Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
LEO BUNGENI DODOMA - Bajeti ya Wizara ya Kilimo
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameelezea umuhimu wa uanzishwaji wa Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema la Jimboni mwao.
Mbunge huyo ameeleza mengi, yakiwemo yafuatayo:
(i) Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufufua Mradi huo uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 bila kutekelezwa
(ii) Mazao makuu yatayolimwa kwa umwagiliaji ni: mpunga, mahindi, alizeti, choroko, kunde, mbaazi, maharage na pamba
(iii) Ziwa Victoria lina umri wa takribani miaka 400,000 na umri wa Mto Nile ni takribani miaka milioni 30. Kwa hiyo, kilimo cha umwagiliaji kiendelee kwani Mto Nile ni mkongwe umekuwepo kabla ya kuwepo kwa Ziwa Victoria
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa:
Tafadhali sikiliza mchango wa leo Bungeni wa Prof Sospeter Muhongo
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 22 May 2025