Leo nafunga pingu za maisha

Karibu sana mkuu katika maisha ya ndoa.Nawatakieni kila la heri
 
Mungu awaangazie nuru ya uso wake na kuwalinda, Mungu awabariki kila mingiapo na mtokapoa,na Mungu awainulie msaada tka patakatifu pake siku zote za maisha yenu. Awape watoto wa viuno yenu watakao ipamba nyumba yenu kwa siha njema, nidhamu na amani.

Hongreni sana wanandaoa wageni.
 
Hongera sana na kila la kheri. Kumbuka sala/maombi ndio msingi wa ndoa yenu.

Soma Zaburi 1:3 na 128
 
Asanteni wadau Mungu awabariki kwa kuunitakia kheri usenior bachelor mtamu lakini... So misele lazima niache
 
hongera sana ..ila na ww ulianza uzinifu wakati bado mdogo bwana ...mungu hapendi mambo hayo...hongera lakini kwa kuingia kwenye chama cha kujitakia BP na Heart attacks na brain concusions za bure.....

Kongosho mhhh hayo mambo hayapo bana. Sijui heart attack sijui BP hakuna bana
Maisha ni mazuri sana utakapompata yule mhusika wa kweli kwenye ndoa yako
Pukudu hongera sana mkuu na karibu sana kwenye chama chetu hiki
Naamini umepata uzoefu wa kutosha kupitia kwa wakongwe hapa akina AshaDii, Mtambuzi, Babu Asprin, na wengineo kuhusu ndoa
Mungu akutangulie katika maisha yako ya ndoa mkuu
 
hongera sana ..ila na ww
ulianza uzinifu wakati bado mdogo bwana ...mungu hapendi mambo
hayo...hongera lakini kwa kuingia kwenye chama cha kujitakia BP na Heart
attacks na brain concusions za bure.....

Mbona unamtisha? Akighairi je? Hongereni mwaya wanandoa wapya.
 
Habari za jumapili wana JF leo tarehe 17 June 2012 nafunga ndoa na mpenzi wangu ambaye tumekuwa na mahusiano since 2007 tukiwa chuoni. Ndoa itafungwa katika kanisa la SDA Njiro wote mnakaribishwa. Namshukuru Mungu kuifikia siku hii
Hongera Sana na jitahidini kukabili ups and downs ndani ya ndowa mkiwa pamoja.
 
Pukudu hongera sana. Mwisho wa safari moja ni mwanzo wa safari nyingine.

Afu badilisha Avatar yako basi ikae Kisabato zaidi, hii unayovuta haifai:
avatar34667_5.gif
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana mkuu. Mungu awajalie maisha marefu yenye upendo, amani na furaha siku zote za maisha yenu.
 
Nakupongeza na kukuombea ndoa yenye amani. Ila uwe unaingia huo mkataba kwa hiari. Maana kuna mengi yasiyokupendeza kuhusu mwenza wako utayajua baada ya ndoa. Vumilia. Wenzio tuliotangulia wakati mwingine tunatamani tusingeoa kabisa. Kila la kheri.
 
Habari za jumapili wana JF leo tarehe 17 June 2012 nafunga ndoa na mpenzi wangu ambaye tumekuwa na mahusiano since 2007 tukiwa chuoni. Ndoa itafungwa katika kanisa la SDA Njiro wote mnakaribishwa. Namshukuru Mungu kuifikia siku hii

Hongera sana asee umenikumbusha miaka minne iliyopita,
Sasa ukumbi wapi kama vipi utanikuta pale mi napangapanga viti?
 
whaaaaat? unafunga PINGU? hii term itabidi ibadilishwe maana it's kinda scary aisee...
 
All the best mkuu,Mola awajalie ndoa ya amani na upendo,mzae watoto wajaze dunia.
 
Back
Top Bottom