Nilichogundua Roho ya umaskini,inaandama watu wengi sana huku nchi za Afrika.
Kuna mama mmoja ni mama wa makamo ana watoto 5 wote wamefanikiwa na wanamaisha yao,walibahatika kusomeshwa.
Wako vizuri kielimu na maisha wanajitegemea.
Wamezaa watoto, huyu Mama sasa anaitwa Bibi,Mumewe yupo taasisi ya Dini.
Huyu Mama loo ni kama aina ya huyu Dada,ana mdomo always she think is right.
Sasa pale kwa Mama dadaz hawakaagi hata mwezi au miezi lazima waondoke,
Wana jumba kubwa(Ghorofa 1)lkn usafi na kudeki lazima utumie matambala na sio mop..zipo lkn zimefungiwa store.
Chakula ni chai na mkate...
(Akiwa hayupo yeye)hakipikwi kitu ila hivyo chai mkate.
Garden kuna miwa,miembe, michungwa ,mipera etc
House boy usionekani umeokota embe lililodondoka au uvunje muwa ule,
Utasakamwa utasemwa na ikiwezekana utalipa(anakukata mshahara)
Ana uza mapapai nazi n.k
Anae mkabidhi kuuza mapapai ni lazima hela kamili ifikishwe kwake,usimwambie Papai lilioza utalipa au lah umuonyeshe (kama hukulitupa)
Kuvaa kwake mwenyewe ni nguo nguo tu ili mradi kavaa,
Looh yapo mengi yakusema lkn siwezi kuandika sana mi siwezagi aisee...
Ni watu waliofanikiwa na mumuwe ila wanaishi kimaskini sana(hasa Mama)
Ndicho nachoona kwa huyu Dada,kumpa Kijinguo tu binti ,mashart kedekede mpk umemuundia kamati ya ushauri Jamii forum kutaka mawazo yako yasipingwe.
Kama ana nguo chache mpe mshahara wake mshauri akanunue nguo nzuri za kutokea.
Umempa malonya lonya ya kushindia mpk yanamshinda kuvaa ispokuwa ile moja angalau inakalika mwilini,muache avae anayotaka, yale malonya kashindwa kuvaa,Jeee baghoshaa hiiiiiii nisemejeeeee[emoji3][emoji3][emoji3]
Na hapo unasema nimempa nguo za kushindia swali ni ngapi?
Isije ikawa vinguo viwili tu na vyote vibuga vimempwaya sana ,navyo hivyo unahesabu.
Kitu kingine, kutoa kitu unachokipenda hayo ndo madhara yake,
Utakifatilia mpaka mwisho wake(hiyo sasa ndo pure roho ya kimaskini)
Maskini akitoa sadaka akimsadia mtu,majirani au mtaa mzima watajua Flani kamsaidia kitu fulani.. atatangaza tu
Ndo huyu dada sasa.....ni shida.
Nasema uongo ndugu zangu?