Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo;
mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari
kake akadondosha simu;
mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,ak
anisonya tena msonyo wa dharau sana na
nikajuta kumgusa bega ka sababu ya kibao
alichonipiga.
Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu
nakuondoka zangu;
wala sikuizima.
Nafika town simu hiyo ikaita
nikapokea kwa shauku ya kujua nani....
haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji..
mimi;Hallo habari yako...
yeye;Nzuri;
mimi;nani wewe ...
yeye;Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
mimi;Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao
pale stand ya ubungo leo na ukanisonya ....
yeye;Basi kaka nisamehe naomba unambie
ulipo nije tuelewane ....
Mimi;Nitakwambia baadaye ..
(nikakata simu na kuzima)
Swali nimwambie napatikana wapi au
nimpotezee ili liwe fundisho kwake?