Lema azidi kuibomoa CCM Arusha

Kama ana uwezo, mkaribisheni humu ndani tuone na tupime uwezo wake. Mbona wenzake wanaojiamini wapo humu ndani?

Fungueni thread yenu ya kujadili hizi kelele za chura mnazopiga.
Aisee hii M4C inawanyima raha kiasi hichi nyie green guards??
Najua hamna namna kwa sababu mko utumwani.
 
... Nguvu za Sala na Kufunga BILA UNAFIKI ndio kama hivo; na hadi hapo bado ni mwanzo tu!!!
 
Wanabodi mtu ukikosa maono nadhani ni ugonjwa mmbaya sana! Hebu fikiria vuguvugu lote hili la chama kubomoka ila kuna mtu kama chatanda anaona chama kipo pouwa na hata uchaguzi ukirudiwa watashinda! Ee mola endelea kuwapa upofu tuchukue nchi kama upepo!
 
Kumbe jibu unalo...

ni kuongezee usemi mwingine aliowahi kuusema "...ni vyama vya msimu..." lakini cha ajabu huo upepo asipo jipanga unaondoka na nymba yeye achekecheke tu..je chadema bado ni cha msimu je msimu wake unaisha lini...
 
Wabunge wote wa chadema wasiojisajiri JF kwa majina yao nina mashaka nao!

why?

Mkuu William aka baharia, alipokutana na Nasary bungeni alimuhakikishia kuwa yeye ni active member JF, lakini cha ajabu

hakuna ID ya nasary tunaoijua.

Tabia hii imepelekea kuanzishwa post za kujisifia hasa za lema na nassary, Mimi natilia shaka huenda ni..........

anyway just guessing .................

tume ya katiba ni jina lako?
 
Kama ana uwezo, mkaribisheni humu ndani tuone na tupime uwezo wake. Mbona wenzake wanaojiamini wapo humu ndani?
Yupo ila anaangalia hoja za kujibu.....
Rejao km Lema angekuwa na IQ ndogo asingewaumiza vichwa namna hiyo
 
Nina uhakika kuwa Mhe. Lema hajisifii kabisa kwani nina vigezo!!
1. Siku moja tukiwa nae katika feri iitwayo "MV MISUNGWI" akiwa katika ziara yake ya KANDA YA ZIWA pamoja na Dr.Slaa; alihutubia ndani ya kivuko hicho kutoka BUSISI-KIGONGO; alivutiwa na umati mkubwa mno; nilipost hapa JF na FB kuhusu huo umahiri wake; kitendo kilichosababisha akapigiwa simu; hakusita kuuliza aliyepost na papo ndipo nikajitokeza; nilimpa simu yangu akatazama comments kisha akanipa simu yangu. (walikuwa wanatoka SENGEREMA nami natoka GEITA).
2. Wanaopost ni watu tofauti tofauti ambao haiwezekani wote wakawa ni Mhe. Lema
... chadema ni Chema chajiuza CCM kibaya chajiuza
 
Last edited by a moderator:
KAMA KIPIMO CHA IQ YA KAMANDA LEMA NI KWA KUZINGATIA VIGEZO BINAFSI VYA REJAO BASI M4C ENDELEENI ZAIDI KUKIFUNDISHA SOMO MAFISADI MPAKA KIJANA HUYU ASUUZIKE NA ROHO YAKE MWENYEWE

Kama IQ ya mtu hupimwa na uwezo wake wa kuchonga dili kuibia Umma na kujinunulia mijumba kwa mamilioni ya hela za kigini, basi hiyo IQ-Rejao siitaki hata tone.

Lakini kama IQ inayozungumziwa hapa ni ile ile Intelligence Quotient na maana yake ya kuonyesha ubunifu wa hali ya juu kukamilisha jambo ambalo huko nyuma lilikua ni kama ndoto tu vichwani mwetu WaTanzania kama vile kuhamisha vijiji jumla jumla toka CCM kwenda CHADEMA (Jambo ambalo Mhe Kikwete pamoja na msururu wa Ma-PhD zake kamwe hawezi kukifanyia chama chake hivi sasa) basi hadi hapo wala sina haja kumuelekeza Kamanda Lema kuti gani zaidi kukifanya kule M4C mpaka Rejao apate kukimbia jukwaa hili kama wenzake Malaria Sugu pamoja na yule mama mbishi kama daga FaisaFox.

M4C chonde, kuna kazi ya dharura inawasubirini kule Mkuranga. Hebu katangulizeni kwanza BAVICHA na BAWACHA na nyinyi kuja kumalizia kiulaini tu.
 
Nina uhakika kuwa Mhe. Lema hajisifii kabisa kwani nina vigezo!!
1. Siku moja tukiwa nae katika feri iitwayo "MV MISUNGWI" akiwa katika ziara yake ya KANDA YA ZIWA pamoja na Dr.Slaa; alihutubia ndani ya kivuko hicho kutoka BUSISI-KIGONGO; alivutiwa na umati mkubwa mno; nilipost hapa JF na FB kuhusu huo umahiri wake; kitendo kilichosababisha akapigiwa simu; hakusita kuuliza aliyepost na papo ndipo nikajitokeza; nilimpa simu yangu akatazama comments kisha akanipa simu yangu. (walikuwa wanatoka SENGEREMA nami natoka GEITA).
2. Wanaopost ni watu tofauti tofauti ambao haiwezekani wote wakawa ni Mhe. Lema
... chadema ni Chema chajiuza CCM kibaya chajiuza
 
Last edited by a moderator:
Rejeo kachukia nini wakati ccm wenyewe wamewakataa wenzao na kuwa-label kuwa ni watu wa chadema?
Imekuwa ni kauli ya kawaida kusikia kuwa Chadema ni chama cha kaskazini. So, Arusha kama kaskazini ni mali ya Chadema full stop.
Karibuni wana ccm tujiunge Chadema kuikomboa nchi yetu tuliyonyang'anywa na wakina Rejeo.
 
Back
Top Bottom