Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal....

Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal....

Mkuu nitapingana na hoja yako, uchomaanisha ndio kile tunaita" steriotypes" yaani kwa kuwa huyo dada aliwahi kuguswa na akatongozwa basi kila anaye mgusa anadhani ana nia ya kumtongoza! Hii si sahihi na usije kuwa mhanga wa hilo,
Halafu nikwambie kitu.. , kuna wadada by default ni wakorofi tu, mfano jana nilisafiri siti moja na dada mmoja kibri sana ,mimi nilikaa dirishani yeye kwenye aisle ,sikuwa na maongezi naye zaidi ya salamu wakati anaingia niliyomsalimia na hakujibu, sasa wakati natoka kuelekea maliwatoni nikamgusa kwa bahati mbaya , reaction yake alinipush kwa nguvu kama vile tuna ugomvi fulani, mind you ,hanijui simjui tumekutana safarini tu, kimbembe baada ya kutua yeye ana conect kuelekea durban hafu hajui utaratibu. mimi ndo nimeshafika destination yangu, nikamkuta nje ameduwaa, akanifuata kiaibu aibu na kuniuliza "eti anko domestic check in counters zipo wapi mi naelekea durban", kwa jinsi alivo behave kutoka dar, sikumjibu chochote .
Mkuu baadhi ya dada zetu huwa wana matatizo sana. Sijui huwa hata wanawaza nini. Kuna story moja niliisikia redioni, dada mmoja alipanda daladala, na kuna kaka mmoja nae alipanda. Yule dada alikaa upande wa dirishani.Huyu kaka alikuwa katikati(Ni kule mbele kwa dereva).Sasa huyu dada wakati anasalimiwa na huyu kaka aliitikia kwa nyodo sana,dharau na maringo sana, na hakutaka story zaidi, alimuona jamaa kama mavi. Huyu dada alitoa simu (Kumbuka yuko dirishani). Kumbe kuna jamaa alikuwa ameishaipigia mahesabu ya milo kama miwili.Wakati daladala imeanza kuondoka, jamaa (kibaka) alipita na simu kama mwewe, akaanza kulia kaka nisaidie. Kuna watu wanaudhi sana.
 
Back
Top Bottom