanii kutoka Kigoma Linex sunday mjeda katika wimbo wake wa Aifola akatupia haya mashairi

'Ni kama niliruka majivu na kukanyaga moto
'Matusi na kunifedhehesha ikawa malipo ya pendo langu kwako
'Mbele za watu nikapiga goti nikaweka pete ya uchumba kwenye kidole chako
'Kumbe ulikua chupa ukang'aa
'kwenye jua kali
'Nikadhani almasi nikakupenda kwa kasi

'Baby i don't wanna waste my time
'Change how you feel
'If you don't want me some will
..............
LINEX akaendelea kulalamika kwamba

'Kwa kuziamini hisia zangu
'Nikakukabidhi moyo wangu aifola
'Kwa kudhania siku moja me nawe tutafunga ndoa aifola
'Nitakutafuta hili nilipe japo theluthi ya wema wako
'Jicho lako la wema
'Kwangu limekuwa pending
'Moyoni mwangu
'Siwezi kukuvua wema na kukulipa mabaya kwa kosa moja

'Yale maumivu uliyonipa
'Nimeshayasahau

1689933468447.png

Mashairi haya ya Linex yanaambatana na nadharia ya pili, ambapo linex alikuwa kama Mume wa Aifola.
......................................
.....................................
Pia kundi dogo la wadau wengine wamekataa nadharia zote hizo mbili na kudai ya kwamba haifahamiki maana yake haswa japo tulikua tunaimba. Ispokuwa Kaburu anaweza akawa ni muanzilishi au na yeye alilikuta enzi za ukuaji wake kisha akalifufua katika kampeni zake.
 
Attachments

  • 1689931879662.png
    1689931879662.png
    146.2 KB · Views: 16
  • 1689932270822.png
    1689932270822.png
    185.1 KB · Views: 18
  • 1689932632797.png
    1689932632797.png
    162.6 KB · Views: 14
Katika picha hii utapaona 'Aifola Beach' ambayo ipo hapa mkoani Kigoma.

Kwa muonekano utaona kwenye ufukwe wa ziwa kuna miti mirefu imejirundika karibu na ziwa Tanganyik maeneo ya Burega.

View attachment 2695186
Burega, muonekano wa mbali

Miti hiyo imepandwa miaka mingi sana na imepandwa kwa mstari ulionyooka japo kwasasa haipo tena kama hapo zamani kutokana na ongezeko la kina cha ziwa kilichosababishwa na mabadiliko ya kimazingira. Iliangushwa na kung'olewa kabisa na maji.

View attachment 2695189
Muoenekano wa karibu

Naanza kuandika makala hii kwa kibwagizo cha mashairi ya Wimbo wa Aifola, sio ule wa Linex! hapana.
Haya ni mashairi ya wimbo wenyewe wa Aifola tangu miaka ya 1994-1995

''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
''Kidudu chamfata nani? chamfuata mwenda salama!

Mashairi hayo yalitamba sana mkaoni Kigoma Mwaka 1995.

'Je yanamaanisha nini? nani aliyatunga? kwa kusudio lipi haswa?
...............
Nakurejesha kwenye kampeni za uchaguzi za mwaka 1995, kulikua na kijana mashuhuri kutokea Kigoma aliyeisha Marekani takriban miaka 20, kijana huyu alikuja kwa nia ya dhati kulikamata jimbo la Kigoma mjini, 1995. Huyu si mwingine ni mtaalamu 'Lukuga' maarufu kama 'Dr. Aman Walid Kabourou'

View attachment 2695195
Kaburu 1995

Awali kulikua hakuna jina la 'Aifola' bali jina hili lilianza tu wakati wa ujio wa Aman Kabour wakati wa harakati zake za kisiasa miaka ya 1990's. Katika kutafuta umaarufu na idadi ya vijana akaona afadhili burudani ya vijana kwenda kuogelea Ziwa Tanganyika.

Kilichompelekea kufanya hivyo ni kama alivyoona beach zingine za huko Marekani ambako ameishi huko kwa takriban miaka 20.

Kipindi hicho kulikua hakuna burudani zaidi ya vijana kwenda kuogelea ziwani, na hapo ndipo akawakusanya watu ziwani na eneo hilo akalipa jina kama ''I Fall Beach'' ikimaanisha naanguka beach, ni kutokana na mchezo uliobuniwa hapo.

Tangu enzi hizo vijana walikuwa wakienda kuogelea waliendeleza tabia zilizokua zikifanyika 'I Fall Beach'

Ambapo kulikua na mashindano ya kuogelea hadi kwenye 'Msalala' (muinuko wa ardhi ndani ya maji). Ukifanikiwa kufika hapo kwenye 'msalala' basi wadada ambao wapo nchikavu hukupigia makofi na kukuimbia ikiwa utashindwa kufika katika msalala kutokana na kuanguka. 'I Fall'

View attachment 2695204

Mwenda salama
Hiyo mwenda salama ni wakati ule mnashindana kufikia msalala, sasa mashindano hayo yawe ni yenye salama, mwendo huo wa safari kutoka nchikavu kwa kupiga mbizi uwe wenye salama kwenu na ufike eneo la msalala ukiwa salama.

Nini kilikua kinatokea katika haya mashindano?

Ni kwamba wakati wewe unajitahidi kusonga mbele kwa kuogelea, wenzako wanaruhusiwa kukuzuwia kwa kukupiga 'Mikambi' mfano wa mamba ndani ya maji' na wewe pia unaruhusiwa kuwapiga wenzako mikambi ambao mnashindana nao kwenda katika msalala.

Wakati huo sasa mnashindana na kupigana mikambi ndio likaja neno
'Kidudu chamfata nani? Likimaanisha yule anayekupiga mikambi ndio anafananishwa na kidudu au mnayama mfano wa mamba.
Sasa hiyo mikambi inamfuata nani wanamaanisha 'chamfuata mwenda salama!'' Huyoo ambaye anagombania kufika huko.

View attachment 2695206

'Hili shindano lilikua kubwa sana na waimbaji walikua ni wadada, na wewe kidume uko ndani ya maji, basi juhudi zote zinaishia hapo ili upate ubingwa wa kufika katika msalala.

Kutokana na lugha na kurahisisha ladha, wakajikuta hawaimbi ''I Fall'' wakaanza kuimba 'Aifola' wakimaanisha 'I Fall'

View attachment 2695207

Hivyo ikawa inaimbwa
''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
(Ikimaanisha = Naanguka, naanguka, naanguka mimi mwenda salama baada ya kupigwa mkambi)
''Kidudu chamfata nani?'
(Ikimaanisha = Mkambi kapigwa nani)
'Chamfuata mwenda salama!'
(Ikimaanisha = Mkambi kapigwa mwenda salama)

View attachment 2695208

Wimbo huo ukawa maarufu, na mchezo huo ukawa mashuhuri na ukapendwa mkoa mzima wa Kigoma, hadi huko kwenye mto Mungonya watu wakawa wanacheza michezo hiyo ya Aifola.
....................
Vyanzo vingine vinadai kwamba hii ''I Fall'' sio sahihi, bali asili yake lilikua ni jina la mrembo wa Kimanyema aliyeitwa 'Aifola' huyu binti aliolewa huko jijini Dar es salaam, kisha aliachana na mumewe na hivyo Mume wake akawa anahaha kumfuatilia sana, akafika hadi Kigoma kumtafuta na kumuulizia sana. Ndipo vijana wa mtaa wakaanza kumtania mume wa Aifola kila wamuonapo walikua wakiimba

''Aifola Aifolaaa, Aifola mwenda salama
''Kidudu chamfata nani? chamfuata mwenda salama!

Wakimaanisha, Aifola amekwenda salama, lakini kidudu (mume wake) anaendelea kumfuata Aifola.
Na kwakua watoto wengi walipenda kwenda kuogolea Ziwani basi wimbo huo ukawa ni wimbo pendwa na ndipo eneo hilo likaitwa 'Aifola Beach'

Na hapo ndipo msanii kutoka Kigoma Linex sunday mjeda katika wimbo wake wa Aifola akatupia haya mashairi

'Ni kama niliruka majivu na kukanyaga moto
'Matusi na kunifedhehesha ikawa malipo ya pendo langu kwako
'Mbele za watu nikapiga goti nikaweka pete ya uchumba kwenye kidole chako
'Kumbe ulikua chupa ukang'aa
'kwenye jua kali
'Nikadhani almasi nikakupenda kwa kasi

'Baby i don't wanna waste my time
'Change how you feel
'If you don't want me some will
..............
LINEX akaendelea kulalamika kwamba

'Kwa kuziamini hisia zangu
'Nikakukabidhi moyo wangu aifola
'Kwa kudhania siku moja me nawe tutafunga ndoa aifola
'Nitakutafuta hili nilipe japo theluthi ya wema wako
'Jicho lako la wema
'Kwangu limekuwa pending
'Moyoni mwangu
'Siwezi kukuvua wema na kukulipa mabaya kwa kosa moja
'Siwezi kukuvua wema na kukulipa mabaya kwa kosa moja
'Yale maumivu uliyonipa
'Nimeshayasahau

View attachment 2695213
Mashairi haya ya Linex yanaambatana na nadharia ya pili, ambapo linex alikuwa kama Mume wa Aifola.
......................................
.....................................
Pia kundi dogo la wadau wengine wamekataa nadharia zote hizo mbili na kudai ya kwamba haifahamiki maana yake haswa japo tulikua tunaimba. Ispokuwa Kaburu anaweza akawa ni muanzilishi au na yeye alilikuta enzi za ukuaji wake kisha akalifufua katika kampeni zake.
Kumbe hata jina lake nilidanganywaaaa
 
Kigoma Region Tanzania nasikitika wana KG mmepoteza identity. Yaani kutoka kuwa wapambanaji hadi kuwa machawa.

Mmekuwa wanafiki na vigeugeu sana. Yaani watu kama DK Kabur hamna tena. Zitto ndio huyu, chawa wa mama.

Mmnatuangusha sana, tumaini la Watanzania limebakia kwa wana Mbeya tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom