Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

Leo mahakama imefurika mapema, hali ya hewa ni nzuri,

Updates:

- Bado hukumu haijaanza kusikilizwa, nyuso za wakombozi zimejaa bashasha. Hii ni dalili nzuri kwa kupokea matokeo!

- Viongozi wote wachadema ndio (Mh Mbowe na waambata wote) wanaingia, watu pipooooziii

- Kamanda Lissu ndio anaingia watu pipooziiii

- Naaam kamanda, Ben Saanane ndio anaingia. Sasa kazi mtindo mmoja, ukombozi unakaribia

- M/kiti wa Bavicha Heche ameshawasili eneo la tukio. Bado tunawasubiri majaji tu

DSC00029.JPG

Lema, Mbowe na Mnyika wakiwa Mahakamani

DSC00031.JPG

Hawa ndo waliofungua kesi

More Updates:

- Tumeamriwa kuzima simu zote, sasa majaji wanaingia,

- Kwanza hukumu inaanza kusomwa!

- Kwanza inasomwa historia ya kesi hii, tukio kwa tukio

- Mtanisamehe sitaripoti kila kinachotamkwa na msoma hukumu, naripoti yale muhimu tu, mfano vifungu vinavyo muingiza au kumtoa mrufani na hitimisho la mahakama tu!,

- Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udharirishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM)

Tumeshindaaaaa!

Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema,

CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia!



Picha baada ya ushindi:
DSC00054.JPG

DSC00067.JPG

DSC00078.JPG



Hapo kwenye red, muwe mnafikiria kwa uangalifu hata kama hamuipendi CCM!!!! Siyo kweli kwamba CCM ndo wanastahili kulipa gharama za kesi...... Anayestahili kulipa ghama za kesi ni yule aliyefungua kesi!!!! Kama ulivyoripoti kwenye picha, hao kina mama waliofungua kesi ndo watalipa gharama. Sahihisha hapo....
 
hongera kamanda LEMA. MUNGU yupo upande wetu, wao wana PESA na sisi tuna MUNGU
 
ushindi wa rufaa hii imeonesha jinsi gani mahakama haiko makini.Mwanzo alivuliwa ubunge sasa hv amerudishwa ina maana mwanzon walikua hawajui wanachokfanya wamezungusha sana chombo hcho ni dhaifu kijpange upya
SAWA mkuu japo ingependeza kama ungetwambia mbali na mahakama ni department gani nyingine iko makini katika nchii hii kwa sasa!
 
Kila mtu apate kinywaji anachotaka, mwambie mhudumu alete bili kwangu hapa. Hata kama wewe ni PM7 na ccm, pata kinywaji tu usijali
 
ushindi wa rufaa hii imeonesha jinsi gani mahakama haiko makini.Mwanzo alivuliwa ubunge sasa hv amerudishwa ina maana mwanzon walikua hawajui wanachokfanya wamezungusha sana chombo hcho ni dhaifu kijpange upya

husilolijua huwa nizaidi hata ya usiku wa giza.
 
Hapo kwenye red, muwe mnafikiria kwa uangalifu hata kama hamuipendi CCM!!!! Siyo kweli kwamba CCM ndo wanastahili kulipa gharama za kesi...... Anayestahili kulipa ghama za kesi ni yule aliyefungua kesi!!!! Kama ulivyoripoti kwenye picha, hao kina mama waliofungua kesi ndo watalipa gharama. Sahihisha hapo....
sawa mkuu lakini unadhani walijituma hao!!??
 
inavyoonekana mahakama ilifanya kwa malengo yake lakini walivyoona kukomaliwa kila upande wakaona hamna tena ujanja lazima kijana arudishwe bila hivyo AR hapakaliki na wakimtosa wataingia kwenye aibu nyingine kwenye uchaguzi maana hata akisimamishwa yeyote kwa bendera ya CDM basi lazima atashinda ndiyo maana wakasema basi mrudishie tu


Ndiyo maana tunasema tunataka mabadiliko
 
hongera kamanda LEMA. MUNGU yupo upande wetu, wao wana PESA na sisi tuna MUNGU

Una maanisha nini? Kwamba wao hawana Mungu? Maana yake nini? Kwamba pesa ni za shetani na Haki ni ya Mungu?
Fafanua..... Maana usije ukawa uko kwenye mkumbo wa kushangilia tu kama ambavyo watu wamekuwa wakiingia kwenye mkumbo wa maandamano wasiyojua lengo lake ni nini, hatimaye kupigwa risasi........ Kuwa mkweli na makini wewe.....
 
Mafisadi wameshindwa! Wameona afadhali wamrudishie kamanda Lema ubunge wake kwani wamegundua kwamba hata wakirudia uchaguzi mafisadi hawawezi kushinda. Viva Chadema. M4C 4EVER!
 
Pipoooooooooooooooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!
Ni habari njema kwa wapenda mabadiliko, Ni habari njema kwa wana Arusha kurudishiwa haki yao iliyo taka kupokwa na wakoloni weusi!
Mahakama kwa sasa lazima watende haki kwani waraka wa Kamanda Lisu kuwahusu umewagusa sana!

Viva Chadema Viva Ukombozi. Hongera G. Lema. Hongereni wana Arusha wote.
 
lakini hii isiishie hapa, pamoja na huyu jaji aliyehongwa kuwa ameshalaaniwa kwa kutetemeka, lazima chadema ishitaki ili avuliwe ujaji, huo ndio ujaji wa kishikaji na kikwete, maana tunajua mshikaji wake Chande hana uwezo wa kumuwajibisha huyo jaji mshenzi
 
sawa mkuu lakini unadhani walijituma hao!!??

Hataki kufikiri ameamua kujifungia kwenye box bila sababu za msingi na bahati mbaya hatuna namna ya kumsaidia!

Mungu tunakushukuru kwa zawadi nzuri ya xmas na mwaka mpya 2013. Kwa Lema, CHADEMA na wote wenye kuitakia mema nchi hii ninawapa pongezi nyingi sana toka moyoni.
 
waliokuwa wanategemea kugombea ubunge arusha mjini kwa kumchafua lema wakachukue form. na wilioapa kwamba lema akishinda warudisha kadi za chadema wakati ndio huu. Chadema, Chadema, Chadema.....................Mungu ibariki Chadema
 
Hongera kamanda Lema, hongera CDM
Naona nina bahati kwani nimejoin JF jana na leo napokea taarifa nzuri
 
Back
Top Bottom