Pentagon kuja na Bomu la Nyukilia lenye nguvu mara 24 zaidi ya lile la Hiroshima, Japan

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Idara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuja na bomu jipya la nyuklia, B61-13, ambalo litakuwa na nguvu mara 24 zaidi ya lile lililoangushwa huko Hiroshima wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945.

Bomu hilo jipya la nguvu ya nyuklia la B61-13 lililopendekezwa na Marekani litabebwa na kuangushwa kutoka kwenye ndege.

Bomu hilo litakuwa na mavuno ya juu ya kilotoni 360, yani mara 24 ya takriban kilotoni 15 ya mavuno ya bomu ambalo lilirushwa kwenye jiji la Japan la Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945.

Bomu lililorushwa Nagasaki siku tatu baadaye lilikuwa na mavuno ya takriban kilotoni 25.

Mabomu ya nyuklia ya Nagasaki na Heroshima yaliangushwa bila kuongozwa (free fall due to gravity) lakini hili jipya litakuwa na vifaa maalumu vya kuliongoza na kusaidia kulenga shabaha kwa ufasaha na kulifanya kuwa sahihi zaidi.

Mpango huu unakuja siku chache baada ya China kupanga kuongeza ghala lake la silaha za nyuklia (Nuclear Warheads) hadi zaidi ya 1,000 kufikia 2030.

Kwa sasa Marekani ina vichwa 3,700 vya nyuklia (Nuclear Warheads), na kati ya hivyo 1,419 vimetumwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukaa chonjo dhidi ya vita yoyote itakayojitokeza.

Hata hivyo Bomu la B61-13s litakuwa na chini ya theluthi moja (⅓) ya uwezo wa silaha kubwa zaidi ya nyuklia ya Marekani - Bomu la Nyukilia la B83 - ambalo lina mavuno ya megatoni 1.2, mara 80 ya bomu lililoangushwa Hiroshima, nchini Japan.

Vyanzo: Fox News, Daily Mail UK, Defense News
 
Mkwara mbuzi huo.
Akitengeneza ajue na mataifa yenye nguvu yatatengeneza zaidi ya hilo.
Zama za Marekani kuogopwa zipo ukingoni
Kutengeneza inaendana na bajeti ya serikali kwenye Jeshi, Marekani ndio nchi inayoongoza kwa bajeti kubwa jeshini... Ndio maana jamaa ana vimba, na hakuna nchi inayomtumishia kifua, sasa hivi anagawa silaha tu huko Ukrein na Israel, hizo nchi zako mbona hatuoni zikigawa silaha
 
Sema anagawa ma toy Ukrein, angekuwa na silaha za maana Rusia asingekuwa Ukrein hadi leo huku akiendelea kujimegea ardhi mdogo mdogo.
 
Idara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuja na bomu jipya la nyuklia, B61-13, ambalo litakuwa na nguvu mara 24 zaidi ya lile lililoangushwa huko Hiroshima wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945.

Bomu hilo jipya la nguvu ya nyuklia la B61-13 lililopendekezwa na Marekani litabebwa na kuangushwa kutoka kwenye ndege.

Bomu hilo litakuwa na mavuno ya juu ya kilotoni 360, yani mara 24 ya takriban kilotoni 15 ya mavuno ya bomu ambalo lilirushwa kwenye jiji la Japan la Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945.

Bomu lililorushwa Nagasaki siku tatu baadaye lilikuwa na mavuno ya takriban kilotoni 25.

Mabomu ya nyuklia ya Nagasaki na Heroshima yaliangushwa bila kuongozwa (free fall due to gravity) lakini hili jipya litakuwa na vifaa maalumu vya kuliongoza na kusaidia kulenga shabaha kwa ufasaha na kulifanya kuwa sahihi zaidi.

Mpango huu unakuja siku chache baada ya China kupanga kuongeza ghala lake la silaha za nyuklia (Nuclear Warheads) hadi zaidi ya 1,000 kufikia 2030.

Kwa sasa Marekani ina vichwa 3,700 vya nyuklia (Nuclear Warheads), na kati ya hivyo 1,419 vimetumwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukaa chonjo dhidi ya vita yoyote itakayojitokeza.

Hata hivyo Bomu la B61-13s litakuwa na chini ya theluthi moja (⅓) ya uwezo wa silaha kubwa zaidi ya nyuklia ya Marekani - Bomu la Nyukilia la B83 - ambalo lina mavuno ya megatoni 1.2, mara 80 ya bomu lililoangushwa Hiroshima, nchini Japan.

Vyanzo: Fox News, Daily Mail UK, Defense News
siku za USA kuwa weak na kuweza kupigwa hata na visiwa vya shelisheli zinakaribia...
 
Back
Top Bottom