Ndugu yangu,
Nilicho maananisha ni kuwa si wajibu wa Lema,Mbowe wala Chadema kuisaidia serikali iliyoko madarakani kutimiza wajibu wake.Kama wanayo hiyo DVD wanao utashi,hasa kwa uzoefu walionao kama chama kuhakikisha kuwa mkanda huo utaleta manufaa kwa kusaidia kuwatia hatiani wahusika ukitolewa.Kama wanaamini kuwa kwa kuwapa polisi ambao ni sehemu ya watuhumiwa watakuwa wamepoteza ushahidi huo mimi naunga mkono kuto utoa katika mazingira hayo.Ni sawa na binadamu amkamate ngedere anakula mahindi shambani kwake halafu ampeleke na ushahidi wa mahindi kwa hakimu ambaye ni nyani!Bila shaka akija asubuhi atakuwa hata hicho "exhibit"alichomkamata nacho mwizi wake hakipo na kesi ndio imejifuta.
CDM,Lema wala Mh.Mbowe sio wajinga kiasi unachodhani.