Kwa kauli ya CDF kwa rais mikoa ya mipakani wajiandae kwa msako wa wahamiaji haramu

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,129
8,651
Kulingana na maombi ya CDF kwa Rais Samia Suluhu Hassan huwenda kukawa na msako wa wakimbizi na wahamiaji haramu kanda ya Magharibi na mkoa wa Kigoma ukiwemo.

Hapa chini nimekuwekea Mambo muhimu ya kuzingatia pindi msako ukikukuta.

Mazingira ya msako

-Kikawaida msako huwa na maafisa wengi tofauti ikiwemo uhamiaji, polisi na jeshi la wananchi JWTZ na wala sio lazima siku ya msako itangazwe.

-Maeneo yanayo athirika zaidi na msako huwa ni vijijini hususan mwambao wa ziwa Tanganyika na vijiji vya nyanda za juu kaskazini (Kasulu na Kibondo).

-Msako unaweza kuchukua hata mwezi mzima na zaidi, hivyo huwa ni zoezi la muda kidogo.

Mambo MUHIMU ya kuzingatia

Bila kujali hali yako ya uraia, iwe ni mtanzania, muhamiaji halali, muhamiaji haramu au mkimbizi tambua kwamba una haki zilizohakikishwa chini ya Katiba.

Jambo la kwanza unatakiwa kutulia usipaniki (sikiliza zaidi kuliko kuongea), Usikimbie, usijifiche, epuka kubishana, kupinga, au kumzuia afisa, hata kama unaamini kuwa haki zako zinakiukwa. Usidanganye kuhusu hali yako au kutoa hati za uwongo.

Msako wa Mwaka 1997-1998 Baadhi ya wadau walikimbia na wengine kujificha lakini matokeo yake walikamatwa na hawakupata nafasi ya kuhojiwa mwisho wa siku walisota hadi kuja kuachiwa wamepoteza siku nyingi.

Unatakiwa kukaa kwa kutulia kwasababu hawatakua na pakukupeleka kama wewe ni Mtanzania.

Jambo moja muhimu sana ukiulizwa kama una ndugu Congo au Burundi: Usidanganye eleza ukweli, wala kuwa na ndugu katika nchi hizo bado sio kigezo cha wewe kutokua raia.

Epuka kuchongea wenzako hata kama mna magomvi au mmepishana katika mambo usimchongei mwenzako. Mwaka 1997 Waha walikua wakiwachongea Wamanyema, mwaka 1998 Wamanyema wakawa wanawachongea Waha kwa maafisa.

Yaani kulikua na msako wa wakongo na msako wa warundi. Tabia hii sio nzuri na inadhoofisha umoja wetu kama wana Kigoma.

Lafudhi ya Lugha:

Huku kwetu Kigoma ni kawaida sana kiswahili cha mwambao wa ziwa kushabihiana na lafudhi za Kongo ikijumuishwa maneno kama 'Shashee, kumkichwa, kunyamba, kutomboka, bayamaa, njoo vile, bafu, n.k Maafisa wanalitambua hilo vyema hivyo usipate hofu, kwani kuna wanakigoma wanafanya biashara Congo na wanaweza kabisa kuzungumza kiswahili cha Congo.

Usiingilie mazungumzo ya mtu mwingine ambaye anahojiwa, yaani usiwe kimbelembele kujibu maswali ya watu. Epuka kuingilia usaili wa mtu.

Umakini wa zoezi hutegemea wingi wa maafisa, wakaguzi wanapokua wengi zoezi huwa linakwenda vyema zaidi, lakini wanapokua wachache zoezi huwa linakua na matumizi ya nguvu na haraka bila ya kutoa nafasi ya kujieleza kwa umakini.

Hapo sasa ndio watu hupewa mitihani midogo midogo ya haraka haraka kama kuhesabu namba 1-4, kutaja viongozi fulani wa taifa, rangi ya bendera na tunu mbalimbali za taifa ikiwemo wimbo wa taifa na mambo mengine madogo madogo ikiwemo ukaguzi wa ndui n.k.

Zoezi hilo linaweza kuwakamata hata watanzania halisi kwani si kila mtanzania anaweza kufahamu vyema tunu za taifa, na wala sio kila mtanzania anaweza akawa na ndui begani. Hivyo usipaniki Ofisa wanalitambua hilo vyema.

Nyaraka muhimu kua nazo

-Kadi ya Kliniki kama unayo
-Cheti cha kuzaliwa kama unacho
-Cheti za darasa la 7 kama unacho
-Cheti cha kidato cha 4 kama unacho
-Cheti cha ndoa kama umeolewa Tanzania au umeoa mgeni
-Kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
-Hati ya kusafiria n.k

Nyaraka hizo sio kila mtanzania anaweza akawa nazo, hivyo usipaniki maafisa wanalifahamu vyema jambo hilo. Muhimu mahojiano yako yaende vizuri bila kuwadanganya au kuwaudhi.

Kipande Maalum kwa WAHA

-Ukiulizwa kabila lako sema mimi ni Muha na wala usichambue vitu ambavyo huvifahamu, epuka sana kudanganya.

-Ukiulizwa mgawanyiko wa himaya za Waha, zipo himaya 6 kuna Waha wa Buyunga, Muhambwe, Heru, Luguru (Kunkanda), Bushingo, na Bujiji (Nkalinzi).

-Ukiulizwa koo za Waha, hakikisha unataja Koo yako, kwasababu kabila hili ni kubwa na lina Koo nyingi.

-Ukiambiwa ongea Kiha kama hujui usiongei, maafisa wanafahamu vyema kwamba Waha wasiofahamu Kiha ni wale waliozaliwa na kulelewa Mjini. Hivyo usipaniki.

-Utaeleza ulipozaliwa, uliposoma, taarifa za baba yako na mama yako ni muhimu uzifahamu.

-Ukiulizwa jambo usilolijua usipaniki, maafisa wanafahamu vyema kunako kile wanachokuhoji.

Kipande Maalumu kwa WAMANYEMA

-Ukiulizwa kabila lako usiseme Mmanyema bali taja kabila lako la asili kama ni Mgoma, au Mbwari, au Muhorohoro, au Mnyakaramba au Mluba au Mbangubangu n.k

-Manyema ni mjumuiko wa hayo makabila, hilo linafahamika vyema kwa maafisa. Kwa hivyo ukijitambulisha kama Mmanyema hawatakufahamu ni Mmanyema yupi, unatakiwa kutaja kabila lako la asili.

-Ukiambiwa ongea lugha ya kabila lako, sema lugha yangu ni Kiswahili kutokana na kabila langu lipo ndani ya mjumuiko wa Kimanyema, maafisa wanafahamu vyema jambo hilo, kwasababu wanaozungumza lugha za Kimanyema ni wachache sana.

Kipande Maalum kwa WABEMBE

-Sasa hapa ndio huwa kuna kashikashi kidogo, Wabembe ambao ni raia watanzania wanaongea kibembe sawa sawa na wabembe waliopo makambini. Hivyo hapa huwa kunahitajia maelezo ya kina, na vielelezo vya kutosha.

-Ni ngumu kidogo kumtofautisha Mbembe Mtanzania na Mbembe wa Kambini, japokua wabembe wengi watanzania kiswahili chao kiko vyema tofauti na wale wa Kambini, hivyo usipaniki, maafisa wanalifahamu vyema jambo hilo. Muhimu taarifa zako ziwe za ukweli. Kwani kuna wabembe watanzania na kuna wabembe wa Kongo.

CR:kigoma region
 
Shukran mkuu, bila shaka wahusika watazingatia ushauri wako ili kuepuka matatizo huko mbele.
 
Bad enough, huwa wakimbizi/wahamiaji haramu unakuta wanakamatiwa Morogoro... Mipakani husikii hata kidogo
 
Hii nchi ni ya ajabu sana sijawahi kuona, raia wa kigeni wana ingia tu utadhani wanaingia chumbani kwao kulala. Iko hivi ni rahisi sana raia wa kigeni kuingia kienyeji tu na akaishi vizuri bila shida yoyote ile tena akipambana anapata nyaraka muhimu Sana. Wewe mtanganyika jaribu kwenda hapo Rwanda tu kienyeji uone utakavyo rudishwa kama kenge. Li nchi limejaa watu wasio kuwa na uchu na nchi yao kila mahala.
 
May be sera ya ujamaa ndo imeleta yote
 
CDF hana shida na hao, yeye anawataka wale walioajiriwa serikalini na wenye nyadhifa kubwa kubwa
Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha tusipodhibiti mwanzoni ndo hko mbeleni tunaweza pata hata PM mnyarwanda
 
wakimbizi 10,000 wameajiriwa wengine kwenye nafasi nyeti za maamuzi serikalini.
waanzie huko Kwanza kwa mawaziri,makatibu wa wizara,bandarini,tiss na majeshi mengine.wapo wengi wanajulikana na tunawajua.
 
Back
Top Bottom