Eddo Sambai
JF-Expert Member
- Aug 1, 2013
- 2,344
- 1,771
Katika Bunge linaloendelea hivi sasa Dodoma, Mb Lema katika kuwasilisha mchango wake kuhusu ripoti iliyowasilishwa bungeni juu ya wizara ya mambo ya ndani amesema
"Katika ripoti yote iliyoandikwa katika kitabu hiki sijaona ikielezea au kuzungumzia bomu la soweto wakati bomu la olasiti limezungumziwa, Chadema ilisema tunaushaidi wa DVD juu ya aliyehusika na ulipuaji wa bomu la soweto na tukashauri Raisi aunde tume huru ya kimahakama ili tuwasilishe ushaidi wetu. Cha kushangaza haijaundwa mpaka leo na hawataki kufuatilia swala hilo" mwisho wa kunukuu.
My take
Hapa inaonyesha kuwa Chadema walionewa na ni kweli Serikali inausika juu ya ulipuaji wa bomu la soweto na sasa wanachokifanya ni kupiga chenga ili kuficha ukweli.
nkongu ndasu[SIZE=3 said:;8108773]Teh teh,kamanda lema, kawashika magamba!
..... Kwa Dr.Mvungi unaona wanavyojivuta kama Mrenda. Ukweli utajichuja hata kama ni taratibu
Muungwana chitambikwa...wenye akili tunajua...nani aliyemnyamzisha Dr....lengo ni kuivuruga Tume ya Warioba...Dr. akiwa ni msomi aliyebobea kwenye sheria hasa KATIBA...alikuwa nguzo ya Tume. Tunajua Tume imeyumbishwa sana na kuondoka kwa Dr...
Wenye akili tunajua Mipango yao ya kuvuruga mchakato wa KATIBA ili waendelee kubaki madarakani.
Iko wazi serikali inahusika, tatizo kubwa hata huko Serikalini kumegawanyika.
Kuna viongozi wengine wa serikali kuu walikuwa hawajui huu mchezo sasa kimenuka kila mtu anakimbia.
Mzigo mwingine Nchimbi atueleze ilikuwajekuwaje
Hili ndilo linanitatiza sana "wenye akili tunajua mipango yao ya kuvuruga mchakato wa Katiba.........." Jee hao wenye akili wanachukua hatua gani? Au ni kunyamaza tuu?
Basi tuwapongeze na kuwatia nguvu watu kama Lema wenye uthubutu wa kuongea na kuweka hadharani maovu ya hao wenye mipango michafu.
Lema anataka apewe majina ya wenye pesa Uswizi ili awataje hadharani. Lakini kuwataja waliolipua bomu anaweka vikwazo.
Kwani kama anauhakika na ushahidi wake kuna ugumu gani kuuweka hadharani?
Wajinga ndio waliwao...