Leo asubuhi kulitokea mabishano home

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,391
3,402
Habari waungwana.

Habari ipo hivi. Nyumbani tuna House gal ambaye Kama kawaida husaidia kazi za Nyumbani pamoja na kulea watoto .Sasa wkt anakuja nikagundua Hana nguo za kutokea kwa maana mfano kutokea tukienda mahali au akiumwa au akienda tembelea ndugu ZAKE weekend.

Nilichofanya nikampa nguo yangu moja NZURI ambayo hata Mimi ni zile za kanisani au kwenda sehemu special na pia nikamuongezea na za kushindia kwa maana za Nyumbani Kama anafanyafanya shughuli ndogo ndogo ,lakini wkt Nampa nilimfafanulia na Tena siku iyo nakumbuka alifurahi Sana na ni siku alikuwa anaenda kusalimia ndugu zake ilibidi avue Ile aliyokuwa ameivaa na kuvaa ile niliyompa akisema anashukuru Sana na ameipenda Sana .

Na alipovaa ni Kama alipimwa ilimpendeza Sana. Baada ya Kama wiki nikagundua Ile nguo ameigeuza ya kushindia na NDO anafanyia usafi.Nikamwita nikamwelekeza kwa Nini asivae zile zingine kwa maana Ile uwe Kama nilivyomuelezea.Akaelewa akaivua na kuifua.

Sasa Leo asubuhi naamka nikamkuta ameivaa anaifagilia nje na hata Jana yake aliivaa anamenyea nduzi(nikiongelea hivyo nduzi Zina utonvu na ni nyeupe) Nikamuuliza mbona umerudia kuifubaisha nguo NZURI na nilikuelezea? Nikamwambia vua ntampa hata ndugu yangu atakayeithamini.

Sasa Baba watoto akasema Kwanza Iyo nguo kumpangia masharti aivae vipi umekosea kwa kuwa wakati unampa hakukuomba ulimpa mwenyewe na kanuni ya kumpa mtu kitu chochote ukishampa umempa matumizi ni juu yake hata angeamua kudekia kufanyaje ni yeye maana imekuwa yake.

Kweli Kama mama nimeshangaa Sana kwa hizo kauli. Je Mimi makosa yangu ni yapi au ni kweli mtoto ndani ya nyumba hupaswi kumshauri(Huyo msichana Ana miaka 18 kwenda 19) Na ikumbukwe ni mista huyo huyo aliyenilalamikia kwamba huyo msichana tangia aje anavaa vinguo vyepesi na khanga tu akijua na yeye yupo kwa maana Kama Ana majaribu na akimfananisha na dada mwingine ambaye aliondoka ambavyo hakuwa na majaribu Kama ya huyu wa Sasa kwa maana kujipitisha Mara kajilaza ovyo Yaani Mambo Kama hayo.

(Kwa hayo malalamiko yake nikaongea na Dada nikamshauri jinsi ya kuvaa na hasa azingatie nguo za heshima.Walau akabadirika.
Sasa Leo NDO hayo.

Naombeni maoni na mista atawasoma Mana kajaa tele humu
 
Hiyo nguo nzuri iliyokuwa ya kwako ndo nguo pekee uliyokuwa ukiivaa inakutoa fresh na kumfanya mwamba aridhike na chaguo lake.

Sasa kaivaa binti wa miaka 18, imemkaa kama kazaliwa nayo umesema! Mwamba keshamsifia/kumkodolea macho binti kwenye vazi hilo mara moja, binti kajua hilo.

Acha sasa yeye atumie hiyo bakora kutimiza yaliyokushinda.
 
Habari waungwana.
Habari ipo hivi..Nyumbani tuna House gal ambaye Kama kawaida husaidia kazi za Nyumbani pamoja na kulea watoto .Sasa wkt anakuja nikagundua Hana nguo za kutokea kwa maana mfano kutokea tukienda mahali au akiumwa au akienda tembelea ndugu ZAKE weekend.
Nilichofanya nikampa nguo yangu moja NZURI ambayo hata Mimi ni zile za kanisani au kwenda sehemu special na pia nikamuongezea na za kushindia kwa maana za Nyumbani Kama anafanyafanya shughuli ndogo ndogo ,lakini wkt Nampa nilimfafanulia na Tena siku iyo nakumbuka
Sasa mr sii ndio kichwa cha familia...fuata maelekezo yake acha ujuaji.
 
Habari waungwana.
Habari ipo hivi..Nyumbani tuna House gal ambaye Kama kawaida husaidia kazi za Nyumbani pamoja na kulea watoto .Sasa wkt anakuja nikagundua Hana nguo za kutokea kwa maana mfano kutokea tukienda mahali au akiumwa au akienda tembelea ndugu ZAKE weekend.
ri jinsi ya kuvaa na hasa azingatie nguo za heshima.Walau akabadirika.
Sasa Leo NDO hayo.
Naombeni maoni na mista atawasoma Mana kajaa tele humu
Endeleeni kubishania dada wa kazi

Mkimaliza njooni tujadili bei ya mafuta
 
Habari waungwana.
Habari ipo hivi..Nyumbani tuna House gal ambaye Kama kawaida husaidia kazi za Nyumbani pamoja na kulea watoto .Sasa wkt anakuja nikagundua Hana nguo za kutokea kwa maana mfano kutokea tukienda mahali au akiumwa au akienda tembelea ndugu ZAKE weekend.
Nilichofanya nikampa nguo yangu moja NZURI ambayo hata Mimi ni zile za kanisani au kwenda sehemu special na pia nikamuongezea na za
Pole mama wa nyumba. Fasta Chukua nguo yako uendelee kuitunza ili uondoe mzizi wa fitina - Kwisha. 😳
 
Nadhani hapo ni Wivu tu (ugonjwa wetu Ke tulio wengi) ndo unakufanya uwe maswali kibao kuhusu hiyo kauli ya Baba mwenye nyumba.

Nionavyo Mr wako yuko sahihi sababu we ushampa nguo huyo msichana usimpangie matumizi. Pia ako ni katabia ka wadada wengi ukimpa nguo yako nzuri usitegemee aiweke yupo radhi aweke hayo maronya ronya yake ila hiyo yako ashindie.

Kikubwa mwambie ajue kilichomleta, usiyoyataka hapo ndani kwako na aina ya mavazi unayotaka yavaliwe baas na mshahara si unampa ataenda nunua kwa hela yake.
 
Mfano wewe mtu anakupa nguo kama zawadi siku amekukuta nyumbani umeshindia anakwambia hio nguo sio ya kushindia

Kila ukivaa hio nguo ukikutana naye mara akwambie hii nguo sio ya kupitia hii njia ina vumbi sana utaifubaza nguo nzuri sana niliyokupa

Utajisikiaje

Ukipata jibu basi utaelewa wewe ni mtu wa aina gani
 
Dada yangu wacha gubu. Hiyo nguo si umeshamgaia huyo msaidizi wenu wa kazi za ndani?? Ya nini sasa kuanza kumpangia namna ya kuvaa?? Angeichukua na kuifanya dekio hiyo ingekuwa ni issue nyengine maana ingekuwa ni dharau. Lakini kwa vile anaivaa basi haina haja ya kuanza kumpangia
 
Back
Top Bottom