Lengo la sisi kuwa hapa duniani ni nini?

Lengo la sisi kuwa hapa duniani ni nini?

Kasome vzuri post yangu....nimezungumzia maisha ya:-
Mimba
Dunia
Kaburini
Akherah

Ndomana tunasema maisha safari...na hzo hatua apo juu ni vtuo vya safari.

Hcho unachozungumzia (process) kipo ndani ya hyo safari....mzee umeelewa apo?
Hapo ndipo tunapotofautiana.sifahamu itikadi yako.ila nakusihi kasome Kisa cha Miiraj.utapata faida.maisha ya mwanaadam sio safari..neno safari ni lazima kuwepo na vitu 2,Msafiri na nyenzo ya kusafiria.pili msafiri ndio muamuzi wa safari...bi maana kua anajua mwanzo wa safari yake na mwisho wa safari yake...
Ndio sbb nakukatalia ..mwanaadamu hajui mwanzo wake na hata khatma yake haijui..unathubutuje kumuita huyu ni msafiri.
 
Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137

Fanya kazi ili ukifa upate makazi mema
 
Kasome vzuri post yangu....nimezungumzia maisha ya:-
Mimba
Dunia
Kaburini
Akherah

Ndomana tunasema maisha safari...na hzo hatua apo juu ni vtuo vya safari.

Hcho unachozungumzia (process) kipo ndani ya hyo safari....mzee umeelewa apo?

Neno safari mnalitumia kimakosa na nimakosa makubwa kusema mimi ni msafiri na hapa duniani ninapita,,,Kwa sabubu ya maneno ya Muumba wetu ambayo tumekua tukiyasoma na kuyanukuu kila tunapozikana."Kutokana na udongo Tumekuumbeni.na humo Tutakurudisheni,kisha tutakuihisheni kama awali ili kila mmoja apate hesabu yake",
Kimsingi asili ya Mwanaadam ni udongo.
Huoni aibu unapotamka kwa macho makavu kuwa udongo unasafiri?,
 
Hapo ndipo tunapotofautiana.sifahamu itikadi yako.ila nakusihi kasome Kisa cha Miiraj.utapata faida.maisha ya mwanaadam sio safari..neno safari ni lazima kuwepo na vitu 2,Msafiri na nyenzo ya kusafiria.pili msafiri ndio muamuzi wa safari...bi maana kua anajua mwanzo wa safari yake na mwisho wa safari yake...
Ndio sbb nakukatalia ..mwanaadamu hajui mwanzo wake na hata khatma yake haijui..unathubutuje kumuita huyu ni msafiri.
...ok,umekuja upande huo..vizuri,achana na visa Mana vinahitaji kdogo elmu ya ziada kuvielewa..

Kuna hadithi sahihi ya mtume inasema..."ISHI DUNIANI KANA KWAMBA MGENI AU MPITANJIA"
Je,huyu mpita njia ana tofauti na msafiri?

Hv ni kweli msafr lazima awe na nyenzo,au kwa vle umezaliwa karne ya vpando ?...watu zaman walkuwa wanasafr kwa miguu ujue.
 
Neno safari mnalitumia kimakosa na nimakosa makubwa kusema mimi ni msafiri na hapa duniani ninapita,,,Kwa sabubu ya maneno ya Muumba wetu ambayo tumekua tukiyasoma na kuyanukuu kila tunapozikana."Kutokana na udongo Tumekuumbeni.na humo Tutakurudisheni,kisha tutakuihisheni kama awali ili kila mmoja apate hesabu yake",
Kimsingi asili ya Mwanaadam ni udongo.
Huoni aibu unapotamka kwa macho makavu kuwa udongo unasafiri?,
...unaijua hadithi hii..ISHI DUNIANI KANA KWAMBA MGENI AU MPITA NJIA...
Mana hzo aya na visa vinaitaji elmu kdogo kufahamu.

Duuuh...kaka unasafari ndefu ya kujifunza juu ya asili yako na maisha yako kiujumla..
 
...ok,umekuja upande huo..vizuri,achana na visa Mana vinahitaji kdogo elmu ya ziada kuvielewa..

Kuna hadithi sahihi ya mtume inasema..."ISHI DUNIANI KANA KWAMBA MGENI AU MPITANJIA"
Je,huyu mpita njia ana tofauti na msafiri?

Hv ni kweli msafr lazima awe na nyenzo,au kwa vle umezaliwa karne ya vpando ?...watu zaman walkuwa wanasafr kwa miguu ujue.
Hadithi ipo sahihi haina mushkel.kosa lako ni moja tu unajenga hoja bila uelewa....na unabisha km sio mtafuta Elimu....vip mbona hajainukuu na riwaya nyingine inayosema "ITAFUTE DUNIA KAMA HUTOICHA" uelewa wk juu ya Mantik ya hadith ni wa chini mnooo.unasoma maandishi bila kufanya uchambuzi...Nichambulie basi hadithi hii
"Ipende dunia kama hutoondaka na itafute akhera kama unaondoka sasa hivi",
 
Kuna nadharia nyingi kwanini tupo hapa Duniani

Kwa hizi imani kuu ni kumtumikia Muumba na kutii maelezo yake kwa mujibu wa vitabu vyake vitukufu ili kuja kuupata uzima wa milele uko mbinguni/Akhera

Pia kwa wadadisi zaidi na ambao wamejikita kwenye spirituality nao wana nadharia zao nyingi

Wengine wanasema tunatakiwa kufikia utambuzi wa juu zaidi kujua lengo letu la kuwa hapa na hasa kupitia njia za Tahajudi/Taamuli ‘meditation’ hatimae unafika kwenye ‘Enlightenment’ utambuzi wa juu kabisa kuhusu wewe na hapo ndo pazia linawekwa wazi kukuhusu wewe na mahusiano yako na maumbile yote kwa ujumla

Utafikaje kwenye huo utambuzi ndo hapo napo changamoto tena maana kuna njia nyingi na walimu wengi

Pia naona upande wa science wao wanaendelea kuumiza vichwa kivyao na labda itafika muda wanaweza ku ki trick kifo , we never know
 
"Ipende dunia kama hutoondaka na itafute akhera kama unaondoka sasa hivi",
Ahahaaa...hii hadith umeiokote jalala gani..embu nletee mapokez na usahihi wake,kama hivi

Kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنهما ambaye alisema:

Mtume صلى الله عليه وسلم alinishika bega na akasema: Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.

Maisha ni safari
...Mimi na wewe ni wasafir
 
Au nakosea kusoma ! Sijaona swali linalouliza "Faida ya uhai wa kuishi hapa duniani ni nn?".

Kuna maswali mengi kwenye hoja ya muulizaji ikiwemo kwanini tupo hapa duniani?, tupo hapa kufanya nini, tunatokea wapi? Kwanini tunazaa, kwanini tunatafuta pesa/ tunajenga majumba na tunazaa Watoto ili wafanyaje?. Na nafkili maswali yote hayo nimeyajibu

. Labda nijibu na hilo swali uliloongeza wewe. Faida ya uhai uhai wa kuishi hapa duniani ni nini? Jibu: kabda mwanadamu hajaumbwa na kuletwa duniani huumbwa nafsi ambazo badae hupachikwa kwenye kiwiliwili kilichopo tumboni kwa mama (Mimba) . Nafsi kabda yakushushwa kwenye kiwiliwili huingia mkataba na Mwenyezi Mungu kuwa itaishi miaka mingap, itakuwa kiumbe cha aina gani na nafsi humuakikishia Mwenyezi Mungu kuwa itakuwa kiumbe bora japo Mungu hujua yaleo na ya kesho hivyo huipa muda wa kuwa hai nafsi ili baada ya maisha (umri walokubariana) kuwa umekamilika aje aiulize tulikubarianaje na umetendaje? ..

Faida ya kuwepo hapa duniani

1: Mwanadamu kaumbwa aje awe kiongozi aitawale dunia na vilivyomo katika kumtukuza Mola .

2: Mwenyezi Mungu katupa nafasi yakuishi ili tutengeneze hatima ya kesho yetu (akhera) wenyewe mana Mwenyezi Mungu haukumu kitu ispokuwa kwa yale kiliyoyatenda.

3: kumbuka hapa duniani tupo viumbe wengi hivyo tunachujwa wale wema tukaishi kwenye ufalme wa mbinguni milele na waovu wakatupwe jikoni

4: Tofauti ya Mwanadamu na viumbe wengine kama Malaika, Wanyama na ndege ni kwamba Mwanadamu amepewa akili na matamanio Malaika amepewa akili Pasi na matamanio Wanyama na ndege wamepewa matamanio bila akili. Ko Faida ni kwamba tuna nafasi yakutumia akili katika muda wa kuishi hapa duniani (tuloingia mkataba na Mwenyezi Mungu) kwa kuendesha maisha yetu huku tukitengeneza hatima yetu .

Kwa hiyo tambua uhai ulopewa wewe ni agano (mkataba) Kati ya wewe na Mola wako hivyo faida yake ni kuutumikia mkataba huo na umepewa akili yakutambua jema na baya ili ukikiuka mkataba uhukumiwe bila kuwa na sababu yakujitetea
Utopolo!
Tuanze na #1 hapo:wewe bnafsi mpaka leo hii unatawala nini na nini ambavyo vipo chini ya utawala wako??
 
Ahahaaa...hii hadith umeiokote jalala gani..embu nletee mapokez na usahihi wake,kama hivi

Kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنهما ambaye alisema:

Mtume صلى الله عليه وسلم alinishika bega na akasema: Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.

Maisha ni safari...Mimi na wewe ni wasafir
Unauona ujinga wako sasa? Hata kama nitakutajia kitabu kinachopatikana hadithi hio umeishakiita jalala.Waswahili wanamisemo yao "Hakika Duburi ni nyumba ya Kimba hata uuoshe kwa sabuni yenye marashi kiasi gani kamwe hautoacha Kunuka",
 
Kuna kitu watu huwa hawawezi elewa kwa sababu they cant think outside the box..

Wea re living in a simulated world( universe) ..
Ni somo pana sana hili kiasi kwamba ukimweleza mtu hawezi kukuelewa na zaidi utaishia kuzinguana nae kwa sababu atakuona unapotoka sijui umemdharau muumba aliyekuumba but reality kabisa we are living in a simulated controlled manner of life..

Amini usiamini something super intelligent being is controlling your(my) life..

We human being and other seenable species are just existing kwa sababu ya experimental issues..

kuna kundi la viumbe somewhere wametengeneza viumbe sisi kwa sababu ya majaribio yao binafsi and probably cross link superhybrid ya genetics zao...

Ukikaa na kufikiria kwa makini lengo la wewe au mimi kuwepo hapa duniani physically ni utopolo kabisa yani unazaliwa unasoma unakuwa unaoa na kuwa na familia yako kisha unazeeka unakufa then unajiuliza lengo la kupitia hizo changamoto zote ni nini sasa ...

Hakuna thamani yoyote hapa duniani zaidi ya kupitia intensity ya maumivu katika kusurvive kwa sababu tunassma "surviving is costful".

Kaaa chini mwenyewe jifungie ndani halafu uwaze bila kumhusicha mtu yoyote kwanini upo hapa utagundua kuwa the world was artificially created for making habitation ya sisi ambao ni experimental organisms kwa ajili ya maisha ya watu( beings of somewhere).

You must believe in any ways kuwa The world is just an eco systeme artificially created enveronment kwa ajili ya kusupport maisha ya hawa viumbe ambao walikuja kumwagwa hapa ili kuenddelea kuchunguzwa..

.........ni kama vile uchimbe bwawa kubwa kisha uje umwage mayai ya samaki kutoka china halafu uanze kumonitor jinsi samaki hao wanavyokuwa na kuzaliana huku lengo unakuwa unaangalia jinsi unavyoweza kuwafanyia hydridization changes katika mfumo wao mzima wa kijenetiki zaidi ili upate the desirable species kwa experiments zako ..

we are living in an eco systemed simulated world ambyo imewekewa mazingira yote ya kusurvive and no body can escape the dome..
View attachment 1586802
Amini usiamini we are nothing rather than experimental part of beings controlled by other species of which you can call in whatever names but belive kuwa hilo kundi lipo..

Chukulia mfano unafuga kuku za kizungu ambazo umewafungia ndani ya jumba kwa kuwapa mwanga wa taa ambazo zinawaka zenyewe giza likiingia na kujizima jua likichomoza(self controlling) , umewekea maji ya bomba ambayo hutiririka baada ya masaa kadhaa ,halafu wanakula mchele wa kudonoa ambao umeuweka kwenye vikontena humo humo ndani ila kuku hao wanatakiwa kujiongeza namna ya kufunua hayo makontena ya mchele,,means kuku anayegundua kuwa humu humu ndani kuna mchele ndo anayesurvive kwa muda mrefu zaidi ila hatajua ni nani ni supplier wa chakula kile kwani stock ni kubwa na ilikuwepo kabla hata hawajatotolewa..so anayejua destination ya maisha ya kuku wale ni mfugaji pekee ambaye kuku hawawezi kumuona ..

Hayo ndo maisha halisi tunayoyaishi..dunia yetu ina majani na mimea na kila aina ya chakula ili kuweza kukufanya wew uendelee kusurvive while contuing being controlled mindly and all other aspect of you life but you can not escape the dome..

View attachment 1586812
The human eye can only see visible light, but light comes in many other "colors"—radio, infrared, ultraviolet, X-ray, and gamma-ray—that are invisible to the naked eye.
human eyes can not see and tell us the real life behind us which controls our fate kwa sababu macho yanaona visible light ambayo ni 3% tu means 97% ni invisible light ...manake nini chochote unachokiona ni 3 percent ya all components za mwanga hence vingi huwez viona so kumuona anayekucontrol ni ngumu sana kwa sababu umepewa limit ya kung'amua mambo..kuna mengi hatuyajui na ni ngumu sana kuyaelewa ..

Kwa hiyo binafsi naamini we are nothing rather than the chosen species to exist in this super conducted life support experimental project ..

..
Real kiongozi
Nmepata kitu aseeeeh
 
Kwani ukiwaheshimu wazazi wako unapata faida gani?
Sababu wao ndio wamekuzaa na wamekulea na wamekupa kila kitu ulichotakiwa kupata ila still kuwaheshimu ni maamuzi yako.

Pia tofautisha kati ya kuheahimu na kuabudu hayo maneno hayaingiliani.
 
Dah mi mwenyewe huwaga nachoka hapo tu,nahangaika ili nipate kitu cha kula leo na kuweka akiba ya kesho na ukisema ukae tu bila kuls chochote unakufa njaa!sasa sijui lengo letu hapa duniani ni kula tu?maana yote wanayosema ndio lengo la kuletwa duniani ukiyaacha kuyafanya haufi sasa acha kula kama week nenda kasali uone.

Mkuu kwani tunaishi ili tule au tunakula ili tuishi...????
 
Kwanza kuzaliwa, Pili mapenzi, tatu kifo...

Tupo hapa kwa ajili ya hivyo vitu vitatu tuu...



Cc: mahondaw
 
Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137
Nimepitia hoja yako kwa umakini mkubwa lakini pia nimepitia comments zote 314 kwa umakini pia ila mpaka sasa hoja au swali lako
'' Lengo la sisi kuwa apa duniani nini? "
Ilo jibu hutalipata apa duniani ata Suleiman alisema '' yote ni ubatili chini ya jua ''

Ili upate jibu inabidi uvue dini ukivua dini utakosa andiko maana ata wanasayansi hawana pakushika.
Ebu lifanye kama fumbo la IMANI.
 
Hapa duniani mwanadamu yupo kwa ajili ya kufikiri, kuwaza, kuvumbua

Kwa kuwa mwanadamu ni mnyama anayejitambua, akitaka kumaliza shida zote hapa duniani njia ni moja tuu kuacha kuzaliana, kufunga kizazi.

kisha kukaa kwa pamoja na kukubali tofauti zilizopo baina yetu wanadamu ambao tumetapakaa dunia nzima ni ujinga kumchukia binadamu mwenzako kisa tu anatoka mahali pengine, ana dini nyingine, ana utamaduni tofauti ... Yapaswa binadamu wote tujue siye ni damu moja

Kifo kwa mwanadamu ni jambo la neema kwani uwepo wa kifo kwa maisha ya mwanadamu kumepelekea mwanadamu kutunga na kufikiri mambo mengi sana. Kuna nyimbo, kuna hadithi, kuna ujenzi mkumbwa kuwahi kufwanya - piramid za mirsi, mahekalu huko ulaya. Na kifo ndicho kinatoa nafasi ya mtu kukumbukwa kutokana na yale aliyofanya enzi za uhai wake

Binadamu yupo ili afanye mambo yatakayo kumbukwa milele na milele mpaka pale wanadamu atakapoacha kuishi au baada ya jua kuexpire
yoga with love
 
Nimesoma bandiko lako pia nimesoma maandiko ya wachangiaji.

Jina lako unaitwa Yoga. Mcheza Yoga ni Yogi sijui kama wewe ni Yogi au jina tuu.

Mimi ni Yogi, na hili swali ndio invitation yetu kwenye Yoga.

Nimejiuliza swali hili toka nina miaka 6 au 7. Baada ya best friend wangu kufa ghafla. Kwa sababu wazazi wangu hawakuwa washika dini. Nimetafuata jibu kupitia dini mbalimbali mpaka nilipojiunga na Yoga na meditation. I have meditating since was 20 yrs old and now I am 60, I got God realization at 58 yrs of age. Jibu la swali lako sio la kufikirika bali nila kiroho. Hupaswi kuambiwa wala kusimuliwa na mtu mwingine. It is called Self realization process.

Kujua purpose of life jifunze kwa mtoto machanga. Pale anaposhangaa na kutaka jua nini kimemzunguka? Kwa macho, kugusa, kusikia. Bahati mbaya tukisha pevusha akiri zetu tuna give up kutafuta jibu la ukweli na sahihi tunakubali kupewa madesa na Dini za wazazi wetu kama nilivyosoma michango mingi ya wachangiaji hapa.

We have purpose to be here, so find it, it will make you free.

Hebu angalia vitu vyote vilivyokuzunguka hapo ulipo vina kila sababu ya kuwepo na sababu kubwa ni kukuhudumia wewe. Sasa haiwezekani uwepowako usiwe na sababu.

Wachangiaji wengi wamesema ilitumuabudu Mungu, je ni kwanamna gani? Mungu ni nani? Au ni nini?.

Narudia tena this is self realization process, althouth jibu ni moja na linafanana lakini halijibiwa kwa simulizi au hear say.

Soma Biblia Yohana 4: 20-23 pia Ufunuo 1 kuanzia 9. Yesu alijua jibu la swali lako lakini hakuwapa majibu wanafunzi wake bali aliwaonyesha njia ya kupata jibu. Njia hiyo ndio njia ya UZIMA WA MILELE.

Yoga ubarikiwe sana, ni mwanzo mzuri.
 
Yaani swali hili huwa najiuliza na linaniumiza kichwa sana. Sipati majibu.
Wiki iliyopita jirani yangu aliamua kujimaliza kwa kuichoma nyumba yake moto yeye mwenyewe akiwa ndani. Bahati nzuri tuliwahi kumwokoa na tukafanikiwa kuuzima ule moto.
Wakati huo yeye alikua tayari ameshapoteza na fahamu. Baada ya muda akaamka, badala ya kuanza kutushukuru kwa kumwokoa, akaanza kututukana matusi na kudai tungemwacha afe.
Sasa mpaka sasa hatujui nini kilimpata mpaka achukue uamuz ule. INAWEZEKANA yeye pia alikua anajiuliza swali hilihili na akapata jibu hakuna faida yoyote ya kuishi/ kupambana na maisha kwani muda wowote sisi ni wakufa tu.
Kwa upande wangu mimi, nipo kwenye ujenzi wa nyumba yangu, najiangalia ninavyojinyima kwa ajili tu ya hii nyumba. Kipato changu kidogo, ikifika mwisho wa mwenzi, nikipata pesa yangu yote napeleka huko.
Sasa najiuliza ikiwa watu wanakufa wa rika zote kwa ajali au magonjwa, mimi ni nani nipo hai. Kama wao pia walikua hai then mimi pia huenda muda wowote nitakufa tu. Sasa kwanini niendelee kuhangaika!? Kwanini nisijikite tu kwenye kula na kuvaa nikisubir siku yangu.
Kwa kweli mimi pia sijui sababu hasa ya sisi binadamu kuwepo hapa duniani kwa sababu uwezekano upo mkubwa watu wanakufa bila kutimiza/kujua lile kusudio la wao kuwepo duniani.
 
Kamwe binadamu hatokuja kujua ni kwa nini anaishi, lengo la maisha ya mwanadamu halitokaa lijulikane na wanadamu ila linafahamika na yule aliyemtengeneza mwanadamu (kama yupo). Kwa hiyo mkuu we endelea na huo mzunguko tu.
Wrong.
 
Back
Top Bottom