kwa kuongezea tu...
Huyo dada hakuwa mstaarabu kutoka mwanzo, ni tabia yake aliyokuwa nayo na inaonesha amepata mafanikio sana na ndo maana amethubutu kumpiga kibao mtoa mada, kamwe hawezi kujifunza kwa somo hilo moja ,
Ningekeuwa mimi baada ya utambulisho ningemwambia kwa kuwa nilikuwa njema nikaambulia kipigo, simu yake sina shida nayo ,ila nakwenda kutupa chooni, akanunue nyingine, ili ujinga wake umgharimu
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo;
mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari
kake akadondosha simu;
mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,ak
anisonya tena msonyo wa dharau sana na
nikajuta kumgusa bega ka sababu ya kibao
alichonipiga.
Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu
nakuondoka zangu;
wala sikuizima.
Nafika town simu hiyo ikaita
nikapokea kwa shauku ya kujua nani....
haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji..
mimi;Hallo habari yako...
yeye;Nzuri;
mimi;nani wewe ...
yeye;Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
mimi;Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao
pale stand ya ubungo leo na ukanisonya ....
yeye;Basi kaka nisamehe naomba unambie
ulipo nije tuelewane ....
Mimi;Nitakwambia baadaye ..
(nikakata simu na kuzima)
Swali nimwambie napatikana wapi au
nimpotezee ili liwe fundisho kwake?
msamehe bure na mrudishie bila sharti lolote. Kama ni mwelewa atajuta kwa alilokufanyia na inaweza ikampa somo la maana sana maishani mwake.
msamehe bure na mrudishie bila sharti lolote. Kama ni mwelewa atajuta kwa alilokufanyia na inaweza ikampa somo la maana sana maishani mwake.
Hii constructed mail ipo siku nyingi.... Ungesema tu nimeicopy mahali na sio wewe imekutokea.
Ya siku nyingi sana hii
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo;.... Today 06:58
Mrudishie na akifika, kuwa Mstaarabu na MKRISTO wa kikweli - Geuza shavu la pili akunase kibao.