Leo ndio mwisho wa matumizi ya 3D, msako kuanza kesho

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Leo alhamisi ndiyo mwisho wa matumizi ya namba za magari zenye uwezo wa 3D na kuanzia kesho ijumaa Jeshi la polisi Tanzania limetangaza kuanza msako mkali kwa wote ambao wameshindwa kuzitoa namba hizo za 3D kwenye magari yao.

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani awali kilitoa muda wa siku kumi na nne kwa wote wenye namba za 3D kuziondoa wenyewe kabla ya Polisi kuingia kwenye utekelezaji wa sheria kutokana na kutoruhusiwa kuwa na namba hizo kwenye magari.

Polisi inasema kuanzia kesho pia wataanza msako wa magari yenye taa za vimulimuli zilizowekwa katika baadhi ya vyombo vya moto visivyoruhusiwa.
 
Back
Top Bottom