"Muwe kama watoto wadogo". Biblia inasema hayo. Biblia haisemi "kuweni na "upendo" kama watoto wadogo".
Kisaikolojia watoto wadogo ni "wabinafsi" - wanataka kila kitu kiwe chao tu wakipate wao tu na kwa ajili yao.
Angalia dunia - kila kitu na katika kila kitu. Unaona nini? Hakika huwezi kuona kitu kingine isipokuwa "Upendo".
Uumbaji wote ni upendo hivi ndivyo pia Mungu analenga mtu awe.
Ulimwengu ulimalizika. Mungu akamuumba mtu. Biblia inasema, tumuumbe mtu kwa sura na mfano wetu.
Mungu ni upendo. Hivi ndivyo ulivyo uumbaji, ni upendo. Mtu ambaye ni sura na mfano wa Mungu, lengo lake la kuwepo duniani ni hilohilo, "UPENDO".
Kwa mantiki hiyo kabla ya Kuwa hai hapa duniani tulikuwa tayari tumepungukiwa upendo ,hivyo tukaletwa hapa kujifunza huo upendo?
Kwa namna zote mtoto yuko close na sacredness kuliko mtu nzima,pamoja na ubinafsi wake, mtoto hana akili za kuficha ubinafsi.
Watu wazima si kwamba si wabinafsi ,wamefunzwa ubinafsi si tabia njema,kwa hiyo wanaficha hiyo intrinsic quality,
Na hii tunaiona siku hizi kwenye shughuli zinazohitaji kujitoa ,hasa maswala mazima ya michango ya harusi ,watu wanatoa michango ila pembeni wanalalamika,
Wanajua kutotoa ni ubinafsi(bad quality), wanalazimika kutoa kinyonge ili kuficha hiyo quality
Binadamu wote wanaoperate kwenye individualism,ukitaka kujua kama binadamu (mtu mzima) ni mbinafsi,put them to test
Waweke kwenye mazingira yanayohatarisha uhai wao,in the very end,Kila mtu atakuwa anapigania uhai wake ,analinda vilivyo vyake,
Ukipata tatizo kubwa either financially au afya ikatetereka ,marafiki huwa wanaanza kupungua mmoja mmoja kadiri tatizo lako linavyokaa na wewe Muda mrefu. UNAPATA UJUMBE GANI KUHUSU BINADAM UKIONA HAYA?
Ukiangalia kwa makini binadamu wanaishi kwenye phases
Wakati wa utoto (zero life experience) na uzee (full life experience) hapo ndo unapata best qualities za binadamu, (in terms of upendo)
bahati mbaya hizi phase mbili mtu huyu anakuwa dependant ,unalazimika kuexpress best qualities instinctively ili usaidike
,japo si wote
Phase ya katikati hapo ina mambo mengi mengi kidogo