Wajameni,
Ni muda mrefu umepita kuushuhudia umati mkubwa kama huu."There are currently 3660 users browsing this thread. (1140 members and 2520 guests)"
Ukiangalia idadi ya members na wasio members, wasio members ni mara mbili ya members, hii inamaanisha jf, inatembelewa zaidi na wasio members kuliko hata members, hivyo this jf is very powerful media!.
Asante kwa hukumu hii ya Lema, leo imetuunganisha na long lost friends tuliopotezana nao kipindi kirefu nyuma!. Kwa maoni yangu, kile kidole Lissu alichounyooshea mhimili huu wa mahakama pia itakuwa imechangia angalau kwa mahakama kuu ya rufani kuwathibishia Watanzania kuwa kuna wakati, wanaweza kutoa uamuzi wa haki!. Sijui kwenye ile kesi ya mgombea binafsi, walishikwa na kigugumizi cha nini!.
Kuna kiongozi mmoja mkuu tuu, alifurahia Lema kuvuliwa ubunge, kwenye mkutano mmoja wa kimaifa uliofanyika mjini pale AICC, alijitapa,"afadhali sasa Arusha imetulia, hata mikutano kama hii imeweza kuja Arusha na watalii sasa wanarejea!. Wito kwa Lema, Chadema na wafuasi wao, "msibweteke na ushindi huu, bali uchukulieni kama changamoto kuelekea 2015!. Chadema lazima ibadilike na kufanya siasa za ukweli na sio siasa za ushabiki wa kushangiliwa na umati wa watu kwenye mikutano au maandamano!.
The politics of confrontations will not get you anywhere!. Chadema must practice real and true politics, hizi ni "resiponsible politics" zenye malengo, mipangi mkakati na work plan ya utekelezaji, na sio "politiking siasa za majukwaani tuu na maandamano!. 2015 sio mbali, Chadema isipobadilika na kujipanga vizuri, 2015 ni CCM Tena!.
Hongera sana Lema, Hongera Chadema, mtihani ni 2015!.
Pasco.