Lema agonga mwamba Arusha

Lema agonga mwamba Arusha

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2008
Posts
7,063
Reaction score
71

NA SHAABAN MDOE. ARUSHA

NJAMA za mbunge wa Arusha Mjini Gogbless Lema (CHADEMA) kushinikiza mgomo wa daladala na pikipiki , ikiwa ni ishara ya kupinga kuwekwa rumande, zimegonga mwamba , baada ya wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri kutomuunga mkono.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinasema wamiliki wa vyombo hivyo waliamua kutounga mkono mgomo huo , baada ya kutafakari na kuhoji mantiki yake kwa kuwa dhamana ulikuwa wazi kwa Lema lakini alikataa kudhaminiwa ili apelekwe rumande.

Jana asubuhi vijana waliosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Lema walifanya vurugu kwa kupiga mawe kila daladala na pikipiki iliyotoa huduma ya usafiri ili kuwashinikiza wahusika kugoma.

SOURCE: UHURU
 
basi hakuna habari hapo bali ni unazi tu
Source: UHURU..
 
Uhuru!! Lakini adhari zake ni kubwa katika suala zima la haki za kibinadamu kwa ujumla.
 
Mkuu thatha.

Hapa Godbless Lema hausiki na hizi jitihada za mgomo tumtendee haki wahusika wakuu ni Nanyaro diwani wa Levolosi na kikundi chake cha wahuni ndiyo wahusika wakuu.Lema alikuwa uwanja wa ndege akiongoza ndege na kufungua matawi kwa wingi ahaaaaa.

NA SHAABAN MDOE. ARUSHA
NJAMA za mbunge wa Arusha Mjini Gogbless Lema (CHADEMA) kushinikiza mgomo wa daladala na pikipiki , ikiwa ni ishara ya kupinga kuwekwa rumande, zimegonga mwamba , baada ya wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri kutomuunga mkono.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinasema wamiliki wa vyombo hivyo waliamua kutounga mkono mgomo huo , baada ya kutafakari na kuhoji mantiki yake kwa kuwa dhamana ulikuwa wazi kwa Lema lakini alikataa kudhaminiwa ili apelekwe rumande.

Jana asubuhi vijana waliosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Lema walifanya vurugu kwa kupiga mawe kila daladala na pikipiki iliyotoa huduma ya usafiri ili kuwashinikiza wahusika kugoma.

SOURCE: UHURU
 
Mkuu thatha.

Hapa Godbless Lema hausiki na hizi jitihada za mgomo tumtendee haki wahusika wakuu ni Nanyaro diwani wa Levolosi na kikundi chake cha wahuni ndiyo wahusika wakuu.Lema alikuwa uwanja wa ndege akiongoza ndege na kufungua matawi kwa wingi ahaaaaa.

Inteligensia ya masaburi. Twiga wanaibwa hapo kiwizi hamjagundua ila tu Nanyaro ndo umemjua. CCM haiponi imelaaniwa tayari!
 
Inabidi tuwe makini na vichwa vya habari tunavyo andika, Kugeuza mtandao kama gazeti ambalo linaandika kichwa cha habari kuuzia gazeti nafikiri hapa sio mahali sahihi.

Sorry nimepita tu.
 
SAKATA la kukamatwa na kushitakiwa kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, limeingia katika hatua ngumu baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kufungua jalada la uchunguzi dhidi ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Zuberi Mwombeji, kuhusiana na madai ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alisema jana kuwa sambamba na kuchunguza kauli hiyo, jalada hilo pia litachunguza makosa yanayodaiwa kutendwa na Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.

"Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyo hiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote," alisema Kamanda Mpwapwa.

Wakati hatua hizo zikichukuliwa, taarifa za kuaminika zimebainisha kuwa watu waliojitambulisha kama askari wa Jeshi la Polisi walivamia nyumba ya kada maarufu wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Kata ya Kati, Rashid Shubeti na kumtishia kumtwanga risasi iwapo angetoka nje ya nyumba yake.

Shubeti akiongea na Tanzania Daima alisema kuwa watu hao walidai kuwa anahusika na kuendesha kampeni na kusambaza waraka unaowahamasisha wananchi kugoma, kushinikiza kuachiwa huru kwa Lema na wanachama wengine 18 wa chama hicho waliofunguliwa mashitaka kadhaa mahakamani.

Alidai kutokana na tishio hilo ametoa taarifa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, Leonard Paul, kuhusiana na kuvamiwa nyumbani kwake na watu wenye sialaha, huku akilitaka jeshi hilo kusimamia haki na uhuru wa wananchi badala ya kugeuka kuwa tishio kwa usalama wa wananchi.
Mgomo wa daladala na pikipiki

Jana katika hatua isiyokuwa ya kawaida, polisi iliwatia mbaroni zaidi ya watu 30 kuhusiana na kuandaa, kuhamasisha na kushiriki mgomo wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala (vifodi), ulioanza saa 2:00 asubuhi na kudumu hadi Saa 5:00 asubuhi.

Kaimu Kamanda Akilimali alisema watu hao walikamatwa kwa wakati na sehemu tofauti, baada ya polisi kupata waraka ulioandikwa na watu wasiojulikana kutangaza na kuhamasisha mgomo huo uliokuwa na malengo makuu matatu, ikiwamo kupinga na kulaani kauli ya OCD kuwaita wananchi mapanya.

Mgomo huo uliodhibitiwa na Jeshi la Polisi walioingilia kati kutawanya makundi ya vijana waliojitokeza kuwashambulia madereva waliokaidi kushiriki, pia ulilenga kulaani na kupinga udhalilishaji na ukatili wa Jeshi la Polisi.

Washiriki wa mgomo huo pia walikusudia kufikisha ujumbe kwa watendaji serikalini kuacha ukibaraka, udhalilishaji na unyanyasaji dhidi ya raia. Hadi jana jioni viongozi mbalimbali walikuwa wakiendelea na harakati za kuhakikisha mgomo huo unadhibitiwa.
Oktoba 28, mwaka huu, akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha katika kesi ya kupinga ushindi wa ubunge wa Lema, iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa CHADEMA kuwa mapanya.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya kesi hiyo kuahirishwa kutokana na wananchi kujazana kupita kiasi ndani ya ukumbi wa mahakama kiasi cha mawakili wa pande zote za walalamikaji na utetezi kumuomba Jaji Aloyce Mjuluzi kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kufungwa vipaza sauti ili wanaokosa nafasi ndani ya mahakama wasikilize mwenendo wa kesi wakiwa nje.
Polisi wadhibiti njia ya kwenda magereza

Katika hatua nyingine, polisi jana waliweka ulinzi mkali huku wakiwazuia na kuwahoji watu wote waliokuwa wakielekea njia ya Kisongo liliko gereza kuu la Mkoa wa Arusha kudhibiti wanachama, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA, waliokuwa wakimiminika kwa wingi kwenda kumtembelea gerezani Mbunge Lema katika utaratibu wa kawaida wa wafungwa na mahabusu kutembelewa Jumatano, Jumamosi na Jumapili.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walifanikiwa kupenya kupitia njia za uchochoroni na kufika gerezani, ambapo walikumbana na kizingiti kingine cha askari magereza waliodai hawaruhusiwi kumwona Lema kwa sababu tayari idadi ya wanaoruhusiwa kumtembelea imekamilika.

Ofisa Magereza mwenye cheo cha mkaguzi msaidizi, aliyevaa beji yenye jina la J. Mmari, aliyekuwa akizungumza na wananchi hao kwa niaba ya mkuu wa gereza, alisema sheria inaelekeza kuwa siku ya Jumatano wanaoruhusiwa kumtembelea mtuhumiwa ni mawakili wake na wageni wasiozidi watatu, lakini kwa busara uongozi wa gereza uliamua kuruhusu watu zaidi.

"Mpaka sasa walioingia kumuona Lema wamezidi na hatuwezi kuendelea kuruhusu kwani tangu saa 2:00 asubuhi mheshimiwa ametembelewa na idadi kubwa ya watu ambapo ameongea kwa zaidi ya dakika moja na kila kundi.

Tafadhalini wengine njooni Jumamosi na Jumapili," alisema Mmari. Hata hivyo alibainisha kuwa hata siku hizo ambazo ni maalumu kwa mahabusu na wafungwa kutembelewa, miundombinu na sheria ya magereza haiwezi kuhimili idadi kubwa ya wanaojitokeza kumtembelea Lema.

Kauli hiyo iliamsha jazba na hasira za vijana walioanza kutoa maneno makali na kumlazimu Mwenyekiti wa Bavicha wa Wilaya ya Arumeru, Joshua Nassari, kuwatuliza.
Lema aipa serikali saa 48

Jijini Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa ikisema kuwa Lema ameipa serikali saa 48 kutekelezwa matakwa yake ili aweze kutoka gerezani.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Erasto Tumbo, amewaambia waandishi wa habari kuwa mbunge huyo ametoa masharti matatu ya kutoka gerezani ikiwa ni pamoja na Polisi kufuta shitaka walilomfungulia la kufanya maandamano bila kibali na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kumwondoa OCD wa Arusha, Zuberi Mwombeji, ambaye anadaiwa kuwa chanzo cha vurugu.

Kipengele kingine ambacho Lema ametaka kitekelezwe ni serikali kuunda tume aliyoahidi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambayo itawajumuisha wajumbe kutoka CHADEMA na CCM, ili kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa meya.

Hata hivyo, hakusema nini kitafuata iwapo serikali itashindwa kutimiza masharti hayo kwa muda alioutoa.

Tumbo aliongeza kuwa CHADEMA kinaunga mkono kwa asilimia 100 hatua zilizochukuliwa na mbunge huyo ambazo zina lengo la kudai haki kwa wananchi wanyonge na wapenda maendeleo na kwamba Polisi wamekuwa wakifanya kazi zao kwa matakwa ya chama cha siasa.

"Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana Polisi imeendeleza zoezi la kamata kamata kwa viongozi wa CHADEMA kwa lengo la kudhoofisha harakati za chama hicho kisiasa," alisema.

Tumbo alidai kuwa kesi ambazo zimekuwa zikifunguliwa na Polisi kwa viongozi wa CHADEMA ni dalili tosha kuwa jeshi hilo linatekeleza maagizo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba hawatakuwa tayari kukubali tena kunyanyaswa.

Lema alikataa kuwekewa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha chini ya Hakimu Judith Kamala na kulazimika kwenda rumande katika Gereza la Kisongo kwa muda wa siku 14, ambako ameendelea kusota hadi leo, japo washitakiwa wenzake 18 waliachiliwa kwa dhamana.

[TD="bgcolor: #ffffff"]
Lema awasha moto
• Daladala zasitisha huduma, maduka yafungwa

na Peter Saramba na Mussa Juma, Arusha

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
[/TD]

NA SHAABAN MDOE. ARUSHA
NJAMA za mbunge wa Arusha Mjini Gogbless Lema (CHADEMA) kushinikiza mgomo wa daladala na pikipiki , ikiwa ni ishara ya kupinga kuwekwa rumande, zimegonga mwamba , baada ya wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri kutomuunga mkono.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinasema wamiliki wa vyombo hivyo waliamua kutounga mkono mgomo huo , baada ya kutafakari na kuhoji mantiki yake kwa kuwa dhamana ulikuwa wazi kwa Lema lakini alikataa kudhaminiwa ili apelekwe rumande.

Jana asubuhi vijana waliosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Lema walifanya vurugu kwa kupiga mawe kila daladala na pikipiki iliyotoa huduma ya usafiri ili kuwashinikiza wahusika kugoma.

SOURCE: UHURU

Dawa yenu David Cameron..... anayetaka muolewe ndo mchapishe gazeti.....!!!
 
Mkuu thatha.

Hapa Godbless Lema hausiki na hizi jitihada za mgomo tumtendee haki wahusika wakuu ni Nanyaro diwani wa Levolosi na kikundi chake cha wahuni ndiyo wahusika wakuu.Lema alikuwa uwanja wa ndege akiongoza ndege na kufungua matawi kwa wingi ahaaaaa.

Unao ushahidi dhidi ya madai yako kwa nanyaro? Au una bwabwaja tuu ili uonekane.
 
Mkuu thatha.

Hapa Godbless Lema hausiki na hizi jitihada za mgomo tumtendee haki wahusika wakuu ni Nanyaro diwani wa Levolosi na kikundi chake cha wahuni ndiyo wahusika wakuu.Lema alikuwa uwanja wa ndege akiongoza ndege na kufungua matawi kwa wingi ahaaaaa.

Ngongo, unaubaya gani na Mh Nanyaro?unaonyesha unayo chuki mbaya sana kuliko hata Chuki ya Kikwete na Seya.
 
Kama ni uhuru taarifa niya Kichina teyari
 
Lema anatuaibisha wanachadema wa Arusha..
Afadhali wamiliki wa vyombo vya usafiri wameliona hilo.
 
Back
Top Bottom