Lema aibuka na 'bomu la Soweto' Bungeni

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
2,335
1,753
Katika Bunge linaloendelea hivi sasa Dodoma, Mb Lema katika kuwasilisha mchango wake kuhusu ripoti iliyowasilishwa bungeni juu ya wizara ya mambo ya ndani amesema

"Katika ripoti yote iliyoandikwa katika kitabu hiki sijaona ikielezea au kuzungumzia bomu la soweto wakati bomu la olasiti limezungumziwa, Chadema ilisema tunaushaidi wa DVD juu ya aliyehusika na ulipuaji wa bomu la soweto na tukashauri Raisi aunde tume huru ya kimahakama ili tuwasilishe ushaidi wetu. Cha kushangaza haijaundwa mpaka leo na hawataki kufuatilia swala hilo" mwisho wa kunukuu.

My take
Hapa inaonyesha kuwa Chadema walionewa na ni kweli Serikali inausika juu ya ulipuaji wa bomu la soweto na sasa wanachokifanya ni kupiga chenga ili kuficha ukweli.
 
Chadema wako FIRM na serikali hapa haiwezi kuruka .Lema kamwaga maneno upya wacha tuone .
 
Ivi kuna asiye juu nani aliyelipua bomu la SOWETO
Ukitembelea Arusha waulize hata wanafunzi watakuambia
Zla zile damu hazitaishia bure Mungu atawaadhibu
Kila auwae kwa upanga na yeye atawawa kwa upanga
Ndo maana nasema hata hapa JF yoyote anayetetea kitu ili hali anajua anatetea uovu utamrudia
Itamrudi ama direct or indirect hapa hapa duniani.
 
Kweli serikali haijawahi kumpa pole mke wa Mwangosi, Kumpa pole Dr.Ulimboka na wa wale waliouwawa na Bomu. Kwa Dr.Mvungi unaona wanavyojivuta kama Mrenda. Ukweli utajichuja hata kama ni taratibu
 
nkongu ndasu[SIZE=3 said:
;8108773]Teh teh,kamanda lema, kawashika magamba!

Ni kweli kabisa mkuu, ila hii ni aibu kwa Serekali yetu inayojisifu kuwa inazingatia utawala bora, wakati huo kuna baadhi ya watendaji wake wanafanya vitendo viovu vya kuuwa raiya wasio na hatia yoyote.[/SIZE]
 
Iko wazi serikali inahusika, tatizo kubwa hata huko Serikalini kumegawanyika.
Kuna viongozi wengine wa serikali kuu walikuwa hawajui huu mchezo sasa kimenuka kila mtu anakimbia.
Mzigo mwingine Nchimbi atueleze ilikuwajekuwaje
 
..... Kwa Dr.Mvungi unaona wanavyojivuta kama Mrenda. Ukweli utajichuja hata kama ni taratibu

Muungwana chitambikwa...wenye akili tunajua...nani aliyemnyamzisha Dr....lengo ni kuivuruga Tume ya Warioba...Dr. akiwa ni msomi aliyebobea kwenye sheria hasa KATIBA...alikuwa nguzo ya Tume. Tunajua Tume imeyumbishwa sana na kuondoka kwa Dr...

Wenye akili tunajua Mipango yao ya kuvuruga mchakato wa KATIBA ili waendelee kubaki madarakani.
 
Hivi kwa nini Serikali inashindwa kuunda hiyo Tume Huru ya Kimahakama kama wana uhakika kuwa hawana damu katika mikono yao.....???
Suala la Utawala Bora hapa mbona Serikali haitaki kuwajibika....it is very disturbing.
Damu iliyomwagika haitapotea bure mpaka wote waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya Sheria ili HAKI itendeke.
Chadema musilinyamazie hili mpaka UKWELI ufahamike.
 
Lema anataka apewe majina ya wenye pesa Uswizi ili awataje hadharani. Lakini kuwataja waliolipua bomu anaweka vikwazo.

Kwani kama anauhakika na ushahidi wake kuna ugumu gani kuuweka hadharani?

Wajinga ndio waliwao...
 
Muungwana chitambikwa...wenye akili tunajua...nani aliyemnyamzisha Dr....lengo ni kuivuruga Tume ya Warioba...Dr. akiwa ni msomi aliyebobea kwenye sheria hasa KATIBA...alikuwa nguzo ya Tume. Tunajua Tume imeyumbishwa sana na kuondoka kwa Dr...

Wenye akili tunajua Mipango yao ya kuvuruga mchakato wa KATIBA ili waendelee kubaki madarakani.

Hili ndilo linanitatiza sana "wenye akili tunajua mipango yao ya kuvuruga mchakato wa Katiba.........." Jee hao wenye akili wanachukua hatua gani? Au ni kunyamaza tuu?
Basi tuwapongeze na kuwatia nguvu watu kama Lema wenye uthubutu wa kuongea na kuweka hadharani maovu ya hao wenye mipango michafu.
 
Iko wazi serikali inahusika, tatizo kubwa hata huko Serikalini kumegawanyika.
Kuna viongozi wengine wa serikali kuu walikuwa hawajui huu mchezo sasa kimenuka kila mtu anakimbia.
Mzigo mwingine Nchimbi atueleze ilikuwajekuwaje

Kwanza Nchimbi anatakiwa atueleze kuhusu yale Mawasiliano ya email ya Emmanuel Nchimbi na Mwigulu, je ni Nchimbi yeye?
 
Misiba ya wavuta unga utamuona mukulu akitoa pole, la ajabu hilo bomu la soweto hata yeye alikaa kimya, watu tulio wapoteza wlichukuliwa kama vile kuku wamekufa kwa mdondo wakati south ameenda mara mbili kwa msiba huohuo! greeeeeeeeeeeeeee!
 
Hili ndilo linanitatiza sana "wenye akili tunajua mipango yao ya kuvuruga mchakato wa Katiba.........." Jee hao wenye akili wanachukua hatua gani? Au ni kunyamaza tuu?
Basi tuwapongeze na kuwatia nguvu watu kama Lema wenye uthubutu wa kuongea na kuweka hadharani maovu ya hao wenye mipango michafu.

Mfano tumeshaonyeshwa na wenzetu wa Mwanza kwa kumpeleka mwenyekiti wa magamba mstaafu kwenye mahakama ya raia na wameshafunga jalada la kesi yake ya Uporaji, sasa akapore kuzimu.
 
Lema anataka apewe majina ya wenye pesa Uswizi ili awataje hadharani. Lakini kuwataja waliolipua bomu anaweka vikwazo.

Kwani kama anauhakika na ushahidi wake kuna ugumu gani kuuweka hadharani?

Wajinga ndio waliwao...

Lema amesimamia msimamo wa chama tume ya kijaji iundwe.Kuna ugumu gani serikali kuunda tume hiyo?
 
Watawala wetu na CCM kwa ujumla wanaamini kuwa kwa kukaa kimya wananchi watasahau kila uovu wanaofanya. Tumeona matukio mengi kama ya kutekwa na kuteswa kwa akina Dr. Ulimboka, Kibanda, kuuawa kwa Mwangosi, kurushwa bomu kwenye ibada na mkutano wa CHADEMA huko Arusha yote hayo na mengineyo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Serikali kwa imani dhalili kuwa wananchi watasahau.

Ni muhimu sana matukio kama hayo na mengineyo kama ya ubakaji na usafirishaji wa madawa a kulevya ambayo yanadaiwa kufanywa na watawala ama washirika wao yakaendelea kupigiwa kelele kila uchao ili watawala watambue kuwa kuna ufuatiliaji wa kina unafanywa na wananchi pamoja na taasisi ama vyama vya kijamii.
 
Tumekuwa mala nyingi tukisikia kauli za viongozi wa vyama vya upinzani tofauti vikiihusiosha serikali na matukio mengi tuu ya kiuovu! Cha ajabu mala nyingi wasemaji wa serikali wamekuwa wakikanusha kwa kutumia kauri nyepesi saana ambazo mwisho wa siku wananchi wengi wamekua wakiamini kwa asilimia kubwa uhusika wa serikali katika matukio hayo.

Kama ni kweli katika mawasilisho ya wizara, kwenye kitabu hamna suala la soweto halipo, ni ushahidi tosha kuwa kweli serikali ilihusika na inaogopa kivuri chake, sasa kwa mtazamo wangu, watendaji wa uovu huo wamekuwa weak kiasi gani hata kusahau kuongelea suala hilo ili ingalau kuiaminisha jamaii kuwa wao hawakuhusika?

Je ni subortage kati ya viongozi wauwaji na viongozi wenye utu? manaake inawezekana kuna viongozi ambao hawakubaliani na upuuzi huu wa kuwauwa raia, hivyo wanaonyesha madhaifu ili mwisho wa siku watu wapembue mchele na mchanga!

Sasa ushahidi umekuwa dhahili kabla ya ushahidi halisi wa mkanda mzima kuhusu tukio la soweto
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom